KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Uongo mtakatifu,
Nina songesha hapa na nimepata mkopo nmb, na crdb,
Kwanza uelewe mikopo inakatiwa BIMA,
acha kudanganya watu
 
Yaani niende NMB leo naomba milioni 17 salaried loan wanigomee kisa nina mkopo songesha wa elfu 80😁😁.

Kama ni mfumo imara kabisa na ni lazima kuufanyia kazi basi,itakuwa inalazimika kulipishwa deni husika kupitia mkopo mpya(top up like),kuliko kugoma kabisa kutoa mkopo,hakuna benki imejaza mbulumundu itakubaliana na mfumo huo utakaosababisha kukosa wateja kijinga jinga tu.

Mfumo wa marejesho ya mikopo ya bank kwa mishahara sio wa hiyari,ukiishachukua hela unakatwa kwa lazima,hiyo high risk alart haina maana kabisa hapo kwa wazee wa hazina.
 
Mie nilisafiri kwenda nje ya nchi na mkopo wa kamilisha elfu42 na nina miezi mitatu sijarudi.

Nikirudi sijui itakuwa je.
 
Kwahio Mwigulu alivyopiga mkwara kumbe hakua na taarifa Sahihi? Duh
 
Ngozi nyeusi shida sana
 
Ngozi nyeusi shida sana
ngozi nyeusi janjajanja sana[emoji1787]sio msomi sio ngumbaru ukizubaa kidogo anakupiga kitu kizito.

nliona kwa wasomali uaminifu ni mtaji muhimu sana yani wakigundua mmojawao ni mpigaji wanaweza hata kumuondoa maana anawaharibia wengine wote.
 
Uongo mtakatifu,
Nina songesha hapa na nimepata mkopo nmb, na crdb,
Kwanza uelewe mikopo inakatiwa BIMA,
acha kudanganya watu
Kama mlipaji mzuri hakuna shida watakupa tu hata ukope benki na mitandao yote na benki zote

Kimbembe kinakuja kama sio mlipaji mzuri popote ulipokopa iwe songesha nk

Hapo Wanakushughulikia kikamilifu.
 
Waliozoea kudhulumu au kutolipa wakibanwa huona wameonewa.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…