KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wengi wetu tunafikiri mikopo ya mitandao ya simu kwa sababu huwa hawataki vielelezo vingi zaidi ya namba za NIDA tulizosajilia basi mtu anaweza akakopa halafu akawakimbia kwa kuhama line.

Lakini wao walishalijua hili mapema so inaonekana walipoenda kuomba license ya kufanya hii biashara waliomba pia wawe na uwezo wa kuingilia taarifa binafsi za wateja wao kwenye mizunguko yao ya fedha nje ya mitandao yao ili inapotokea mteja kukosa uaminifu kwao wawe na uwezo wa kuzishawishi taasisi nyengine zizuie mikopo watakapoenda kuwakopa mpaka watakapowalipa na hili linafanikiwa kwa sababu ya namba za NIDA tulizosajilia.

Ukienda popote kukopa wakiingiza ID card # yako kama una kimeo unawekwa uchi,na ukweli ktk hilo wamefanikiwa sana nimemsoma mdau mmoja humu asubuhi akilalamika songesha ya 5K imemfanya awe na sifa ya kutokopesheka hata alipoilipa still akaonekana ni mzigo hakopesheki,nadhani wanatumia ile kanuni ya ”ukikosa uaminifu kwa kitu kidogo huwezi kuwa muaminifu na kitu kikubwa”
Hahaha...........bora kama wamefanya hivyo, maana Vijana wasio waaminifu wamekuwa wanakopa na kuvunja laini zao 🙌
 
Changamoto Mkuu unalipa lakini Bado wamekuweka Kwenye High risk ,Wakati umeshalipa ,na hata kama ulikuwa unalipa mda umeenda wanakupiga risk Kwenye kukopa bank
Sidhani kama unalipa on time haiwezekani mikopo ya mitandaoni wakakuweka kwenye kundi la Risk ni kitu hakiwezekani
 
Hahaha...........bora kama wamefanya hivyo, maana Vijana wasio waaminifu wamekuwa wanakopa na kuvunja laini zao 🙌
Mjinga anavunja laini wakati mikopo rekodi ziko benki Sio kwenye line zimekuwa linked na kitambulisho Cha taifa kilichosajili laini ya hiyo Namba ya simu hata akivunja atupe line chooni deni liko pale pale Kwa laini iliyosajiliwa Kwa NIDA

Vitambulisho vya NIDA vilianzishwa kupambana na matatizo mojawapo likiwa Hilo la wakopaji kwenye mitandao

Watu wasiojua maana ya kitambulisho Cha NNIDA watajua
 
Waache tamaa
 
Kama hili halipo basi ni hatari sana na pengine wamechelewa tu kunganisha. Kwenye mikopo, inatakiwa system iliyokuwa intergrated, yaani ukitaka kukopa institution A, wawe na uwezo wa kuona kama umeshakopa au una mkopo sehemu nyingine zote zinazokopesha. Bila kuwa na uwezekano wa namna hii, mtu mmoja anaweza kukopa sehemu nyingi na akakimbia na fedha. Ndiyo maana nchi zilizoendelea kuna kitu kinaitwa credit rating, yaani ni namna ya kuonyesha mkopaji ni mtu wa aina gani, ana mikopo mingi? Ana tabia ya kulipa madeni?
Vodacom, tigo sio makampuni ya kukopesha, wanShirikiana na bank kufanya hili, ukikopa usipolipa ni umeiibia bank husika.
 
Waache tamaa
Kwa hiyo unavunja line Wakati ulikubaliana masharti kabla ya kukopa ikiwemo riba

Ulikuwa unagonga tu accepted au nakubali husomi Yale masharti

Hawakopeshi kijinga Wewe ndie mwenye tamaa ukiwinda pesa iingie utokomee gizani

Kabla kukukopesha mkeka wa masharti unakuja na unaukizwa unakubali wewe unasema ndiyo

Kukopa Harusi kulipa matanga
Utakoma Ndipo utajua wakopeshaji mitandaoni sio wajinga kama wewe
 
Hatulipi ng'o hata mje na nini?
Kwanza mnariba sio rafiki, pili mnadanganya wateja
Boss, huu ujanja ni suala la muda tu utakomeshwa na mifumo. Itafika kipindi jina likiandikwa IFAC mpaka bili za hospitali zilizokimbiwa zinaonekana. Sasa hivi bado Saccos na Microfinance uchwara ndo hazijawa link na CRB, ila huko mbeleni ukikopa utalipa tu au hutokopa tena.
 
Sidhani kama unalipa on time haiwezekani mikopo ya mitandaoni wakakuweka kwenye kundi la Risk ni kitu hakiwezekani
Kama hulipi inaingia. Tena ina sifa mbaya zaidi iwapo una vimikopo vya kijinga jinga vingi usivyovilipa. Unaweza omba ripoti yako ya CRB uone mkeka unavyofanana.
 
Mjinga anavunja laini wakati mikopo rekodi ziko benki Sio kwenye line zimekuwa linked na kitambulisho Cha taifa kilichosajili laini ya hiyo Namba ya simu hata akivunja atupe line chooni deni liko pale pale Kwa laini iliyosajiliwa Kwa NIDA

Vitambulisho vya NIDA vilianzishwa kupambana na matatizo mojawapo likiwa Hilo la wakopaji kwenye mitandao

Watu wasiojua maana ya kitambulisho Cha NNIDA watajua
That's huge improvement

Wamebakiza kulink vitambulisho vya Nida/Leseni ya udereva/Kadi ya mpiga kura/Pasi ya kusafiria n.k
 
SONGESHA na MIKOPO mingine ya simu imepelekea watumishi KUNYIMWA mikopo WAnapoenda bank kukopa, na hii ni kutokana na mamlaka zinazosimamia mikopo kuweka utaratibu wa madaraja high risk,risk na low risk katika kadiri mteja anaposongesha.

Hilo limetokea Leo Mimi mwenyewe nilipoenda bank na kuingia Kwenye mfumo wa ess utumishi, bank walivyoingia na kutumia mkopo ukawa rejected,nikaenda voda nikawalipa SONGESHA yote lakini Bado mfumo ulisoma high risk.

Nawashauri wale ambao hamjaingia Kwenye hili jini SONGESHA msijalibu mbeleni litawaleta shida

Mamlaka zinasimamia Mikopo hili LA simu hasa Mikopo ya nivushe, SONGESHA, Gold, bustisha ziwe na term of condition, Yani taratibu za mwanachama kukubali
Chai
 
Mkuu kama hilo limetokea itakuwa ni vibenki vya vichochoroni. Nina ushahidi usio tia shaka kuwa hizi benki kubwa zote hazifanyi huo ujinga. Hawawezi kukunyima mkopo kwa sababu unadaiwa na mitandao ya simu. Nina mifano hai ya watu watatu wanaodaiwa na kampuni moja ya simu na wamechukua mikopo benki, tena mmoja wao ilikuwa ni mwezi uliopita tu
Yaani unadaiwa 150K na kampuni ya simu alafu unataka kukopa 10M au zaidi benki, then wakunyime!!!. Na huyo jamaa alichukua mkopo benki na hajalipa 120K anayodaiwa na kampuni ya simu, na laini bado anaitumia.
 
Back
Top Bottom