Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Maadili yanayotolewa katika nafasi tofauti hasa katika malezi toka kwa watu wa karibu na namba moja ni wazazi na ili kuelekeza vijana/mtoto atende vile inamjenga vizuri yeye kuzunguka jamii hivyo wazazi na walezi ikiwa ndio namba moja katika maadili ya mtoto ukiona yuko kinyume na maadili mema bhas wa kulaumiwa wa kwanza ni mtoto ndipo itafuata mabadiliko hayo mengine kama ya utandawazi n.k

Nje kidogo ,😉😉 na mimi nitafutie mchumba wa kitanzania lakini zingatia maadili.
Wapi tunakosea? Nini kifanyike?
 
Wazazi/Walezi/Walimu/Viongozi wa dini wajitambue na kulichukua jukumu la malezi serious,Serikali pia ihusike kwa namna moja ama nyingine.
Tumshauri nini waziri wetu wa ustawi wa jamii? Maana masikini ya Mungu, ndiyo kwanza plan ya wizara yake ipo kwenye kuandikwa. Wanayoiandika anafahamu mwenyewe ni akina nani.

Wajibu wetu tujadili na kushauri, wakiyapokea haya, wasipoyapokea haya.

Dkt. Gwajima D
 
Sasa watoto wadogo wanaona vibao kata huku mitaani unategemea nini
Wasaz wao wenyewe wanashiriki vibao kata huku wanajumuika na watoto zao
Baba mama mkononi wameshikilia smartgean

Ova
Hilo nalo neno.

Utakuta watoto wadogo wa kuanzia miaka 3 nyumbani wanachezeshwa kukata viuno, na watu wazima, wazazi wakiwemo ndiyo wanamsifia na video clips kuchukuwa na kutumiana kwenye jamii, kama vile kile wanachokishadidia ni chema sana.

Jamii inayaona, inayatazama na kuyachekelea tu. Inabidi kama jamii, unapotumiwa kitu kama hicho tukemee kwa ukali japo aliyekutumia aamke aelewe kuwa hilo si jema.
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunaoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi na walezi ndiyo tulikosea?
Ukitaka kujua maadili yamekua ya hovyo kwa vijana, tembelea Arusha, usikie kiswahili chao, uone mavazi yao, na namna wanavyo jifananisha ktk kitu wasicho nacho, unaona wazi kabisa tunakoelekea ni kubaya sana sana kwa vizazi, wakidhani kupokea watalii watakua ni kama hao watalii ktk maisha yao, kumbe wako Arusha ktk Africa, na mtalii atarejea kwao kuendelea na utamaduni wake

Mji huu unaongoza kwa maadili machafu hapa nchini
 
Ulitaka nieneze chuki za upagani?

Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?
Wewe unazungumzia maadili ya dini yako?
 
Wazazi wa hiyo miaka uliyoitaja ndio wameshindwa kulea hawa watoto unaowaona leo hawana maadili.

Wazazi wenye maadili huzaa na kutoa watoto wenye maadili. Nyoka hawezi zaa jongoo.
Mbona kuna watoto wenye maadili, kumaanisha walilelewa na wazazi kimaadili.

Mzizi wa wa matatizo yote ni wazazi walioshindwa kutimiza majukumu yao. Ndio walioharibu hiki kizazi.
Jukumu la mzazi ni malezi kwa mtoto. Mtoto unavyomlea ndivyo anayokua.

Kusema sijui mambo ya utandawazi ni uongo na kisingizio cha kipuuzi cha wazazi walioshindwa majukumu yao.

Mtoto anajilea mwenyewe tangu akiwa mdogo unategemea nini?

Unakuta mzazi hajazeeka, hata miaka 60 haijui na haumwi ati anamtegemea mtoto amtunze, mtoto anitafute, upuuzi tuu.

Kila siku nasema hapa, lakini wapumbavu wanateteana na kuona kama nakosa adabu.
Nitakuwaje na adabu na watu waliokimbia majukumu yao?
Umeainisha matatizo, hilo ni la kwanza. Linalofatia ni kila tatizo tulichukulie kulitatuwa kwa falsafa ya "Resilience", tuligeuze kuwa fursa.

Tuitafute fursa ya namna ya kuokoa jahazi na kurekebisha tulipokosea ili tusitatuwe kosa kwa kufanya makosa zaidi.

Suala muhimu linalotukabili, ni nini kifanyike kwa kila tatizo tulilonalo linalotuathiri kumomonyoka kwa maadili kijamii?
 
Wewe unazungumzia maadili ya dini yako?
Sielewi kama kuna "dini" ambayo haifundishi maadili mema. Ikiwepo hiyo itakuwa ni ya Kishetani, maana ushetani siku hizi umejaa.

Kabisa, tena kwa kujivunia dini yangu, mimi nazungumzia maadili niliyojifunza kwa mafunzo ya Kiislam.

Una wasiwasi na mafunzo ya Kiislam kimaadili?
 
Sielewi kama kuna "dini" ambayo haifundishi maadili mema. Ikiwepo hiyo itakuwa ni ya Kishetani, maana ushetani siku hizi umejaa.

Kabisa tena, mimi nazungumzia maadili niliyojifunza kwa mafunzo ya Kiislam.

Una wasiwasi na mafunzo ya Kiislam kimaadili?
Wewe ni kama unasema hakuna maadili ya kiafrika tofauti na hayo yaliyoletwa na wageni.

Kumbuka umesema “bila dini hakuna maadili”

Hilo siyo kweli.
 
Umeainisha matatizo, hilo ni la kwanza. Linalofatia ni kila tatizo tulichukulie kulitatuwa kwa falsafa ya "Resilience", tuligeuze kuwa fursa.

Tuitafute fursa ya namna ya kuokoa jahazi na kurekebisha tulipokosea ili tusitatuwe kosa kwa kufanya makosa zaidi.

Suala muhimu linalotukabili, ni nini kifanyike kwa kila tatizo tulilonalo linalotuathiri kumomonyoka kwa maadili kijamii?

Chakufanya ni kuwa kila mtu afanye wajibu na majukumu yake.
Mtoto hana wajibu wa kujilea wala kulea wazazi wake.

Unampa mtoto jukumu la kujilea unajiondolea haki na wajibu wake wa kukuheshimu.

Mtoto akutunze umeshafikisha miaka 60 kuendelea.
Lakini sio kuendekeza uvivu na kumpa majukumu mtoto huyo ni uhuni na Sisi tutausema siku zote. Hilo nimeliona sana.

Angalia watoto wengi waliokosa maadili utagundua asilimia 90% wazazi wao wamekimbia jukumu la malezi.
Nenda kaangalie Malaya, nenda Bara, angalia Wadada wa majumbani, nenda kwa machokoraa.

Vijana wanajitutumua kufanya kazi zozote ilimradi wawatumie WAZAZI (wabinafsi) pesa za kuwatunza.
Alafu huyo mzazi mwenyewe unakuta nguvu anazo, umri haujaenda, kuumwa haumwi. Hiyo ni akili au matope.

Acha mambo yaende jinsi yalivyo. Hiyo ndio namna ya kuisadia dunia. Acha mambo yaende vile yaendavyo.
Hiyo ndio maana ya kizazi cha nyoka.
Unazaa watoto, alafu watoto wanajilea wenyewe
 
Ukitaka kujua maadili yamekua ya hovyo kwa vijana, tembelea Arusha, usikie kiswahili chao, uone mavazi yao, na namna wanavyo jifananisha ktk kitu wasicho nacho, unaona wazi kabisa tunakoelekea ni kubaya sana sana kwa vizazi, wakidhani kupokea watalii watakua ni kama hao watalii ktk maisha yao, kumbe wako Arusha ktk Africa, na mtalii atarejea kwao kuendelea na utamaduni wake

Mji huu unaongoza kwa maadili machafu hapa nchini
Hao watalii wenyewe wanatushangaa sisi kuliko wanyama wanaokuja kuwaona.
 
Wewe ni kama unasema hakuna maadili ya kiafrika tofauti na hayo yaliyoletwa na wageni.

Kumbuka umesema “bila dini hakuna maadili”

Hilo siyo kweli.
Naam nimesema hivyo. Labda tunachotofautiana ni uelewa wa neno "dini".

Wewe ukisikia neno "dini" linamaanisha nini kwako?
 
Chakufanya ni kuwa kila mtu afanye wajibu na majukumu yake.
Mtoto hana wajibu wa kujilea wala kulea wazazi wake.

Unampa mtoto jukumu la kujilea unajiondolea haki na wajibu wake wa kukuheshimu.

Mtoto akutunze umeshafikisha miaka 60 kuendelea.
Lakini sio kuendekeza uvivu na kumpa majukumu mtoto huyo ni uhuni na Sisi tutausema siku zote. Hilo nimeliona sana.

Angalia watoto wengi waliokosa maadili utagundua asilimia 90% wazazi wao wamekimbia jukumu la malezi.
Nenda kaangalie Malaya, nenda Bara, angalia Wadada wa majumbani, nenda kwa machokoraa.

Vijana wanajitutumua kufanya kazi zozote ilimradi wawatumie WAZAZI (wabinafsi) pesa za kuwatunza.
Alafu huyo mzazi mwenyewe unakuta nguvu anazo, umri haujaenda, kuumwa haumwi. Hiyo ni akili au matope.

Acha mambo yaende jinsi yalivyo. Hiyo ndio namna ya kuisadia dunia. Acha mambo yaende vile yaendavyo.
Hiyo ndio maana ya kizazi cha nyoka.
Unazaa watoto, alafu watoto wanajilea wenyewe
Hayo majukumu ya wazazi ndiyo yepi? Tuwe specific, maadili huwezi kuya "generalize."

Ndipo niliposema, unaloliona wewe silo, mzazi mlezi mwengine analiona ndilo bora.
 
Jukumu la mzazi ni kuhakikisha anamlea mtoto mpaka atakapojitegemea, kwani hao wazazi wanashindwa akili na wanyama?

Malezi ni pamoja na kumfundisha mtoto tabia njema, uadilifu, nidhamu, kazi na stadi za Maisha. Ili mtoto ajitegemee.

Na ili mtoto ajifunze hayo yote lazima wewe kama mzazi lazima uwe mfano kwake(Role model)
Kama mzazi mwenyewe huwezi kujitegemea utamfundishaje mtoto ajitegemee?
Hapo ndipo maadili yanapoanza kuyumba, kwenda alijeje.

Mtoto utamfundishaje aache aheshimu Watu ilhali anaona kila siku unawatukana, unawadhulumu, unatoka na waume/wake za Watu?

Au malezi ni hotuba za maneno zilizowashinda wazazi?

Nimeshakuambia Nyoka hazai jongoo.
 
......mi binafsi huwa najiuliza mabinti wa leo kuzaa zaa ovyo ovyo sijui wanajisikiaje, sijui wazazi tumefeli wapi. Binti mdogo kabisa anabeba mimba tena niseme isiokua na baba, mzazi nae atashiriki kumuandalia baby shower shame!! Shame!! Akikaa kidogo kaenda tena kuzaa na mwingine, yani kawaida sahivi kila mtoto kuwa na baba ake.
Kizazi cha 2000+ kina laana...[emoji28]
 
Malezi, tunaiga sana ughaibuni.

Mtoto ana maamuzi, kipi afanye kipi asifanye. Mtoto ananyolewa/kusukwa mitindo ya kiutu uzima anayoona wasanii wavaa utupu wanasuka/kunyoa.

Mtoto anaveshwa hovyo kama kina zuchu na nandy. Mpaka anajitambua akiona mtu kavaa nguo ndefu anamshangaa coz yeye hawezi.

Mtoto anakua akiona tamthilia za mapenzi, makiss kama yote.

Na mbaya zaidi mtoto anakua haijui dini maana si baba wala mama wanaenda msikitini/kanisani wala kumpa nasaha zozote mtoto, zaidi ya kusherehekea kila sikukuu ya kidini.

Yaani madogo wanakua kingonongono tu. Wamedekezwa kiasi kwamba hawezi kuishi na mtu mwingine.

Hawa wa sasa ni cha mtoto subiri 2030.
 
Jukumu la mzazi ni kuhakikisha anamlea mtoto mpaka atakapojitegemea, kwani hao wazazi wanashindwa akili na wanyama?

Subiri niyakatekate majibu yako yajadilike vizuri.

Hilo swali lako umeliuliza kijazba sana, umekuwa "emotional" zaidi ya kujibu.

Nikufahamishe falsafa kidogo; Binaadam ni hatari kuliko mnyama yeyote unayemjuwa wewe duniani. Labda pia nikufahamishe kisayansi, sayansi inajitahidi kutuaminisha kuwa Mwanadamu ni mnyama.

Kidini (Uislam); Binadam siyo mnyama.

Sifahamu kiimani zingine.

Kama wewe ni mtu unayeiamini sayansi zaidi ya Uislam, jibu umeshalipata, kuwa binadam kama ni mnyama basi ni lazima atashindwa akili na wanyama wengine. Hapo hakuna utata.

Lakini Kiislam kama nilivyokwambia juu hapo, mwanaadam siyo mnyama na hawezi kushindwa akili na mnyama, mwanadam anatakiwa awe ni msimamizi (kwa wenzake) na kila kilichopo duniani, wakiwemo binadam wenzake.
 
Malezi, tunaiga sana ughaibuni.

Mtoto ana maamuzi, kipi afanye kipi asifanye. Mtoto ananyolewa/kusukwa mitindo ya kiutu uzima anayoona wasanii wavaa utupu wanasuka/kunyoa.

Mtoto anaveshwa hovyo kama kina zuchu na nandy. Mpaka anajitambua akiona mtu kavaa nguo ndefu anamshangaa coz yeye hawezi.

Mtoto anakua akiona tamthilia za mapenzi, makiss kama yote.

Na mbaya zaidi mtoto anakua haijui dini maana si baba wala mama wanaenda msikitini/kanisani wala kumpa nasaha zozote mtoto, zaidi ya kusherehekea kila sikukuu ya kidini.

Yaani madogo wanakua kingonongono tu. Wamedekezwa kiasi kwamba hawezi kuishi na mtu mwingine.

Hawa wa sasa ni cha mtoto subiri 2030.
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunaoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi na walezi ndiyo tulikosea?
Tatizo chama cha mambuzi
 
Back
Top Bottom