Hahahah jamaa ana vimba bana! Huko kuishi standard life zipo familia zinaishi hivyo kiukweli ila rate ni kama 1% ya watu wote nchini! Naijua familia moja ya jamaa na mkewe mchizi ni senior MDH na mkewe yuko PEPFAR ni senior!
Budget zao ni kama ifuatavyo:
-Watoto wawili ada ni 18M kwa mwaka!
-Utilities pamoja na chakula ni 4M kwa mwezi mafuta yakula yanaagizwa USA, viungo Zanzibar, Samaki Mwanza, Kuku na matunda Tanga! Vyote ni fresh yani.
-Dereva wakupeleka watoto shule na kuwarudisha home na ractis ya watoto.
-Mama Prado baba Harrier tako la Nyani full tank mda wote!
-Mapumziko ya mwisho wa mwaka watoto hupelekwa Disney land!
-Mshahara mama anakunja 7M ila michezo anayocheza kwa mwezi anaingiza kati ya 9-12M nje ya salary!
-Jamaa nae 10M na michezo mibaya inahusika.
Sasa je ni wangapi wenye hii bahati hapa nchini nje ya wafanya biashara wakubwa? Ajira za BOT zimetoka ila watu watavunja hata nazi waingiemo mle! Nina hakika mshahara kwa wengi hautafika 3M ila its alot kwa level zetu za kimaskini mkuu! Kumbuka unapata na benefits nyingine nje ya mshahara huo maybe house allowance,transport, bima nakadhalika.
Kwa 2.8M take home gari unaendesha+Maintance na nyumbani watoto wanaenda msalani bila tatizo ukiwa na mke mwenye akili na savings unafanya kabisa au unachukua loan unajenga kabisa!