Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 16,096
- 49,651
Umesema sahihi Mkuu, ndiyo maana una nafasi ya kutambua namba zilizosajiri Kwa kitambulisho chako.Hili ni janga zaidi kwa wale wanaowasajilia line ndugu jamaa na marafiki zao.
Unamsajilia mtu line na haya maisha yetu ya utafutaji leo umehama au yeye amehama mkoa anaenda anaitia kwenye kausha damu siku imepotea uwezo wa kui-renew hana anatafuta mtu mwengine anamsajilia nyingine huku nyuma line aliyoisongeshea msala unabaki kwako siku umepata shida ukijijua kabisa kwamba wewe ni msafi unakopesheka unashangaa unakutana na muhuri mwekundu madai umekuwa mdaiwa sugu,ukimpigia jamaa akupe ABCs ya kilichokuwa kinaendelea humpati.
Jioni hii nilikuwa nazungumza na jamaa yangu yupo Airtel akaniambia line zote zilizokopewa zikitoweka hewani iwe kwa bahati mbaya (kupotea /mmiliki kufariki) au kwa makusudi (kuzimwa/kuvunjwa baada ya kukopa pesa au salio) hazitagawiwa kwa mtu mwengine kama ilivyo kawaida hata kikipita kipindi cha siku 90 (miezi mitatu) mpaka itakapojulikana hatma ya wamiliki wake nini kimewakuta,jamaa wameamua kukomaa.
Ukiona vipi kazifungie