KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Halafu wanazinguwa kama m pawa unaweza kukopa miezi minne na unalipa kwa wakati lakini hawaongezi kiwango cha mkopo.
 
Nina hakika mabenki yanayo tegemea faida kwa kukopesha watumishi yatapoteza wateja wengi mnoo. Maana kiukweli asilimia kubwa wana vimikopo walivyo default.

Jana nilikuwa benk ya CRDB,wanasema maombi ya wateja wapatao 10 kwa ajili ya mikopo yamekataliwa na system kwa sababu ya udaiwa sugu. Yule loan officer alikuwa anasikitishwa na hyo Hali na akawa anasema wanafanya communication na makao makuu ili waachie tu hyo mikopo.
 
Hii ni fursa nzuri kwa vi microfinance pia mitaani. Maana kiukweli kwa huu mfumo watumishi wengi watakosa sifa ya kukopesheka benki..
 
Nawashauri wale ambao hamjaingia Kwenye hili jini SONGESHA msijalibu mbeleni litawaleta shida
Kama si mwaminifu wa kurejesha mkopo wao lazima wakublack list.

Nimekaa na Airtel money vizuri kwa miaka kadhaa, Sasa wananiamini wanaweza kunikopesha hadi 1.6 m bila shida. Kaeni vizuri na wanaowakopesha kwa kuwa waaminifu na kulipa deni kwa wakati mliokubaliana.
 
Mkuu tafakari vizuri, hapo muhuni ni wewe ambaye umeshindwa kulipa kwa wakati. Mkopo sio zawadi, lipa kwa wakati ujiwekee heshima
 
Hiyo ndio Hali halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…