Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Dar inapangwa upya, Sinza inasukwa upya, maeneo jirani na Mlimani City yanasukwa upya. Serikali inaenda kutwaa eneo la ukubwa wa mita za mraba 233,000 na kulipanga upya.

Maeneo kama Sinza yana viwanja vya 20/20, na maeneo hayo kwa sasa ndio ujenzi mkubwa wa maghorofa unakuja. Ni vyema serikali imeyatwaa maeneo hayo ili iyamiliki, ifute ramani ya eneo hilo, ifidie, kisha ilipange upya, na kugawa viwanja vikubwa kwa uwekezaji mkubwa.

Kama ujenzi ungeendelea kwa hali ilivyo, maeneo hayo yangekuwa hayana mvuto, na yenye msongamano.

Hii iende mpaka Tandale kwa awamu, tuipate Dar tunayoitaka.

Screenshot_20241207-133429.jpg

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI:

IMG_8793.jpeg
 
Piga ghorofa 20 kwenda juu tu hapo. Ofisi na apartments.

Panga parking za magari za kutosha.

Ongeza miundombinu ya kuongeza maji. Wekeza kwenye mifumo ya maji ya zimamoto na ofisi/ vifaa vyao.

Weka usafiri wa kueleweka wa mwendokasi.

Panga mitaa na shule, parks, open spaces etc.

Dar es salamm ina population growth rate ya 5%. Kwa rate hii, Dar ita double population kila baada ya miaka 15.

Serikali inatakiwa kujiandaa na mfumuko huu. By 2040 Dar itakuwa na watu mara mbili ya sasa.

Njia pekee ya kueleweka kujiandaa ni kujenga kuenda juu.
 
Wakifanikiwa kuipanga upya kimakazi Dar! Na baadae kufanya haya nchi nzima! Hili linaweza kuwa jambo kubwa zaidi la kimaendeleo kuwahi kufanywa katika nchi hii.

Ila kama kupanga na kuijenga upya waanze na maeneo yaliyojengwa vibaya zaidi kama Manzese, Kigogo, Mbagala, Mabibo na kwingneko. Then ndo waende hayo maeneo mengine.
 
Piga ghorofa 20 kwenda juu tu hapo. Ofisi na apartments.

Panga parking za magari za kutosha.

Ongeza miundombinu ya kuongeza maji. Wekeza kwenye mifumo ya maji ya zimamoto na ofisi/ vifaa vyao.

Weka usafiri wa kueleweka wa mwendokasi.

Panga mitaa na shule, parks, open spaces etc.

Dar es salamm ina population growth rate ya 5%. Kwa rate hii, Dar ita double population kila baada ya miaka 15.

Serikali inatakiwa kujiandaa na mfumuko huu. By 2040 Dar itakuwa na watu mara mbili ya sasa.

Njia pekee ya kueleweka kujiandaa ni kujenga kuenda juu.
Umetoa point za maana sana, hongera, lakini Fahamu,
Mapinga pinga chadomo yataanza kuzua maneno ya SHOMBO, ccm songa mbele!...
Katika operation zao wafikirie pia kuitwa VINGUNGUTI.
 
Chini ya Land Acquisition Act, serikali inaruhusiwa kufanya "redevelopment" ya maeneo
Ok,kwaiyo hapo si inatakiwa wananchi wapelekewe taarifa ya maandishi(kama Notice) na wafanyiwe tasmini, square mtr 233,000 eneo kubwa , boko basiaya nadhani lile eneo la wazi karibu na office za Dawasa, na kunduchi kule palipokuwa machimbo zamani,ambako kwasasa wana hati na walishapimiwa
 
Piga ghorofa 20 kwenda juu tu hapo. Ofisi na apartments.

Panga parking za magari za kutosha.

Ongeza miundombinu ya kuongeza maji. Wekeza kwenye mifumo ya maji ya zimamoto na ofisi/ vifaa vyao.

Weka usafiri wa kueleweka wa mwendokasi.

Panga mitaa na shule, parks, open spaces etc.

Dar es salamm ina population growth rate ya 5%. Kwa rate hii, Dar ita double population kila baada ya miaka 15.

Serikali inatakiwa kujiandaa na mfumuko huu. By 2040 Dar itakuwa na watu mara mbili ya sasa.

Njia pekee ya kueleweka kujiandaa ni kujenga kuenda juu.
Ayo maeneo serikali inataka kuweka karakana ya mwendokasi pale mbuyuni na mji mpya wa mashimoni, na pale boko basihaya wanaweka stendi kuu ya mwendokasi
 
Back
Top Bottom