Ukiwajua Polisi Tanzania, hutawashangaa kabisa na taarifa zao

Ukiwajua Polisi Tanzania, hutawashangaa kabisa na taarifa zao

Nimeona watu wanashangaa polisi kuja na taarifa za mtu aliedhaniwa katekwa kuwa kafa kwenye ajali ....siko hapa kuwatetea polisi ..wala kushutumu lakini ningependa kuongea Kwa uzoefu wangu ...kuhusu polisi Tanzania...

Niliwahi kuwa na kesi ya mtu alienitapeli ...polisi Chango"mbe nikapewa Askari wa upepelezi tukawa tunamtafuta Kwa karibu miezi miwili...now wakati tunamtafuta huyo mtu tulishirikisha hadi kitengo cha cyber. Askari hao niliopewa kupitia"connection ya mtu powerful "kwahiyo sikuwa na wasiwasi na kuwa labda hawana nia au wamehongwa...walikuwa serious kazin....sasa cha kuchekesha ni kuwa Kwa kipindi ambacho "mtuhumiwa wetu" tunamtafuta...huyo mtuhumiwa akaenda Fanya matukio mengine ya kitapeli akakamatwa polisi Magomeni...akaachiwa...huku Sisi bado "tunamtafuta"..na mtuhumiwa baadae akaenda kumshitaki mtu mwingine polisi Kilwa road waliotapeliana...huku Sisi tunamtafuta...baadae kabisa akafanya tukio lingine akakamatwa polisi Oysterbay ndo tukaja kupata taarifa.

Kichekesho kingine ni jinsi polisi walivyokuwa wanachukulia hayo matukio kama tofauti na yanajitegemea na sio Ku combine matukio na kufungua kesi moja with strong evidence...na jinsi kila kituo kinamgombea mtuhumiwa....baadae nikaja gundua structure ya polisi ya ni ya kizamani Sana ...na Sheria zinaunda jeshi la polisi za kizamani sana....Kwa ufupi mahitaji ya kuwa na chombo cha Ku deal na organised crime ya mwaka 2024 yako tofauti kabisa na muundo wa jeshi la polisi....lilivyo sasa...

So sometimes tunawauliza polisi maswali na lawama nyingi wakati kiukweli hili jeshi la polisi Lina operate kama Tanzania bado uko miaka ya sabini tunawapa lawama nyingi sana bila kukaa chini na kuangalia namna ya kuwa na chombo vya mahitaji ya sasa na Sheria za sasa dunia inabadilika sana.

Leo ukiibiwa simu ndani ya mwendokasi..taratibu inasema uende polisi pale ulipopandia mwendokasi...yaani kama umepanda mwendokasi kimara ukaibiwa simu labda Magomeni itabidi urudi kimara kuandika jalada wakati pengine mwizi kateremkia posta...huu ni mfano Tu wa dunia inavyo kwenda na polisi walivyo baki kizamani.​

Jeshi la polisi linahitaji overhaul kabisa
Ndio maana kwa miaka 20+ tumekuwa tukipigia kelele muundo mpya wa TanPol.
Tumelipigia kelele hili swala mpaka basi, hivyo ndugu ujue tuu hili ukiloandika linajulikana na ndio maana wenye utimamu wa akili wote wanataka Tanpol iundwe upya.

Kongole kwa kuliona hilo leo na kulianzishia uzi hapa JamiiForums.
 
Solution ni ku-digitalise mfumo, kila data iingizwe kwenye mfumo isomeke nchi nzima. Kama details za huyo aliyekutapeli zingekuwa kwenye mfumo wa taarifa za jinai za kidigiti za polisi, data ikiingizwa kituo cha polisi kilwa, inatakiwa ipige alarm pale kituo cha polisi Magomeni kuonyesha kwamba the suspect amekuwa located kilwa. Pia isomane na vituo vya uhamiaji, akiwa anafanya michakato ya kuvuka boda, afisa uhamiaji akiwa ana-process, jina likiingia tu katika mfumo, alarm ilie ili afisa huyo afanyie clearance za alarm husika. Isomane na magereza, Mahakama....

Isomane na mochwari kwamba ukiingia mwili wa mtu aliyekufa pasipo kujulikana, cha kwanza police na Hospitali wachukue DNA ya mtu huyo, iingie kwenye mfumo, ili akija ndugu au mtu kumtafuta ndugu, mtu huyo aliyekuha kutafuta nduguye atoe DNA, ikifanana na ya marehemu, basi mfumo nchi nzima unaweza kusema labda yuko mochwari mbeya, Nkasi, au Buzebazeba kutokana na DNA data iliyojazwa.

Hii itapunguza kutafutana manually katika mochwari coz mwananchi hawezi kutembelea mochwari za nchi nzima. Hata akifanikiwa, atatoka na ugonjwa mwingine kutokana na kuangalia watu waliokufa nchi nzima

Once I heard kwamba kuna utaratibu wa kutengeneza Database ya taifa zima ya DNA unafanywa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali. Matukio kama ya ghorofa la kariakoo, DNA ingetosha kufanya utambuzi. Matukio ya watu kuungua na moto mpaka kufa, majivu au mabaki yakiingia katika DNA database, wanatambulika

There is a need to create a digital cobweb ya jinai, na taasisi zote zinazo process jinai.

Suala la kuibiwa simu liwe reported anywhere, tena online, kama mtu ana IMEI number, imsome mwizi alipo pa po hapo bila kusubiri issue za watu wa Cyber, na mfumo uwe unaampa taarifa aliyeibiwa timely, papo hapo.

Therefore, there us a need to establish a sophisticated department of IT at the Police Force
Huko Buzebazeba ndiyo home mkuu?

Jokes aside....umeongea vitu vya msingi sana nami nakubaliana nawe kwa 100%

Swali....kwa nini hawafanyi hiyo digitization na synchronizations ya mifumo?

Sababu ni nyingi lakini mbili naona zina uzito zaidi:

1. Sehemu kubwa ya askari ni watu wasio na uwerevu wala weledi kwenye utendaji. Kutambua kuwa technology inaweza kusaidia kuboresha utendaji na kuongeza ufanisi inahitaji weledi na werevu....watu waliofeli shule kama ambavyo polisi wengi walivyo hawawezi kupenda sana mifumo iliyokaa kisomisomi...

2. Ufisadi.....mifumo mibovu inafanya kukosekane ufanisi. Kukosekana kwa ufanisi ni kichocheo cha wao kufanya ufisadi.....mtu kaiba kigamboni, ukimuona morogoro huwezi kutoa report morogoro na ikafanyiwa kazi. sana watakachofanya wale polisi wa morogoro ni kumtisha na kudai rushwa. Huu uholela wa kufanya mambo wanautumia kujinuifaisha.
 
Hoja dhaifu sana, kuna shahada plus G.P.A kali huko mitaani na zimekosa mwelekeo wa maisha (uelewa wako finyu kuhusu maisha) zimeamua kuendesha bodaboda na bajaji, wa kike wameamua yao!

Unahisi shahada,uzamili n.k ukiwa kwenye taasisi za kiusalama zina tija?? Hivi unapoambiwa tii amri ya mkubwa wako hapo shahada au div 1 inahusika vipi??

Unafahamu muundo wa mafunzo yao?? Pale div 1 au shahada inakusaidiaje?? Siku zote watawala (maboss)(vitengo) ni wachache na wanaofanyishwa kazi ni wengi.

Halafu nani aliyekudanganya ukipata div 1 au shahada kwa elimu yetu hii tunaoifahamu eti unajisifu una akili!

Nahisi hujatembea duniani na hujakutana na mikasa kuhusu elimu yetu! Unajua serikalini kuna first class ngapi?? Zimeleta tija??
Daaah...jamaa amekuwa mkali huyo, ila nadhani hatuwezi beza kabisa umuhimu wa vyeti
 
Angalia maisha Yao baada ya Kustaafu! Fanya utafiti kidogo tu utajua karma is real! Mwingine anajitengenezea kaburi huko,huku akiwa hama maelewano na familia yake kabisa anaitwa 7sita
Naunga mkono hoja
 
Even when they tell you, they can’t justify their position without evidence, but can only agree by implying based on general accusations of the police force.
But you" agreed", don't you remember?

Here is the exact quote, just to remind you if you have such a short memory"
Why do you want to run away from your own "perspective" as you state?
 
Nimeona watu wanashangaa polisi kuja na taarifa za mtu aliedhaniwa katekwa kuwa kafa kwenye ajali ....siko hapa kuwatetea polisi ..wala kushutumu lakini ningependa kuongea Kwa uzoefu wangu ...kuhusu polisi Tanzania...

Niliwahi kuwa na kesi ya mtu alienitapeli ...polisi Chango"mbe nikapewa Askari wa upepelezi tukawa tunamtafuta Kwa karibu miezi miwili...now wakati tunamtafuta huyo mtu tulishirikisha hadi kitengo cha cyber. Askari hao niliopewa kupitia"connection ya mtu powerful "kwahiyo sikuwa na wasiwasi na kuwa labda hawana nia au wamehongwa...walikuwa serious kazin....sasa cha kuchekesha ni kuwa Kwa kipindi ambacho "mtuhumiwa wetu" tunamtafuta...huyo mtuhumiwa akaenda Fanya matukio mengine ya kitapeli akakamatwa polisi Magomeni...akaachiwa...huku Sisi bado "tunamtafuta"..na mtuhumiwa baadae akaenda kumshitaki mtu mwingine polisi Kilwa road waliotapeliana...huku Sisi tunamtafuta...baadae kabisa akafanya tukio lingine akakamatwa polisi Oysterbay ndo tukaja kupata taarifa.

Kichekesho kingine ni jinsi polisi walivyokuwa wanachukulia hayo matukio kama tofauti na yanajitegemea na sio Ku combine matukio na kufungua kesi moja with strong evidence...na jinsi kila kituo kinamgombea mtuhumiwa....baadae nikaja gundua structure ya polisi ya ni ya kizamani Sana ...na Sheria zinaunda jeshi la polisi za kizamani sana....Kwa ufupi mahitaji ya kuwa na chombo cha Ku deal na organised crime ya mwaka 2024 yako tofauti kabisa na muundo wa jeshi la polisi....lilivyo sasa...

So sometimes tunawauliza polisi maswali na lawama nyingi wakati kiukweli hili jeshi la polisi Lina operate kama Tanzania bado uko miaka ya sabini tunawapa lawama nyingi sana bila kukaa chini na kuangalia namna ya kuwa na chombo vya mahitaji ya sasa na Sheria za sasa dunia inabadilika sana.

Leo ukiibiwa simu ndani ya mwendokasi..taratibu inasema uende polisi pale ulipopandia mwendokasi...yaani kama umepanda mwendokasi kimara ukaibiwa simu labda Magomeni itabidi urudi kimara kuandika jalada wakati pengine mwizi kateremkia posta...huu ni mfano Tu wa dunia inavyo kwenda na polisi walivyo baki kizamani.​

Jeshi la polisi linahitaji overhaul kabisa
Mkuu uliyoandika ni kweli ila ni kama unaji-contradict mwenyewe baadhi ya maeneo. Umeandika ''So sometimes tunawauliza polisi maswali na lawama nyingi wakati kiukweli hili jeshi la polisi Lina operate kama Tanzania bado uko miaka ya sabini tunawapa lawama nyingi sana bila kukaa chini na kuangalia namna ya kuwa na chombo vya mahitaji ya sasa na Sheria za sasa dunia inabadilika sana''. Haya maneno yanaonyesha polisi ndiyo wa kulaumiwa. Kwa nini wanaiweka serikali madarakani kwa kutumia mitutu wakati wanajua haiwajali?
 
Back
Top Bottom