Ukiwa umeenda kuosha gari zingatia haya

Ukiwa umeenda kuosha gari zingatia haya

Fanya Practical ewe mwenye gari:

Nunua Chocolate ama biscuits kidogo zipake pilipili kichaa za kutosha nenda nazo car wash, ziache kwenye gari halafu uone hao TUMBILI wadokozi watakavyolia na kusaga meno..

Hutaua ila utawakomesha!

Baadae waambie zilikua za kutegemea panya nyumbani
Nimecheka sanaa aisee hii kitu ya kujaribu kabisa
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta ila siyo car wash zote ni wahuni, binafsi nimefunga camera natizama muda wowote hata nikiwa safarini na niliwaambia nikisikia malalamiko yoyote kutoka kwa mteja kwanza natizama tukio lilivyo kwa camera angle zote na kijana aliyeshughulikia hilo gari kisha polisi na kazi ndio mwisho
 
Namshukuru sana Mungu kwa kunipa upekee!Mimi gari nalioshea nyumbani na fundi wa kutengeneza ni nyumbani,nikisafiri linabaki na tope hadi nirudi nyumbani.
Huoni kama unaharibu gari..? Matope si mazuri kwa afya ya gari hasa huko uvunguni..
 
Gari oshea nyumbani.
Ukiwa Safarini unafanyaje? Au utakuw unarud nyumbani kuosha then unaendelea na Safari ikichafuka unarudi tena.

Mfano: Nyumbani Dar, safari DODOMA.

Gari imechafuka ukiwa Morogoro unageuza kuosha Dar alaf unaanza safar upya?

Nazungumzia ktk muktadha tofauti kdg mfn wakati wa Masika etc.. ni muhimu gari kuwa safi muda wote.
 
Gari langu naosheaga sehemu moja tu; Hata ikitokea nimemuazimisha mtu gari; namuelekeza sehemu ya kuoshea...., nimeenda mbali zaidi, mafuta pia nawekea only one place. Nabadiri tu maeneo kama nimesafiri, huko nakua sina choice
 
Back
Top Bottom