Ukiweka milioni 200 kwenye fixed deposit unapata mrejesho wa 1.5m kwa mwezi

Government bonds nazo vepee mkuu zinaangukiaga pua???
 
200M kama unajua Biashara utatengeneza faida kubwa sana kuliko kuweka huko kwenye upuuzi
 
nimerudi sasa!
ngoja tusumbue akili ili jioni ya leo angalau tuwe na mawazo zaidi ya mafanikio huku tukiondoa woga
  1. tukiwa na mradi wa milioni 200/- na tukianzia na Bond za Benk kuu za kila mwezi shillingi 2,700,000/- kama mchangiaji mwingine alivyotushirikisha.
  2. base kwenye assumption kwamba mwenye hela hizi anategemea kupata pension yake kwa mkupuo isiyopungua fedha tajwa hapo juu.
  3. ameshasomesha watoto
  4. ana pato kwa mwezi lisilopungua 900,000/- kama sehemu ya pension yake
  5. ana vimiradi nyumba mbili zinazomlipa 500,000/- kila moja kwa mwezi sawa na 1000,000/-
  6. amejenga frame 5 kila moja anapata 100,000 kodi sawa na 500,000/- kwa mwezi
  7. anavimifugo na bustani ndogo ya kumpiga company ili apunguze sukari na pressure na pia kuendelea na wigo wa kufoka na kutawala wafanyakazi wake wa hizo IGA zake.
  8. kwa kifupi huyu hoja ya basic need hana kabisa
sasa turudi kwa mkopo wetu tukilinganisha na uwekezaji wetu. tuchukue tumenunua security Bond Bank Kuu ya Tanzania kwa kuwekeza milion 200 kwa miaka 5 huku iklipa 2,700,000/- kwa mwezi.
  1. NMB wanawezakutoa mkopo kwa asilimia 17 kwa mwaka na kufanya marejesho kwa mwezi kuwa
    3,818,916.19
  2. kwa muda miezi 60 hivyo ni vizuri ukawa na marejesho japo mawili kabla ya mradi kuanza kwa kuwa fedha utakayolipwa kama faida haitatosha bali itabidi iongezeke kwa shillingi 1,118,916.19 japo kwa mtazamo wa hapo juu mtu huyu anaweza kumudu tu bila shaka.
  3. ukijenga apartment utachelewa jenga nyumba mbili ikiwezekana ghorofa moja yenye bachelor rooms mbilimbili kwa wateja 16 ambacho kila kimoja utalipwa 200,000/- sawa na 3,200,000/- kwa mwezi.
  4. ukitoa gharama za kuhudumia nyumba kama 30% na ukiongeza na deni la benki si haba anabaki 1,121,084.81
kwanini mtu huyu asiimbe wimbo wa taifa vijana mjiajiri!
 
Hapo ongezea Kama una gari tenga laki 2 kila mwezi,bado mavazi haujaenda kuzungusha round baa .
Kwa maisha moderate 1.5m haitoshi ila kwa maisha ya chai na andazi moja hata laki 3 ni nyingi sana
 
Option nyingine ni kuwekeza kwenye real estate. Ukipata kiwanja location inayoeleweka unaweka. Kwa milioni 200 unasimamisha apartments za kueleweka. Hata kwa US$500 kwa mwezi kama ziko 5 utaiona faida.

Apartment 5 kwa milioni 200?! Apartment hizo za udogo au?!
 

Kiwanja cha 30M upate apartment za kupangisha usd 500!? Unaota ndoto ya mchana[emoji23][emoji23][emoji23] maana hizo bei ni mikocheni mbezi msasani huko utapata kiwanja cha 30M?!
 
Option nyingine ni kuwekeza kwenye real estate. Ukipata kiwanja location inayoeleweka unaweka. Kwa milioni 200 unasimamisha apartments za kueleweka. Hata kwa US$500 kwa mwezi kama ziko 5 utaiona faida.
Sky 200M inaweza kujenga apartment 5? sehemu zinazoeleweka?
 
Kiwanja cha 30M upate apartment za kupangisha usd 500!? Unaota ndoto ya mchana[emoji23][emoji23][emoji23] maana hizo bei ni mikocheni mbezi msasani huko utapata kiwanja cha 30M?!
Hata mimi nimeshangaa Kumbe Sky anatulisha kamba
 
1.5m kwa matumizi ya mwezi mzima labda uwe unaishi kisela bila familia na usiwe mtu wa bata sana.
Hapo assumption yake ni kwamba ulishakuwa na nyumba yako watoto walishasoma wanajitegemea umebakia wewe na wife . Ukiamka unasoma magazeti tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…