Kwa kipato cha 1.5m hapo mbona unatoboa kabisa , mwez wa 1unachukua laki 5 unakodi shamba eka 10, mwez wa 2 unachukua laki 8 kwa ajili ya kusafisha na kupanda mpunga shambani, mwez wa 3 unachukua laki 4 kwa ajili ya palizi, baada ya miezi miwili mbele unavuna eka zako kumi za mpunga ambapo kwa wastani wa gunia 10 kwa eka unapata jumla ya gunia 100, kwa bei ya shamba gunia 1 unauza sh elf 80 , kama utauza magunia yote mia utavuna sh mil 8 fasta . Hiyo yote inatokana na faida ya kuwekeza fixed deposit kwamba hela ya kula nyumbani inakuwepo na hapo hapo unapata muda wa kunafanya uwekezaji mwengine juu yake.