Ukiwa nje usiwaamini ndugu Bongo, ndoto ya kurudi nyumbani mazima imefifia kutokana na ujenzi hafifu

Principal za ujenzi ukiwa mbali ni kama ifuatavyo: 1.Fika mwenyewe utafute fundi wa uhakika na mpatane kazi kwa awamu (kuanza msingi mpaka kumwaga jamvi, kuinua tofali mpaka kufunga lenta, kupaua, kupiga plasta, kupiga gypsum, kupiga rangi etc) 2.Tafuta hardware ya uhakika ambapo vifaa vyako vyote utanunua hapo. 3.Msimamizi wa kuona kazi inaendaje. 4.Vifaa vyote vya ujenzi lipa straight kwa mwenye hardware, hata ukitaka mchanga na kokoto mtumie yeye (kumbuka asiwe na hawa wenye njaa njaa) 5.Fundi mlipe kwa awamu mlivyokubaliana kwa makubaliano ya kutuma video clips zikionyesha work progress.. 6.Walau after every 3 months wewe au mkeo lazima mfike kuona hali halisi.
 
Yaani wewe, unawaamini ndugu zako ambao hata JF hawaijui? Maana wangekuwa wanaijua usingeweka picha ya hiyo nyumba yako na kuwasema namna hii
 
Basi nikajua kwa malalamiko haya utakuwa mjengo wa kisasa hadi nitamani kuzamia Ughaibuni.
Sio mbaya, hiyo nyumba haina uzio yaani ukuta na naona finishing bado sidhani kama kwa muda huo unatosha.
Watu mnaopata bahati kwenda nje na mkaamua kufanya uenzi wa makazi bora muwa mnajenga kwa kutumia makampuni badala ya ndugu zenu, mnakwepa makampuni ya ujenzi ila ndugu mnaowaamini wanawapiga pesa nyingi kuliko mngezolipa ktk kampuni.
Sinza hapa nilikuwa nafanya nami vimichakato vyangu, kuna jirani yangu alinunua nyumba mbli kupata moja, bei alioambiwa na ndugu zake alipigwa zaidi ya mil 28, kwenye ujenzi ni balaa tupu hadi roho inaniuma. Kuna kibustani mbele ya nyumba kidogo ndugu yake kwamwambia kinahitaji mil 3 ili kikae mkao duuu.
 
Unavyoona watu wengi wa hapa duniani wanapata majuto makubwa na kuanguka ni kutokana na watu wa karibu especially ndugu hawana uaminifu sometime mtu baki kama rafiki anaweza kuplay fair kuliko ndugu...better kumuamini mke kama mshazaa na mna familia kuliko kwa sasa Tamaa ni nyingi mno mbele ya pesa
 
Nimetoka kuwatumia tena ndugu pesa wafanye fasta fasta, lkn kama vile na wao wanajaribu kuchuja chuja ili wapate za kula na wakati nawatumiaga za kufanyia mambo yao, kupigia misele nk.
Ishu kama hizi unatenga tu muda kama ni mwezi mmoja unakuja unasimamia mafundi mpaka sehemu fulani unasimama ukipata tena nafasi unarudi
 
Mkuu niuzie huo mjengo kwa million 25 TZS
 
Usije tuma tena pesa kwa ndugu zako,Ni heri uje mwenyewe ukiwa na hela zako usimamie ujenzi mwenyewe.wabongo kwenye uaminifu wa hela ni 0%

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Kampuni za ujenzi mbona zipo una sainiana mikataba tu unawapa chao.

Wanakukabidhi funguo nyumba kukamilika ndani ya muda

Njia nyingine nunua nyumba zilizokwisha kamilika
 
Mkuu tupe connection huko kaburu, passport zipo tayari. Niandae kiasi gani ili niweze kufika nakusaka tonge huko?
Wenyewe hawataki wageni, mtaelewa lini hili somo?

Hata ufanye kazi miaka 20 South Africa kwa mshahara wa deiwaka hutoki, wanaofanikiwa na kufanya mambo Bongo hawatokaa wakwambie siri ya mafanikio yao.
 
Mkuu kama hutojali, badala ya kuwalaumu ndugu humu ambao hawawezi kujitetea, hebu fanya quick estimation utuambue mbaka hapo ilipofika umetumia sh ngapi ilitujue kama kweli umepigwa ama ni wasiwasitu.

Pia tuambie ndani umeshapiga Dari? je chini kuna rough floor?.
Madirisha mangapi, vyumba vingapi,eneo zima lenye nyumba ni square mita ngapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…