PharaohMtakatifu
JF-Expert Member
- Jul 3, 2023
- 713
- 1,208
Umeeongea point tupu.shida iliyopo ni wazazi wenyewe imagine mtoto wa umri miezi6 anaachiwa house girl mama anarudi saa2-3 usiku kesho anaondoka sa12 asubuhi halafu mtoto akifikisha umri wa miaka 3-4 anapelekwa yule anaanza kulelewa huko Kwa kisingio Yuko shule kumbe umeshindwa kumlea wewe.Wazazi wa hiyo miaka uliyoitaja ndio wameshindwa kulea hawa watoto unaowaona leo hawana maadili.
Wazazi wenye maadili huzaa na kutoa watoto wenye maadili. Nyoka hawezi zaa jongoo.
Mbona kuna watoto wenye maadili, kumaanisha walilelewa na wazazi kimaadili.
Mzizi wa wa matatizo yote ni wazazi walioshindwa kutimiza majukumu yao. Ndio walioharibu hiki kizazi.
Jukumu la mzazi ni malezi kwa mtoto. Mtoto unavyomlea ndivyo anayokua.
Kusema sijui mambo ya utandawazi ni uongo na kisingizio cha kipuuzi cha wazazi walioshindwa majukumu yao.
Mtoto anajilea mwenyewe tangu akiwa mdogo unategemea nini?
Unakuta mzazi hajazeeka, hata miaka 60 haijui na haumwi ati anamtegemea mtoto amtunze, mtoto anitafute, upuuzi tuu.
Kila siku nasema hapa, lakini wapumbavu wanateteana na kuona kama nakosa adabu.
Nitakuwaje na adabu na watu waliokimbia majukumu yao?
Umeshindwa kumlea mtoto wako ni nani atakae kulelea? Kulea mtoto ni wajibu wa mzazi hutaki kulea acha kuzaa