Solution ni ku-digitalise mfumo, kila data iingizwe kwenye mfumo isomeke nchi nzima. Kama details za huyo aliyekutapeli zingekuwa kwenye mfumo wa taarifa za jinai za kidigiti za polisi, data ikiingizwa kituo cha polisi kilwa, inatakiwa ipige alarm pale kituo cha polisi Magomeni kuonyesha kwamba the suspect amekuwa located kilwa. Pia isomane na vituo vya uhamiaji, akiwa anafanya michakato ya kuvuka boda, afisa uhamiaji akiwa ana-process, jina likiingia tu katika mfumo, alarm ilie ili afisa huyo afanyie clearance za alarm husika. Isomane na magereza, Mahakama....
Isomane na mochwari kwamba ukiingia mwili wa mtu aliyekufa pasipo kujulikana, cha kwanza police na Hospitali wachukue DNA ya mtu huyo, iingie kwenye mfumo, ili akija ndugu au mtu kumtafuta ndugu, mtu huyo aliyekuha kutafuta nduguye atoe DNA, ikifanana na ya marehemu, basi mfumo nchi nzima unaweza kusema labda yuko mochwari mbeya, Nkasi, au Buzebazeba kutokana na DNA data iliyojazwa.
Hii itapunguza kutafutana manually katika mochwari coz mwananchi hawezi kutembelea mochwari za nchi nzima. Hata akifanikiwa, atatoka na ugonjwa mwingine kutokana na kuangalia watu waliokufa nchi nzima
Once I heard kwamba kuna utaratibu wa kutengeneza Database ya taifa zima ya DNA unafanywa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali. Matukio kama ya ghorofa la kariakoo, DNA ingetosha kufanya utambuzi. Matukio ya watu kuungua na moto mpaka kufa, majivu au mabaki yakiingia katika DNA database, wanatambulika
There is a need to create a digital cobweb ya jinai, na taasisi zote zinazo process jinai.
Suala la kuibiwa simu liwe reported anywhere, tena online, kama mtu ana IMEI number, imsome mwizi alipo pa po hapo bila kusubiri issue za watu wa Cyber, na mfumo uwe unaampa taarifa aliyeibiwa timely, papo hapo.
Therefore, there us a need to establish a sophisticated department of IT at the Police Force