Ukiweka milioni 200 kwenye fixed deposit unapata mrejesho wa 1.5m kwa mwezi

Ukiweka milioni 200 kwenye fixed deposit unapata mrejesho wa 1.5m kwa mwezi

Kwa knowledge ndogo ya bankruptcy accounts, savers wa kawaida na Fixed Deposits wote wanaangukia pamoja wanakuwa kwenye kundi la umewakopesha benki bila dhamana.

Kwa hiyo statutory deductions, workman compensations, mortgaged loans, nk zinatangulia kwanza.
Government bonds nazo vepee mkuu zinaangukiaga pua???
 
200M kama unajua Biashara utatengeneza faida kubwa sana kuliko kuweka huko kwenye upuuzi
Wale waliokuwa wanauliza interest inayolipwa na benki kwa fixed deposit account. Niliongea na mmoja aliniambia wastani wa malipo ni kama hivyo ilivyo.

Hii inawafaa wasioweza kuzungusha pesa kwa njia ya biashara. Una uhakika wa kula kila mwezi na pesa yako
 
Hii inalipa sijui nchi yetu lakini kwingine inawezekana ukatumia hizo Bond kukopa mpaka 80% kwa benki nyingine kwa miaka mitano ambayo sawa na 160,000,000/- sawa na marejesho ya 2.6 kwa mwezi ukajenga nyumba mbili zenye uwezo wa kukulipa 1,200,000/- zikaweza kulipa riba na kubaki na kiasi kidogo huku ukiwa umeongeza thamani ya fedha yako.

hili ni kama benki zinaweza kukubali kuchukua bond kama security ya mkopo. Ukimaliza nyumba chukua nyumba moja iwe dhamana ya mkopo mwingine wa kutafuta mradi mwingine hata kama ni duka la jumla na maisha yanaenda.
nimerudi sasa!
ngoja tusumbue akili ili jioni ya leo angalau tuwe na mawazo zaidi ya mafanikio huku tukiondoa woga
  1. tukiwa na mradi wa milioni 200/- na tukianzia na Bond za Benk kuu za kila mwezi shillingi 2,700,000/- kama mchangiaji mwingine alivyotushirikisha.
  2. base kwenye assumption kwamba mwenye hela hizi anategemea kupata pension yake kwa mkupuo isiyopungua fedha tajwa hapo juu.
  3. ameshasomesha watoto
  4. ana pato kwa mwezi lisilopungua 900,000/- kama sehemu ya pension yake
  5. ana vimiradi nyumba mbili zinazomlipa 500,000/- kila moja kwa mwezi sawa na 1000,000/-
  6. amejenga frame 5 kila moja anapata 100,000 kodi sawa na 500,000/- kwa mwezi
  7. anavimifugo na bustani ndogo ya kumpiga company ili apunguze sukari na pressure na pia kuendelea na wigo wa kufoka na kutawala wafanyakazi wake wa hizo IGA zake.
  8. kwa kifupi huyu hoja ya basic need hana kabisa
sasa turudi kwa mkopo wetu tukilinganisha na uwekezaji wetu. tuchukue tumenunua security Bond Bank Kuu ya Tanzania kwa kuwekeza milion 200 kwa miaka 5 huku iklipa 2,700,000/- kwa mwezi.
  1. NMB wanawezakutoa mkopo kwa asilimia 17 kwa mwaka na kufanya marejesho kwa mwezi kuwa
    3,818,916.19
  2. kwa muda miezi 60 hivyo ni vizuri ukawa na marejesho japo mawili kabla ya mradi kuanza kwa kuwa fedha utakayolipwa kama faida haitatosha bali itabidi iongezeke kwa shillingi 1,118,916.19 japo kwa mtazamo wa hapo juu mtu huyu anaweza kumudu tu bila shaka.
  3. ukijenga apartment utachelewa jenga nyumba mbili ikiwezekana ghorofa moja yenye bachelor rooms mbilimbili kwa wateja 16 ambacho kila kimoja utalipwa 200,000/- sawa na 3,200,000/- kwa mwezi.
  4. ukitoa gharama za kuhudumia nyumba kama 30% na ukiongeza na deni la benki si haba anabaki 1,121,084.81
kwanini mtu huyu asiimbe wimbo wa taifa vijana mjiajiri!
 
Pesa ya kula kwa familia:-

1. Unga 1000 kilo moja
2.Mchele kilo moja 2500
3.Nazi moja 1500
4.Maji ya kunywa elfu 2000
5.Maji ya kutumia kwa siku dumu 10 = 2000
6.Mkaa vikopo viwili = 2000
7.Nyama kilo elfu 7
8.Sato/sangara kilo 11,000/8,000/=
9.Mafuta ya kupikia buku vibaba viwili......1000/=
10.mafuta ya taa nusu lita 1400/=
11.Sabuni ya kuogea Rungu 500/=
12.Sabuni ya kufulia Toffy 1000/=
13.Umeme kwa siku 2000/=
14.Nyanya 1000/=
15. Vitunguu 500/=
16.Karoti 2 @ 500/=
17.Hoho2 @ 500/=
18.Fungu la mboga 500/=
19.Maharage nusu 1500/=
20.Vocha ya bandle....... 2000
Hapo ongezea Kama una gari tenga laki 2 kila mwezi,bado mavazi haujaenda kuzungusha round baa .
Kwa maisha moderate 1.5m haitoshi ila kwa maisha ya chai na andazi moja hata laki 3 ni nyingi sana
 
Option nyingine ni kuwekeza kwenye real estate. Ukipata kiwanja location inayoeleweka unaweka. Kwa milioni 200 unasimamisha apartments za kueleweka. Hata kwa US$500 kwa mwezi kama ziko 5 utaiona faida.

Apartment 5 kwa milioni 200?! Apartment hizo za udogo au?!
 
Sehem inayoeleweka yenye kupangishika ya kuweka hzo apartments kadhaa huwez pata kwa mtaj huo wa 200m.....sehem inayoeleweka square metres price znaanzia Tsh 30,000...kwa maana kiwanja cha sqm 1000 ni 30m...sasa kwa apartments utaweka ngap?...kiwanja tu hyo hela unaikata nusu nzima..kama unataka kiwanja kikubwa.

Kiwanja cha 30M upate apartment za kupangisha usd 500!? Unaota ndoto ya mchana[emoji23][emoji23][emoji23] maana hizo bei ni mikocheni mbezi msasani huko utapata kiwanja cha 30M?!
 
Option nyingine ni kuwekeza kwenye real estate. Ukipata kiwanja location inayoeleweka unaweka. Kwa milioni 200 unasimamisha apartments za kueleweka. Hata kwa US$500 kwa mwezi kama ziko 5 utaiona faida.
Sky 200M inaweza kujenga apartment 5? sehemu zinazoeleweka?
 
Kiwanja cha 30M upate apartment za kupangisha usd 500!? Unaota ndoto ya mchana[emoji23][emoji23][emoji23] maana hizo bei ni mikocheni mbezi msasani huko utapata kiwanja cha 30M?!
Hata mimi nimeshangaa Kumbe Sky anatulisha kamba
 
1.5m kwa matumizi ya mwezi mzima labda uwe unaishi kisela bila familia na usiwe mtu wa bata sana.
Hapo assumption yake ni kwamba ulishakuwa na nyumba yako watoto walishasoma wanajitegemea umebakia wewe na wife . Ukiamka unasoma magazeti tuu.
 
Back
Top Bottom