Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ume assume mengi sana ambayo sijasema.Tanzania haikuumbwa kwa ajili ya kila mwekezaji dunia nzima kuja kupewa ardhi hapa.
Hao wananchi unaoshabikia wanyang'anywe ardhi zao uelewe maisha yao ya kiuchumi na kijamii yamefungamanishwa na mahali hapo wanapotaka kuhamishwa. Hivyo kitendo cha kuwaondoa hapo tu hata kama wanalipwa fidia kwanza hiyo fidia sio market value na haiwawezeshi kupata naeneo mengine yenye hadhi sawa na hapo hivyo watarudishwa nyuma kiuchumi na mfumo wao wa maisha utavurugika. Mtu aliyekuwa anapangisha nyumba yake sinza na kuingiza kipato tayari anerudi katika umaskini mkubwa.
Pili hao watu wanaohamishwq wanaenda wapi na kwa gharama za nani?
Kinachofanya makazi yawe duni ni hali za kiuchumi za wananchi hivyo hata majengo ya kisasa, yakijengwa bado kama mtu hana kipato kikubwa hataweza kupanga na kuishi.
Hii sheria ya ardhi inayoruhusu mwananchi kunyang'anywa ardhi yake kwa manufaa ya umma ilipaswa kuvadilishwa.
Ume assume nimesema kila mwekezaji wa dunia nzima aje kupewa ardhi hapo. Sijasema hili.
Ume assume nataka wananchi waondolewe hapo. Sijasema hilo.
Ume assume nataka walipwe fidia isiyo market value. Sijasema hilo.
Ume assume sijui kuwa kuna masuala mengine ya uchumi yanayotakiwa kufanyiwa kazi. Sijasema hilo.
Kote humo ume assume wrong.
Mimi Bibi yangu alikuwa na nyumba hapo Sinza si mbali na Mlimani City. Kuna mjomba wangu karithi yupo mpaka leo.
Ukivunja nyumba kama zile tano na kujenga ghorofa 25, halafu pale chini ghorofa ya chini kabisa kukawa na nyumba tano za wale uliowavunjia nyumba wabaki palepale, ukawalipa fidia ya kuvunja nyumba zao (ya sentimental value)halafu uwaache wawe pale ghorofa ya chini wapangishe watu au kutumia kama nyumba au biashara, hapo unahitaji kuwahamisha waende wapi tena?
Huoni kwamba kuwa hapo si tu hujawahamisha, bali pia umewaongezea value sehemu hiyo itakuwa inavutia biashara zaidi, wanaweza kuzidisha rent na wakiamua kufanya biashara wanaweza kufanya biashara kubwa zaidi?