Ukiwa na mapesa unaweza kununua kila kitu, isipokuwa mambo haya

Ukiwa na mapesa unaweza kununua kila kitu, isipokuwa mambo haya

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
Ukiwa na Mapesa HUWEZI...

1️⃣ Kununua Wokovu – Wokovu wa Mungu haupatikani kwa fedha bali kwa imani katika Kristo Yesu. (Waefeso 2:8-9)

2️⃣ Kununua Amani ya Moyoni – Amani ya kweli inatoka kwa Mungu. (Yohana 14:27)

3️⃣ Kununua Upendo wa Kweli – Upendo wa dhati haupatikani kwa pesa. (1 Wakorintho 13:4-7)

4️⃣ Kununua Furaha ya Kudumu – Furaha ya kweli inatoka kwa Bwana. (Zaburi 16:11)

5️⃣ Kuongeza Muda wa Maisha Yako – Kama Mungu amekusudia uishi muda wa sekunde 1,576,800,000, hata ukiwa billionaire kama Musk, huwezi kununua hata sekunde moja zaidi ya muda huo. (Luka 12:25). As of Feb 2025, Elon Musk's net worth is estimated at approximately $397.4 billion

6️⃣ Kununua Heshima ya Kweli – Heshima ya kweli hupatikana kwa kuwa na tabia njema, si kwa kuwa na mapesa. (Methali 22:1)

7️⃣ Kurudisha Uhai wa Mpendwa Wako – Pesa haziwezi kurudisha maisha ya wapendwa waliotangulia mbele za haki. (Mhubiri 3:1-2)

8️⃣ Kununua Baraka za Mungu – Baraka za kweli haziwezi kununuliwa kwa mapesa, bali hutolewa na Mungu kwa neema. (Mithali 10:22)

💡 Tafuta Pesa kwa Bidii: Pesa ni muhimu, lakini tusidanganyike, mambo yenye thamani ya milele hayawezi kununuliwa kwa mapesa. Nope!

Ubarikiwe! 🙏
 
Money is a valuable tool, but it is not everything, as demonstrated by the eight points in the post. Whoever loves money never has enough; whoever loves wealth is never satisfied(Ecclesiastes 5:10)
Kwa ambao wamewahi shika pesa za kutosha ama ambao wanapesa tayr, wanakuelewa point Yako, ila Hawa masikini wa jf hawawezi kukuelewa mkuu
 
Wewe endelea kuzitafuta tu, kuna kitu zitakupa
Sawa, naendelea kuztafuta; ila najiepusha nisiingie katika "mtego" wa kupenda pesa

"Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi."(1 Timotheo 6:10 BHN)
 
Back
Top Bottom