Ukiwa mtumishi wa umma hakikisha kila wiki unatengeneza fedha sawa na mshahara wako wa mwezi mmoja

Ukiwa mtumishi wa umma hakikisha kila wiki unatengeneza fedha sawa na mshahara wako wa mwezi mmoja

Kwamfano mualimu grade A mwenye mshahara wa 370,000 mwenye familia ya watoto wawili na mke anae hitajika kazini kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 jioni afanye ujasiliamali gani
hapo bado hajakopa benki halaf mipango haikwenda sawa na salary slip isome 200,000 bado kuna madeni ya vikoba...
 
Serikali Haina muda na watumishi wa umma.Mugufuri ndiye aliye waharibia maisha kwa kutowapandishia mishahara wakati wote wa utawala Wake wa kutofuata katiba ya nchi.
 
Utapata tu mke mwenye shida zaidi na za kwako hamna mwana mke mzuri mwenye wazazi wanao juelewa anaruhusu mwanae aolewe na mualimu mwenye mshahara wa 370,000 kwa mwezi manaake hamwezi kuvaa nguo mpya viatu vipya au kuenda holiday nyumbani ni ugali mboga za majani au maharage, nani avumilie hizo shida.......labda uwe singo maza wa wstoto zaidi ya moja ila sio pisi kali.
Ahahahah
 
Huu ni ushauri tu kwa watumishi.
Kutokana na kupigwa na vitu vizito kichwani kama vile Sheria mpya za kikokotoo, na danadana za ongezeko la mshahara pamoja na serikali kushindwa kukopesha watumishi wake bila riba au kwa riba isiyozidi 5% napenda kuwashauri watumishi wa umma wahakikishe chini juu kila wiki wafunge na hesabu ya mshahara wa mwezi mmoja.

Kama unalipwa laki 8 basi kwa mwezi makusanyo yako nje ya mshahara yagote 3.2 ml.

Kama mshahara wako laki 6 basi ikimbize milioni 2.4.

Kama mshahara wako ni milioni 1 basi ikimbize milioni 4 ndani ya mwezi.

Hii itakusaidia kujipanga na maisha baada ya kustaafu.

Hii itakusaidia pia kuishi kwa furaha wewe na familia yako kama wanavyoishi wanasiasa.

Utaipata wapi hiyo Mimi hainihusu.

Hakikisha tu unaingiza 400% ya mshahara wako kila mwezi.

Kuna Mzee mmoja kastaafu mwaka mwezi Machi.

Anazimia hovyo hovyo, sukari imepanda , pressure imepanda. Kikokotoo kimemkokotoa. Kama angekuwa makini kwenye biashara za ujasiriamali asingefikia huko.

Fanyeni ujasiriamali watumishi 😭😭😭😭.
Nimependa ushauri wako mdau, ubarikiwe sana sana.
 
Back
Top Bottom