Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Nmewai kiu true,nmewahi kaanga injini Kwa kuuziwa castrol oil feki, Tena toka Kwa dealer, akiniaminisha inatembea kilometers nyingi kuliko oil za kawaida

Nmeskia milio ya ajabu nikapuuza eti kisa nmemwaga oil juzi juz TU hapa.

Aisee, nilinunua mswaki
 
Likijaga swala la oil kubadirisha naogopa. Bora Total na Puma uhakika ila hizi nyingine haujui ipi fake ipi original.
 
Mmh turbo inafunguka mapema tu sio hadi ufike 100 sio kweli,hata ukipaki ukiikanyagia utaisikia tu.
Zingatia neno kukanyagia.

Inaweza kufunguka wakati wowote kama unavyosema lakini ukihitaji nguvu ya mwendo zaidi lazima ifunguke. Kuna Ile gari unaongeza mwendo taratibu Hadi kufikia speed kubwa na Ile unataka uipeleke mbio Kwa haraka. Hapo ndio kwenye kiini Cha post yangu.
 
Waelezee pia hizo battery Zina expire na kufanyia replacement inaweza kuku kost 16m anbayo ni hiyo hiyo uliyoisave kutokununua mafuta.

Mwambie kuwa asipobadili battery ikiwa imeshachoka haikawii kuoverheat na kuwaka moto..

Ajue Pia na masaa ya kucharge had iwe full.. asifikir nusu saa tu.. anaweza akacharge kuanzia 3 hrs had 24 hrs kutegemea na uwezo wa charger na ubora wa battery maana anasema dodoma na kurudi.. labd akama ana nyumba huko dodoma wamefunga EV charger au anafikiri unachomeka tu kwenye socket za umeme na umeme wenu wa bongo huu sio Msafi

Kifupi EV ni cost effective kwenye swala la mafuta.. ila ili uifaidi hakikisha umepata mpya na kaa nayo ndani au chini ya miaka 3 uza. Na isiwe ndo gae ya kauka nikuvae . sasa ww uingize second hand EV bongo tayar battery yake inasoma 75% ya uwezo wake.. ukikaa nayo mwaka halafu ndo kauka
Nikuvae Hapa battery inaweza ikakusomea 50% kureplace hiyo battery achilia mbali bei yake ila kama hawajafanya wenyewe au certified agent hiyo ni warrant void..

choice nzur ni hybrid.. na siku hz ziko option tofaut za hybrid kuna ambayo ukiendesha kwenye speed ya 50 ama
Chini ya hapo au ikiwa idle unatumia Umeme ukizidisha juu ya hapo ndo ina engage kwenye engine ya mafuta.. na wakat huo huo inacharge battery... yaan ukiwa unaenda mkoa unatumia mafuta ukiwa misele ya town umeme tu.. toyota wanazo, nissan wanazo
 
Teknolojia inakua after 10 years mambo yatakua yameboreshwa mara dufu
 
We jamaa unatoa elimu ya magari utafikiri umezaliwa na nagari nasio binadamu.
 
Umeongea madini mkuu, ila nyingine ni nadharia pia umeongea. Hope tunajifunza wote.

1. Swala la kuchoka kwa battery (degradation) ni kweli, kama simu au hybrid cars, battery lazima ziishiwe nguvu ya kuhold charge.

Lakini, Teknolojia ilipofikia battery unakuta lina life cycles hadi 1500 (mfano Tesla). Na life cycle moja ni kutoa chaji from 100% to 0% na ikiwa 100% lets say inasafiri kilometa 400.

So ili ichoke kabisa iwe ya kutupa inamaanisha ni kilometa 400 x 1500. Imagine.

Study zimeonesha EV nyingi zinapoteza wastani wa 1% ya kuhold charge kila mwaka.

2. Kuhusu kucharge tumeshadiscuss kwenye huu huu uzi.
Kama ulivyosema zinategemeana na charger iliopo. Level I ni ya nyumbani iko slow. Level II unaweza kuweka home au ukaikuta makazini. Level III ni DC charger iko fast ndio izo unakuta zipo kwenye masupamaketi.
 
Reactions: Lax

ni sahihi kabisa ulichoongea.. ila mimi nazungumzia kwa hapa kwetu bongo wa sasa hv tu a charging network sina hakika kama zipo za kutosha.. tuchukulie mtu anaamua kuingiza EV sasa hv na ndio anaofanya gari yake ya kilaSiku utaona changamoto zitakuwa kubwa ingawa ata save kwenye mafuta ila atajikuta gizo gharama alizosave kwenye wwse zinarudi indirect pengine za zaid maana atakuwa very limited kwenye safar zake kwa sababu zifuatazo

1. Location za kucharge na ubora/aina ya charging system - mpaka sasa hv hakuna universal charging sysytem ya kuelewwka hata huko dunian. Tesla ana mfumo wake manufacture wengine nao The same . So hapa maana yae uhakika ni kuchaji gar home tu.. maana kwenye public place ni lazima wahusika waone kama watafaidika hawawezi tu kufunga mfumo Huo ili mradi tu..sasa chukulia apate safar ya mkoan maana yake itabidi aipaki EV atafute means nyingine maana nje ya Morogoro kwingine hana uhakika wa kwenda na kurudi

Kuna aina ya life style ufanisi au tu get the best out of it unategemea na utayari wa mifumo wa nchi husika.. EV cars zimekuwa kwenye soko almost for 10+ years huko Ulaya, US na Asia na mpaka sasa hivi kuna debate kama Europe iko tayar ku phase out Engine cars ili kuimbrace EV .. US ameweka policy hadi 2030 wawe full EV ila changamoto ni nyingi..

Technology inakuwa na changamoto
Zinapaitiwa solution. ingawa sio kwa pace ya kufanya in The next 10 years wawe kwenye EV 100%

US consumers wana raise argument kuwa initiative iwe kwenye hybrid na sio full EV maana inaoneka kama nationalwide EV bado ziko kwenye kujitafuta.. hakuna supporting system ya EV nchi nzima.. kuanzia charging network.. gharama za kununua au kubadili battery ziko juu almost nusu ya thaman ya gari ilipokuwa mpya..

Changamoto nyingi zimesababisha EV ku depriciate haraka na hazihold value of Money kwa Mda mrefu hata bima za EV ni ghali kuliko za Engines cars..

The changes is inavitable ila upande wetu africa tusiharakishe.. kama itawachukua ulaya na US 10+ yrs kuweza kuwa comfortable na EV basi sie ni next 30+ years

Maana ss hv ukiwekeza kwenye EV basi uwe walau kipato chako cha mwez kiwe 10+m plus na hiyo iwe surplus tu.. ila vinginevyo mh
 
aisee!
 
Dah umeongea ukweli nadhani ndio wengi pia wanaogopa hii kitu, charging network.

Kuna mtu ana Prius Plughin Hybrid, ila amesema hajawahi ichaji ata siku moja na ata mwaka sahivi anayo, kwasababu ya network ya charges.

Kwa sasa kweli bora tukomae kwanza na Hybrids, zinasave vizuri tu bila complications nyingi.

Mfano badala ya kununua Tesla Model 3 ya 2020 ambayo naona beforward na ushuru jumla Mil 55+ bora maboss wanunue Prius 5th generation ya 2023 naona bei na kodi sawa.

Utapata range ya EV ya 10km ambayo ni tosha kabisa kwa hybrid na fuel consumption ya hadi 30km/L
 
Reactions: Lax

Yes sahihi kabisa tuanze na hybrid tu.. sema kibongo bongo inabidi ukiwa na hybrid uwe na mkangafu mmoja hv maana kipindi cha masika dar haieleweki posta unakuta maji ya magoti.. halafu uwe na hybrid prius maji yakipanda pale mbele kwenye motor kaz unayo
 
Mwakani 2025 Mungu akibless naishi na Prius 3rd generation, naona 4th bei ya moto sana siwezi ingawa ndani nzuri.

Nilitaka Honda Fit ila naona kaduchu sana ova Vitz.
 
Reactions: Lax
Mwakani 2025 Mungu akibless naishi na Prius 3rd generation, naona 4th bei ya moto sana siwezi ingawa ndani nzuri.

Nilitaka Honda Fit ila naona kaduchu sana ova Vitz.

Ila kwenye EV gari 3 katika entry level ndio zinasifika kwa durability Prius, FIt na Nissan leaf Ev ila prius na leaf zina nafas Fit kadogo

Ila hizo tatu naona Europe wanazisifia kuwa ni durable na battery perfomance ni nzuri
 
Reactions: Lax
Miezi kadhaa iliopita liliibuka wimbi la vi pikipiki vya umeme. Tafuteni wale watu wawape maendeleo ya vile vipikipiki vya kichina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…