Ukíwa unajitafuta ndio wakati sahihi wa kutafuta mke. Namaanisha mke wa ujana wako (miaka 21 - 30)

Ninapingana na wewe, uyo baba uliyemtolea mfano ameishi katika kizazi tofauti na sisi. Kwa maisha ya sasa katika suala la kuyapa usiriaz mahusiano iyo range ya umri ni rafiki zaidi kwa mwanamke kuliko mwanaume.

Kwanza lazima ujue mwanaume unanunua upendo na hauependwi wewe kama binadamu isipokua unapendwa kutokana na status yako, mwanaume 20's sio umri sahihi wa kuyapa kipaumbele mahusiano.

Huo ni umri wa kutengeneza maisha yako, kuongeza thamani yako na kujitafuta.

Mapenzi ni matamu lakini kama ukiyazingatia muda ambao sio sahihi basi unajiandalia majanga maishani mwako.

Katika 20's usiwape kabisa kipaumbele wanawake, usijiangaishe kutengeneza mahusiano. Moja ya kitu cha kijinga mwanaume unatakiwa kujiepusha nacho ukiwa 20's ni kumpenda mwanamke, usifanye huo ujinga hata mara moja kwa maana itakugharimu sana utakapofika 30's
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…