KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hahaha...........bora kama wamefanya hivyo, maana Vijana wasio waaminifu wamekuwa wanakopa na kuvunja laini zao 🙌
 
Changamoto Mkuu unalipa lakini Bado wamekuweka Kwenye High risk ,Wakati umeshalipa ,na hata kama ulikuwa unalipa mda umeenda wanakupiga risk Kwenye kukopa bank
Sidhani kama unalipa on time haiwezekani mikopo ya mitandaoni wakakuweka kwenye kundi la Risk ni kitu hakiwezekani
 
Hahaha...........bora kama wamefanya hivyo, maana Vijana wasio waaminifu wamekuwa wanakopa na kuvunja laini zao 🙌
Mjinga anavunja laini wakati mikopo rekodi ziko benki Sio kwenye line zimekuwa linked na kitambulisho Cha taifa kilichosajili laini ya hiyo Namba ya simu hata akivunja atupe line chooni deni liko pale pale Kwa laini iliyosajiliwa Kwa NIDA

Vitambulisho vya NIDA vilianzishwa kupambana na matatizo mojawapo likiwa Hilo la wakopaji kwenye mitandao

Watu wasiojua maana ya kitambulisho Cha NNIDA watajua
 
Waache tamaa
 
Vodacom, tigo sio makampuni ya kukopesha, wanShirikiana na bank kufanya hili, ukikopa usipolipa ni umeiibia bank husika.
 
Waache tamaa
Kwa hiyo unavunja line Wakati ulikubaliana masharti kabla ya kukopa ikiwemo riba

Ulikuwa unagonga tu accepted au nakubali husomi Yale masharti

Hawakopeshi kijinga Wewe ndie mwenye tamaa ukiwinda pesa iingie utokomee gizani

Kabla kukukopesha mkeka wa masharti unakuja na unaukizwa unakubali wewe unasema ndiyo

Kukopa Harusi kulipa matanga
Utakoma Ndipo utajua wakopeshaji mitandaoni sio wajinga kama wewe
 
Hatulipi ng'o hata mje na nini?
Kwanza mnariba sio rafiki, pili mnadanganya wateja
Boss, huu ujanja ni suala la muda tu utakomeshwa na mifumo. Itafika kipindi jina likiandikwa IFAC mpaka bili za hospitali zilizokimbiwa zinaonekana. Sasa hivi bado Saccos na Microfinance uchwara ndo hazijawa link na CRB, ila huko mbeleni ukikopa utalipa tu au hutokopa tena.
 
Sidhani kama unalipa on time haiwezekani mikopo ya mitandaoni wakakuweka kwenye kundi la Risk ni kitu hakiwezekani
Kama hulipi inaingia. Tena ina sifa mbaya zaidi iwapo una vimikopo vya kijinga jinga vingi usivyovilipa. Unaweza omba ripoti yako ya CRB uone mkeka unavyofanana.
 
That's huge improvement

Wamebakiza kulink vitambulisho vya Nida/Leseni ya udereva/Kadi ya mpiga kura/Pasi ya kusafiria n.k
 
Chai
 
Mkuu kama hilo limetokea itakuwa ni vibenki vya vichochoroni. Nina ushahidi usio tia shaka kuwa hizi benki kubwa zote hazifanyi huo ujinga. Hawawezi kukunyima mkopo kwa sababu unadaiwa na mitandao ya simu. Nina mifano hai ya watu watatu wanaodaiwa na kampuni moja ya simu na wamechukua mikopo benki, tena mmoja wao ilikuwa ni mwezi uliopita tu
Yaani unadaiwa 150K na kampuni ya simu alafu unataka kukopa 10M au zaidi benki, then wakunyime!!!. Na huyo jamaa alichukua mkopo benki na hajalipa 120K anayodaiwa na kampuni ya simu, na laini bado anaitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…