Ukiwa na hizi tabia 9, jiandae kufa maskini wa kutupwa

Ukiwa na hizi tabia 9, jiandae kufa maskini wa kutupwa

_"Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu" (Nelson Mandela, R.I.P)_

_"Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio"(Mwl Nyerere, R.I.P)._

_"Kile unahokifanya muda huu ndicho kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako"(Mahatma Gandhi, R.I.P)_

_"Ukizaliwa maskini sio kosa lako, ila ukifa maskini hilo ni kosa"(Bill Gate, The richest man in the world)._

Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa, "mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini". Mpaka leo sijaelewa alimaanisha nini.

*Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo, uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na haya mambo 9 yafuatayo;*

*1. KUTOKUJARIBU.*
Katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. "Chagua kufa, au kupambana". "Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.

*2. KUTOKUJIFUNZA.*
Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima asome kitu kipya. "JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia, Hamasika.(Prof Jay)

*3. WOGA & WASIWASI.*
"Tunaweza tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa mchana"(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

*4. KUJILINGANISHA.*
Kuna baadhi ya watu, huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Usitamani kuwa Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu. Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi maisha yako yote.

*5. KUWEKA VINYONGO.*

"Kuweka chuki na konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine". Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.

*6. UONGO*
"Uongo utakupa ushindi wa siku moja, ukweli utaishi milele"(WEUSI), "Muongo hata akiongoea ukweli usimuamini"(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja. "Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati wote"(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi kuvificha.

*7. UVIVU & UZEMBE*
"Nyumba yenye njaa ukisizi unapata zero"(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya. Neno "kazi" katika biblia limeandikwa mara 600. Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila siku. We kwepa majukumu tu, kesho utakula magodoro. "Uvivu unalipa muda huu, bidii & juhudi vinalipa baadae".

*8. STAREHE & ANASA KUPINDUKIA*
Pombe, sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. "Sisi ni kile tunacho kula". Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako". Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. "Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana"(Nikki Mbishi,).

*9. LAWAMA & UMBEA*
"Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu" We upo kwenye kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la "wachawi". Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako.
Haya yote kwa kuyasoma ni rahisi,ngumu kuyatekeleza. Mengine hapa ni ya kurithi. Mfano, Uvivu! Unaweza kuta ukoo fulani watu wake ni wavivu kuanzia babu hadi wajukuu!
Hili ni somo zuri kwa watakaotaka kubadilika.
 
Nimefanya utafiti kidogo kwa kuchukua sample ya watu kama kumi hivi juu ya uhusiaano uliopo kati ya maisha ya ujana na uzee.

Nimegundua kuwa vijana wanaoshindwa kujidhibiti kwenye masuala ya uzinzi na ulevi huishia kwenye uzee mbaya.

Hii hasa inawahusu wale wenye kipato cha chini na kati na wale wenye kipato kikubwa hawaathiriki zaidi na hili.

Nimeona wengi sana waliochezea pesa kwa masuala ya uzinzi na ulevi wamekuwa na mwisho mbaya tena wengi nimewahoji na kufunguka bila haya.

Ukiona kila ukishika aidha million moja break ya kwanza bar unywe ndipo upate akili ufanyie nini ile laki tisa na point inayobaki basi usiwe na shaka tambua kuwa uzee wako unauroga wewe mwenyewe.

Umepata million kumi au tano break yako ya kwanza Lodge kwenye uzinzi, nakwambia kuwa wewe ni maskini au fukara ajaye.

Binafsi nimewahi kupata millioni moja mpaka kumi. Mimi nawafyeka mademu ila nikipata million moja, mbili, Tatu au zaidi huwa sipokei simu ya mchepuko mpaka pesa ikate kwenye mradi niliolenga kuiweka ndipo naanza kuwatafuta. Pombe siijui.

Mademu tawatafuta nikiwa na change kamili tu. Najua si ndugu zangu ndio maana usipowapa pesa hawana time na wewe.

Sijaandika hapa kwa lengo la kumhukumu mtu bali kutoa alert kwa atakayekubali kuonywa.
 
Mawazo ya kimaskini hayo tafuta connection ya pesa ndio utajua starehe na pesa ni mapacha,

Watu wana starehe na mipango inaenda na jamii zinawashangaa

Kuwa mwaminifu, heshimu watu na kazi za watu uone kama mambo hayaendi
Hao wanaipiga starehe na mambo yao yanakwenda basi kipato chao ni cha juu na kama kipato chao ni cha chini ni suala la muda tu, mishe zao zikikwama watageuka ombaomba maana account zitasoma zero.
 
Mawazo ya kimaskini hayo tafuta connection ya pesa ndio utajua starehe na pesa ni mapacha,

Watu wana starehe na mipango inaenda na jamii zinawashangaa

Kuwa mwaminifu, heshimu watu na kazi za watu uone kama mambo hayaendi
Final uzeeni.
 
Hao wanaipiga starehe na mambo yao yanakwenda basi kipato chao ni cha juu na kama kipato chao ni cha chini ni suala la muda tu, mishe zao zikikwama watageuka ombaomba maana account zitasoma zero
Sasa account kusoma zero unaona ajabu pengine nikuambie wapenda starehe wanatofautiana

1. Wapo wa mjini
2. Wapo wa mashinani vijijini
3. Wapo wa kileo
4. Wapo wa kizamani

Wapenda starehe wakileo awe was mjini au kijijini akipata pesa ndevu hukimbilia kwenye assert tena assert ambayo shida au tatizo likitokea hakuna shida kupata mteja na assert ya kileo na ya kisasa isiyo na kelele kuuza ni mifugo na mazao siyo nyumba wala viwanja au gari upo hapo, nyumba, gari au kiwanja unaitaji dalali na mda ila mfugo au mazao haitaji hiyo mambo ni kutamka tu nauza ng'ombe, mbuzi, mpunga au mahindi unafutwa MFA huo huo.

Kwaiyo account ikisoma zero unskimbilia store unarudi barabarani maisha yanaendelea.
 
Sandali Ali,

Mzee maisha hayoko rahisi hivo.Ila ni kweli uzinzi na ulevi una mwisho mbaya ila ndo starehe pekee ambazo zina value for money.
 
Sandali Ali,

Mkuu upo sahihi, yalinikuta hayo...nilipata pesa kama m 15 hivi at pa, zilikuwa dollar 10000 at that time.

Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa kupata tena na tena, zile pesa nilifanya kila aina ya starehe

Mungu si athuman, kuna matatizo yalijitokeza katika project yangu ile.

Nilikula msoto wa kufa mtu three years consecutively. Nilikumbuka kila kitu na kujilaumu sana na kuapa sitorudia

Nilipokuja kunyanyuka, mimi na anasa tofauti, nimekuwa na nidhamu ya pesa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tajiri na starehe ni pacha na pacha hakuna tajiri asiyekula starehe nenda kwenye kumbi zote classic za starehe utakuta watu wanapiga zao hennesy na kupeana michongo ya biashara mtu anatoka kula bia na michongo kibao tatizo maskini mnataka mlewe tu hakuna cha maana mnachoongea mnaishia kufulia.

Tafuta pesa mkuu' kakae na kula bata na wenzako uone story wanazopiga utakuja kujua starehe pia ni moja ya njia ya kutafuta pesa.
 
Back
Top Bottom