KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Si kweli hata kidogo, labda ungesema baadhi ya hivyo vibenki uchwara vilivyoingia ubia na makampuni ya simu
 
Nadaiwa mgodi, songesha,mpawa ,salary advance na mkopo nimevuta.... Acha ulaghai .....
 
Ni CRDB? Maana ndo wameanza kufanya hivyo
CRDB na NMB ni kama umechukua salary advance ukahamisha mshahara ndio wanakuripoti hiyo imemkuta mshkaji mi sikuhamisha mshahara na salary advance nilichukua ...na nikaprocess mkopo CRDB hata siku haikuisha imo..... Ila madeni ya mitandao ya simu sio kweli....
 
Hahaha...........bora kama wamefanya hivyo, maana Vijana wasio waaminifu wamekuwa wanakopa na kuvunja laini zao 🙌
Hili ni janga zaidi kwa wale wanaowasajilia line ndugu jamaa na marafiki zao.

Unamsajilia mtu line na haya maisha yetu ya utafutaji leo umehama au yeye amehama mkoa anaenda anaitia kwenye kausha damu siku imepotea uwezo wa kui-renew hana anatafuta mtu mwengine anamsajilia nyingine huku nyuma line aliyoisongeshea msala unabaki kwako siku umepata shida ukijijua kabisa kwamba wewe ni msafi unakopesheka unashangaa unakutana na muhuri mwekundu madai umekuwa mdaiwa sugu,ukimpigia jamaa akupe ABCs ya kilichokuwa kinaendelea humpati.

Jioni hii nilikuwa nazungumza na jamaa yangu yupo Airtel akaniambia line zote zilizokopewa zikitoweka hewani iwe kwa bahati mbaya (kupotea /mmiliki kufariki) au kwa makusudi (kuzimwa/kuvunjwa baada ya kukopa pesa au salio) hazitagawiwa kwa mtu mwengine kama ilivyo kawaida hata kikipita kipindi cha siku 90 (miezi mitatu) mpaka itakapojulikana hatma ya wamiliki wake nini kimewakuta,jamaa wameamua kukomaa.
 
Inaweza ikawa ni bahati yako au tawi walilokuhudumia hawaja-update bado system zao ili ku-copy na sheria mpya zilizoingizwa (tukumbuke haya malalamiko yameanza leo so labda ni sheria imeanza kutumika kuanzia jana au juzi).

Haiwezekani kila mtu analalamika kutakuwa na tatizo mahali.
 
Laini akipewa mtu mwingine huwezi kudaiwa?
 
Unataka kusema Mteja wa Vodacom Songesha anaweza kuwa na Deni linaloweza kuathiri kukopeshwa na Benki?

Kivipi jambo hilo likahusiana?
Huo mkopo iliutoa ni benki. Voda ni mlipaji na mpokeaji wa rejesho. Hivyo jina lako lipo kwenye vitabu vya benki x. Kalipe na usipolipa utaonekana were mifumo kuwa sio mteja mzuri
 
Yaani bank wakatae kula hela ya mtumishi 200k kwa mwezi kisa alikopa 20k Songesha? We utakua haukopesheki.
Maswala ya mikopo chechefu ni very sensitive.

Zamani benki zilikuwa na uwezo wa kuhesabu mkopo chechefu kama "hasara" kwa benki i.e inapunguza faida i.e inapunguza mzigo wa kodi. Baada ya kuja database ya taarifa za wateja, benki kabla ya kutoa mkopo ni lazima wapitie huko kwanza kujiridhisha kuhusu tabia za mkopaji. Ikitokea bank wametoa mkopo either kwa kutoangalia au kutozingatia taarifa za database, na huo mkopo ukashindwa kulipika; imekula kwa bank.
 
Hiyo benki ni wapumbavu kabisa.Walipaswa wakupe mkopo haraka kwa sababu ulionesha wewe ni muhitaji hadi ukakopa SONGESHA.Wewe ni mlengwa wa TASAF II Phase 3 unaevaa suti.Haujahitimu.
 
Tatizo riba zao sio rafiki, mfano mzuri ni SONGESHA. Hawa ni sawa sawa na kausha damu tuu. Mkopo mzuri niliouona kwasasa ni "saraly advance" only 5% na ndani ya mwezi lazima urudishe deni la watu utake usitake. Sasa hawa kina Songesha kila unavyochelewesha deni lao rate inapanda, hizi mamlaka zinazo blacklist hawalioni hili?

Sent from my SM-E045F using JamiiForums mobile app
 
Umasikini kmnioko.Mtu unakopa hadi buku/1000/one tau?Duh!Tufumbe macho tuombe ufukara utokomee mbali.
 
Hawana leseni ya kutoa mikopo hili hata waziri wa fedha aliwahi kulitolea fufafanuzi bungeni. Kinachofanyika ni uholela tu kama nchi yetu ilivyo holela

Sent from my SM-E045F using JamiiForums mobile app
 
Wasiwasi wangu hii mada imeanzishwa na mmoja wa wafanyakazi wa hizi kampuni za simu na amewaalika wenzake waje wachangie kwa nguvu zote ili wanaodaiwa walipe madeni. Hii nguvu inayotumika hapa sio kawaida. Nina deni Songesha zaidi ya laki moja na nusu kwa mwaka sasa, na wiki iliyopita nimepata mkopo wangu saaafi kabisa kutoka benki

Sent from my SM-E045F using JamiiForums mobile app
 
Unataka kusema Mteja wa Vodacom Songesha anaweza kuwa na Deni linaloweza kuathiri kukopeshwa na Benki?

Kivipi jambo hilo likahusiana?
Inawezekana kabisa, in digital world namba yako ya nida inafanya mambo mengi siku hizi ikiwemo hilo la kutunza rekodi mbaya za madeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…