Ukiwajua Polisi Tanzania, hutawashangaa kabisa na taarifa zao

Ukiwajua Polisi Tanzania, hutawashangaa kabisa na taarifa zao

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Nimeona watu wanashangaa polisi kuja na taarifa za mtu aliedhaniwa katekwa kuwa kafa kwenye ajali ....siko hapa kuwatetea polisi ..wala kushutumu lakini ningependa kuongea Kwa uzoefu wangu ...kuhusu polisi Tanzania...

Niliwahi kuwa na kesi ya mtu alienitapeli ...polisi Chango"mbe nikapewa Askari wa upepelezi tukawa tunamtafuta Kwa karibu miezi miwili...now wakati tunamtafuta huyo mtu tulishirikisha hadi kitengo cha cyber. Askari hao niliopewa kupitia"connection ya mtu powerful "kwahiyo sikuwa na wasiwasi na kuwa labda hawana nia au wamehongwa...walikuwa serious kazin....sasa cha kuchekesha ni kuwa Kwa kipindi ambacho "mtuhumiwa wetu" tunamtafuta...huyo mtuhumiwa akaenda Fanya matukio mengine ya kitapeli akakamatwa polisi Magomeni...akaachiwa...huku Sisi bado "tunamtafuta"..na mtuhumiwa baadae akaenda kumshitaki mtu mwingine polisi Kilwa road waliotapeliana...huku Sisi tunamtafuta...baadae kabisa akafanya tukio lingine akakamatwa polisi Oysterbay ndo tukaja kupata taarifa.

Kichekesho kingine ni jinsi polisi walivyokuwa wanachukulia hayo matukio kama tofauti na yanajitegemea na sio Ku combine matukio na kufungua kesi moja with strong evidence...na jinsi kila kituo kinamgombea mtuhumiwa....baadae nikaja gundua structure ya polisi ya ni ya kizamani Sana ...na Sheria zinaunda jeshi la polisi za kizamani sana....Kwa ufupi mahitaji ya kuwa na chombo cha Ku deal na organised crime ya mwaka 2024 yako tofauti kabisa na muundo wa jeshi la polisi....lilivyo sasa...

So sometimes tunawauliza polisi maswali na lawama nyingi wakati kiukweli hili jeshi la polisi Lina operate kama Tanzania bado uko miaka ya sabini tunawapa lawama nyingi sana bila kukaa chini na kuangalia namna ya kuwa na chombo vya mahitaji ya sasa na Sheria za sasa dunia inabadilika sana.

Leo ukiibiwa simu ndani ya mwendokasi..taratibu inasema uende polisi pale ulipopandia mwendokasi...yaani kama umepanda mwendokasi kimara ukaibiwa simu labda Magomeni itabidi urudi kimara kuandika jalada wakati pengine mwizi kateremkia posta...huu ni mfano Tu wa dunia inavyo kwenda na polisi walivyo baki kizamani.​

Jeshi la polisi linahitaji overhaul kabisa
 
Leo ukiibiwa simu ndani ya mwendokasi..taratibu inasema uende polisi pale ulipopandia mwendokasi...yaani kama umepanda mwendokasi kimara ukaibiwa simu labda Magomeni itabidi urudi kimara kuandika jalada wakati pengine mwizi kateremkia posta...huu ni mfano Tu wa dunia inavyo kwenda na polisi walivyo baki kizamani.
  1. Hatuwezi kuwa na jeshi bora kwasababu askari hao ni form 4 failures, na wengine ni std 7 wanaotumia vyeti vya watu wengine
  2. Hao askari na baadhi ya maboss wao wapo kwenye nafasi hizo ili kujinufaisha wao binafsi na waliowaweka kuliongoza jeshi
  3. Mtandao wa hilo jeshi ni wa kuendeleza rushwa zaidi kuliko kuihudumia jamii
 
Watu wanaofeli shule(4M4) na kukosa mwelekeo kimaisha unakuta ndo wanajiunga na mafunzo ya jeshi la polisi kwa connection za ndugu zao ambao ni polisi, hapo unategemea weledi upi? wachache hukumbuka kujiendeleza kielimu hadi wanapata masters hasa kwenye sheria ila wengi wao kuwauliza maswali magum ni kuzionea akili zao. PT wape kazi ya kupiga raia virungu, kuwarusha mabom na kudai hela za kubrashi viatu hapo watakufurahisha. Kinachotupoza waafrika ni kurithi muundo na mfumo wa jeshi la polisi toka kwa wakoloni ambalo malengo yake ni kulinda na kutetea maslahi ya watawala.
 
Solution ni ku-digitalise mfumo, kila data iingizwe kwenye mfumo isomeke nchi nzima. Kama details za huyo aliyekutapeli zingekuwa kwenye mfumo wa taarifa za jinai za kidigiti za polisi, data ikiingizwa kituo cha polisi kilwa, inatakiwa ipige alarm pale kituo cha polisi Magomeni kuonyesha kwamba the suspect amekuwa located kilwa. Pia isomane na vituo vya uhamiaji, akiwa anafanya michakato ya kuvuka boda, afisa uhamiaji akiwa ana-process, jina likiingia tu katika mfumo, alarm ilie ili afisa huyo afanyie clearance za alarm husika. Isomane na magereza, Mahakama....

Isomane na mochwari kwamba ukiingia mwili wa mtu aliyekufa pasipo kujulikana, cha kwanza police na Hospitali wachukue DNA ya mtu huyo, iingie kwenye mfumo, ili akija ndugu au mtu kumtafuta ndugu, mtu huyo aliyekuha kutafuta nduguye atoe DNA, ikifanana na ya marehemu, basi mfumo nchi nzima unaweza kusema labda yuko mochwari mbeya, Nkasi, au Buzebazeba kutokana na DNA data iliyojazwa.

Hii itapunguza kutafutana manually katika mochwari coz mwananchi hawezi kutembelea mochwari za nchi nzima. Hata akifanikiwa, atatoka na ugonjwa mwingine kutokana na kuangalia watu waliokufa nchi nzima

Once I heard kwamba kuna utaratibu wa kutengeneza Database ya taifa zima ya DNA unafanywa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali. Matukio kama ya ghorofa la kariakoo, DNA ingetosha kufanya utambuzi. Matukio ya watu kuungua na moto mpaka kufa, majivu au mabaki yakiingia katika DNA database, wanatambulika

There is a need to create a digital cobweb ya jinai, na taasisi zote zinazo process jinai.

Suala la kuibiwa simu liwe reported anywhere, tena online, kama mtu ana IMEI number, imsome mwizi alipo pa po hapo bila kusubiri issue za watu wa Cyber, na mfumo uwe unaampa taarifa aliyeibiwa timely, papo hapo.

Therefore, there us a need to establish a sophisticated department of IT at the Police Force
 
Jeshi la polisi linahitaji overhaul kabisa​
Naunga mkono hoja, Issue ya Mzee Kibao wa Chadema ni typical example。
  1. scene 1。Ijumaa September 6,saa 1 usiku Mzee Kibao apanda basi la Tashrifu la usiku kwenda Tanga。
  2. Scene 2。Kufika maeneo ya Regeta, basi lasimamishwa,na watu waliojitambukisha kama polisi wasio na sare, lakini na silaha za moto,wamtia pingu Mzee Kibao na kushuka nae toka kwenye basi,la Tashrifu baada ya kusimamishwa na landcruser mbili hard top, kisha wakamuingiza na kutokomea nae。
  3. Scene 3。September 6 Saa 4:10 usiku wa tarehe 6 JJ Mnyika atoa taarifa mtandaoni John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana
  4. Scene 4, September 7,saa 2:asubuhi polisi yaokota mwili wa mtu maeneo ya Kunduchi Ununio,na kuupeleka。Mwananyama hospital kimya kimya
  5. Scene 5:Jumakosi。Septemba 7 saa 5 Asubuhi JJ Mnyika afanya press conference kutangaza kutekwa kwa kada wao CHADEMA: Mzee Ali Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
  6. Scene 6, Jumamosi September 7 saa 10 jioni。PT yatoa taarifa kwa umma kuwa wameipokea taarifa ya JJ Mnyika wanaifanyia kazi Kuelekea 2025 - Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ali Kibao
  7. Scene 7:Jumamosi September 7 saa 1:usiku kada wa Chadema Boni Yai aandamana na ndugu kutambua ule mwili uliookotwa。asubuhi Ununio ndipo ukagundulika ni wa Mzee Kibao TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
  8. Scene 8:Jumapili September 8, Jeshi la polisi latoa taarifa ya tukio Polisi yasikitishwa na kifo cha kada wa CHADEMA, Ali Kibao. Latoa wito kwa mwenye taarifa za kweli na uhakika awasilishe kwa mujibu wa taratibu hapa naomba niwakumbushe polisi walioukota mwili Jumamosi asubuhi, wakati JJ Mnyika anaongea kwenye press conference yake,mwili tayari uko M/Nyamala,wakati PT wanatoa taarifa kupokea taarifa ya Chadema kuwa watafanya uchunguzi wa tukio hilo,mwili tayari walikuwa nao!
  9. Scene 9 Jumapili September 8, CinC ,Rais Samia aamuru uchunguzi wa kina na wa haraka Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao
  10. My Take,kitendo cha polisi kupokea mwili asubuhi na ku mute, hadi kesho yake, news ya kupokea a mutileted dead body of an unidentified man ni bigger news kuliko kupokea taarifa ya Chadema!。 Kauli ya CinC ni amri, uchunguzi wa haraka ulifanyika,ila hakuna mrejesho。 hili na mimi nimeliandikia
  11. Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!
  12. Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe
P
 
Kaazi kweli kweli

Ina maana nchi imepoteza billions of TZ shillings za walipa kodi kutengeneza data base ya kusaka wahalifu.

Halafu kazi bure, mtuhumiwa mradi ana connection zake ndani ya jeshi la polisi akamatiki.

Maswali ni mengi ni vipi Jerry Slaa alitolewa wizara ya ardhi.
 
Jerry ana kashfa ya rushwa, sehemu alizokuwa anaenda kupiga mikwara alikuwa anaacha chawa wake washawishi mipango, pale mikocheni kwa Tibaijuka kwenye Sheli ni mfano mzuri. Pia alikuwa bize kusaidia jamaa zake wa karibu, huwezi muona Sumbawanga au kigoma au ruvuma.

Yeye ni masaki, mikocheni, mbweni, kariakoo, mwanza, arusha. Vijijini ahhaaaa....! Haendi, huko hawana hela
 
Watu wanaofeli shule(4M4) na kukosa mwelekeo kimaisha unakuta ndo wanajiunga na mafunzo ya jeshi la polisi
Hoja dhaifu sana, kuna shahada plus G.P.A kali huko mitaani na zimekosa mwelekeo wa maisha (uelewa wako finyu kuhusu maisha) zimeamua kuendesha bodaboda na bajaji, wa kike wameamua yao!

Unahisi shahada,uzamili n.k ukiwa kwenye taasisi za kiusalama zina tija?? Hivi unapoambiwa tii amri ya mkubwa wako hapo shahada au div 1 inahusika vipi??

Unafahamu muundo wa mafunzo yao?? Pale div 1 au shahada inakusaidiaje?? Siku zote watawala (maboss)(vitengo) ni wachache na wanaofanyishwa kazi ni wengi.

Halafu nani aliyekudanganya ukipata div 1 au shahada kwa elimu yetu hii tunaoifahamu eti unajisifu una akili!

Nahisi hujatembea duniani na hujakutana na mikasa kuhusu elimu yetu! Unajua serikalini kuna first class ngapi?? Zimeleta tija??
 
Good point
 
Wewe kweli zero brain. Hili povu kafulie sidiria za mkeo maana ni chaf sana.
 
Jerry ana kashfa ya rushwa, sehemu alizokuwa anaenda kupiga mikwara alikuwa anaacha chawa wake washawishi mipango, pale mikocheni kwa Tibaijuka kwenye Sheli ni mfano mzuri. Pia alikuwa bize kusaidia jamaa zake wa karibu, huwezi muona Sumbawanga au kigoma au ruvuma.

Yeye ni masaki, mikocheni, mbweni, kariakoo, mwanza, arusha. Vijijini ahhaaaa....! Haendi, huko hawana hela
Nakubaliana na wewe nusu.

Ukweli lile sakata la Mikocheni kulikuwa msukumo wa rafiki yake fisadi; inawezekana pia zipo isolated kesi nyingine ya prime areas alitumika.

Lakini overall Jerry alikuwa waziri mzuri ardhi alifanya mabadiliko makubwa.

Kuna mwana JF sijui anatumia jina gani nilimuuzia kiwanja changu Tegeta huo mziki wa kumbadilishia hati salaleh.

Halafu jamaa anaonekana ni afisa usalama kwa msimamizi wangu wa mjini alivyokuwa anamuona. Trip za Dar-Dodoma na ziara za viongozi haziishi.

Shida zaidi mwanasheria wake alikuwa na mambo mengi balaa mpaka karibu nisuse.

Jerry alifanya shughuli ya kununua kiwanja kitapeli ngumu, mambo mengi kama muuzaji unatumia third party kukuuzia.

Watu kama Jerry uwa hawadumu ardhi.
 
Nimeona watu wanashangaa polisi kuja na taarifa za mtu aliedhaniwa katekwa kuwa kafa kwenye ajali ....siko hapa kuwatetea polisi ..wala kushutumu lakini ningependa kuongea Kwa uzoefu wangu ...kuhusu polisi Tanzania...

Niliwahi kuwa na kesi ya mtu alienitapeli ...polisi Chango"mbe nikapewa Askari wa upepelezi tukawa tunamtafuta Kwa karibu miezi miwili...now wakati tunamtafuta huyo mtu tulishirikisha hadi kitengo cha cyber. Askari hao niliopewa kupitia"connection ya mtu powerful "kwahiyo sikuwa na wasiwasi na kuwa labda hawana nia au wamehongwa...walikuwa serious kazin....sasa cha kuchekesha ni kuwa Kwa kipindi ambacho "mtuhumiwa wetu" tunamtafuta...huyo mtuhumiwa akaenda Fanya matukio mengine ya kitapeli akakamatwa polisi Magomeni...akaachiwa...huku Sisi bado "tunamtafuta"..na mtuhumiwa baadae akaenda kumshitaki mtu mwingine polisi Kilwa road waliotapeliana...huku Sisi tunamtafuta...baadae kabisa akafanya tukio lingine akakamatwa polisi Oysterbay ndo tukaja kupata taarifa.

Kichekesho kingine ni jinsi polisi walivyokuwa wanachukulia hayo matukio kama tofauti na yanajitegemea na sio Ku combine matukio na kufungua kesi moja with strong evidence...na jinsi kila kituo kinamgombea mtuhumiwa....baadae nikaja gundua structure ya polisi ya ni ya kizamani Sana ...na Sheria zinaunda jeshi la polisi za kizamani sana....Kwa ufupi mahitaji ya kuwa na chombo cha Ku deal na organised crime ya mwaka 2024 yako tofauti kabisa na muundo wa jeshi la polisi....lilivyo sasa...

So sometimes tunawauliza polisi maswali na lawama nyingi wakati kiukweli hili jeshi la polisi Lina operate kama Tanzania bado uko miaka ya sabini tunawapa lawama nyingi sana bila kukaa chini na kuangalia namna ya kuwa na chombo vya mahitaji ya sasa na Sheria za sasa dunia inabadilika sana.

Leo ukiibiwa simu ndani ya mwendokasi..taratibu inasema uende polisi pale ulipopandia mwendokasi...yaani kama umepanda mwendokasi kimara ukaibiwa simu labda Magomeni itabidi urudi kimara kuandika jalada wakati pengine mwizi kateremkia posta...huu ni mfano Tu wa dunia inavyo kwenda na polisi walivyo baki kizamani.​

Jeshi la polisi linahitaji overhaul kabisa
Na kinatakiwa chombo cha ku oversee utendaji wa polisi ambacho si polisi
Polisi wengi ni wezi wenye uniform!. Imagine mtu wa level ya RPC anaposhiriki kwenye dhulma dhidi ya watuhumiwa.
 
Wala sina ninachokijua zaidi ya kushangazwa tu. I can assure you.
Sina inside info lakini the moment Jerry alipoanza kusema anasimamisha vibali vya petrol station mpya sijui hadi nini nini nikajua Tu ataondolewa haraka sana...hii kauli ya kusimamisha vibali vya petrol station aliwahi kuitoa Mabula pia hapo Ardhi na haku last miezi mitatu....kwenye vita za siasa lazima uchague maadui zako na lazima upigane na adui mmoja Kwa wakati... angebaki na walanguzi WA viwanja na rushwa za ardhi...huko kwenye petrol station aligusa nyaya ambazo hazijui vizuri mizizi yake
 
Back
Top Bottom