Chambusiso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 2,592
- 4,640
Unajua mnapenda kujadili vitu vya kufikirika sana. Story za hivi ndio mnapenda. Hilo tangazo na sijui ramani nani kakueleza?
Mm nakueleza uhalisia, pesa ya kulipa watu fidia kwa sqm200000+ inatoka wapi? Ubungo maziwa pale Kuna eneo linatakiwa kuchukuliwa na kulipwa fidia kwa ajili ya BRT depot, toka 2022 hadi leo kesi imeenda mahakamani sababu ya mgogoro wa pesa za fidia kwa wananchi 90 tu. Ni bilion 8 lakini mvutano wake sio kitoto. Leo eneo Kama sinza kwa sqm 200000 unategemea nn? Mnahisi pesa zipo tu?
Wawekezaji walipe fidia kubwa kwa eneo kama Hilo ili kuweka kitu gani kitachorudisha pesa iliyowekwa? Na huyo mwekezaji ni nani? Nakumbuka enzi za JK kulikua na hizi story za kigamboni itatengenezwa kama Dubai.
Nadhani ni Bora tujadili vitu halisia na sio hisia.
Atakayetaka kununua ndiye atakayelipa fidia lakini kumbuka sio lazima iwe fidia ni kwamba wanaolipwa fidia ni maeneo serikali itakayoyataka kwa miuondombinu yake, wengine wote ni kwamba wamepewa ruhusa ya kuuza nyumba/assets zao! Watakasubiri fidia ni barabara zitakapopita na mali za umma zitakapojengwa, wengine wote watauza kwa raia na makampuni yanayotaka
Na miradi ya namna hii kama ina mikopo na misaada inakuja? Who knows, serkali hii ina maovu mengi lakini pia sio lazima kila kitu kiwe kiovu. Itakuwa mpango huu umechukua miaka na wataalam wa nje na ndani kuuandaa hadi umefikia viwango vya hatua hizi, wakati ni ukuta tusubiri na tuone kama hii ambitious project/program itafanana na zingine ila napongeza kwa maono haya hata kama yatachukua miaka 100 yatabaki kwenye historia