Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Binafsi naamini mambo ambayo tunayaona madogo madogo sanana ya kawaida tu, kama uliyoyasema ya"mavazi" na mengineyo mengi sana, ni mlolongo wa mambo maodgodogo ambayo tunayachukulia ni kawida tu kumbe si kawaida na ni kichocheo kikubwa cha ukosefu wa maadili.

Mavazi kuanzia utotoni, inabidi Watanzania tusichukulie mavazi kwa watoto wadogo ni kitu cha kawaida tu na anaweza kuvalishwa vyovyote tu. Pia unayovaa sisi na tunayowavalisha wajukuu zetu, kwa wengine watoto zetu, iwe nyumbani au nje ya nyumbani, ni muhimu sana.

"dress codes" za kiheshima ni muhimu sana a'all across".Haijalishi wapi na nani, mavavi yetu ni moja ya kichocheo cha ukosefu wa maadili.

Nakumbuka "historia ya ukweli kabisa" Nyerere alipoanza maisha ya Kisiasa jijini Dar alikuja na vazi ambalo kwa siku hizo ni "fasheni", kaptura, na likivaliwa sna na wazungu, alipoanza kutambulishwa kwa wazee akaambiwa hilo vazi sasa wachana nalo, wazee hawatakuelewa, wewe unapigania kuwaondowa wakoloni basi usivae kama wakoloni ambao wazee wanachukulia kinyume cha maadili yao.

Nyerere hakubisha akawacha kuvaa kaptura katika harakati zake.

Siku hizi imekuwa kawaida eti kumkuta mtu kavaa "bukta" nyumbani kwake mbele ya wanawe au watoto wadogo wa kike na wakiume na mbele ya mama zake na baba zake na watu wazima, wengone ndiyo mpaka nje.

Juzi hapa tukaona kundi la watanzania wakivalishwa bukta zilizokunjwa mpaka kuonesha tupu zao na kupakwa mafuta mmeremeto na moosefu wa maadili mmoja, na mijinga, wanawake kwa wanaume wakafata na wengine wanaiga mpaka leo mitaani.

Tumekuwa taifa la ajabu sana.
Nakazia hapa[emoji419][emoji375]
 
Ugumu wa maisha ukosefu wa kazi kipato huchangia sana maadili kuyumba. Maana watu ili mkono uende kinywani wanafanya vitu kinyume na maadili mfano umalaya nk.
Hivi naninkasema zamani maisha yalikuwa marahisi...
 
Yalikuwa na afadhali sana kuliko maisha ya leo. Zamani ukimaliza elimu yako unapewa form ya kuchagua kazi. Sio siku hizi.
Mkuu napinga ukiegemea kwenye cheti na ajira nitakushangaa sana.
Zamani kidato Cha nne walikuwa wanashinda 3-7 tu halafu la Saba wanaweza faulu wanafunzi 9 darasa Zima hata chini ya hapo. Je wale wengine walikuwa Wana ajiliwa na nani hasa walio feli?


Story ni nyingi hasa Kwa wazee wetu wanakuambia Mimi nimesoma na fln na pengine ndo Dr, mwalimu mstaafu Kwa Sasa,Askari nk mbona walibaki na maaadili?
 
Mkuu napinga ukiegemea kwenye cheti na ajira nitakushangaa sana.
Zamani kidato Cha nne walikuwa wanashinda 3-7 tu halafu la Saba wanaweza faulu wanafunzi 9 darasa Zima hata chini ya hapo. Je wale wengine walikuwa Wana ajiliwa na nani hasa walio feli?


Story ni nyingi hasa Kwa wazee wetu wanakuambia Mimi nimesoma na fln na pengine ndo Dr, mwalimu mstaafu Kwa Sasa,Askari nk mbona walibaki na maaadili?
Huo ni mfano mdogo nimekupa. Ipo mingi tu hata matibabu yalikuwa bure sio siku hizi.
 
Zamani hata kabla hujatoa single(wimbo)ilikuwa lazima mashairi yahaririwe ..Leo hii Kwa nyimbo za kina wasafi etc. usitegemee maadili..Zamani hata mke wa mtu alikuwa anazini Kwa Siri mno,Leo hii mke wa mtu anakuomba namba ya simu..
Na ukimnyima anakununia balaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hali ni ya hatari sana mpaka kufika 2030,2035 huko watoto watakuwa wamechakaa

Ova
 
Ulitaka nieneze chuki za upagani?


Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?

CCM haifunzi maadili kwani??
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?

Wazazi wa hiyo miaka uliyoitaja ndio wameshindwa kulea hawa watoto unaowaona leo hawana maadili.

Wazazi wenye maadili huzaa na kutoa watoto wenye maadili. Nyoka hawezi zaa jongoo.
Mbona kuna watoto wenye maadili, kumaanisha walilelewa na wazazi kimaadili.

Mzizi wa wa matatizo yote ni wazazi walioshindwa kutimiza majukumu yao. Ndio walioharibu hiki kizazi.
Jukumu la mzazi ni malezi kwa mtoto. Mtoto unavyomlea ndivyo anayokua.

Kusema sijui mambo ya utandawazi ni uongo na kisingizio cha kipuuzi cha wazazi walioshindwa majukumu yao.

Mtoto anajilea mwenyewe tangu akiwa mdogo unategemea nini?

Unakuta mzazi hajazeeka, hata miaka 60 haijui na haumwi ati anamtegemea mtoto amtunze, mtoto anitafute, upuuzi tuu.

Kila siku nasema hapa, lakini wapumbavu wanateteana na kuona kama nakosa adabu.
Nitakuwaje na adabu na watu waliokimbia majukumu yao?
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunaoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi na walezi ndiyo tulikosea?
Maadili yanayotolewa katika nafasi tofauti hasa katika malezi toka kwa watu wa karibu na namba moja ni wazazi na ili kuelekeza vijana/mtoto atende vile inamjenga vizuri yeye kuzunguka jamii hivyo wazazi na walezi ikiwa ndio namba moja katika maadili ya mtoto ukiona yuko kinyume na maadili mema bhas wa kulaumiwa wa kwanza ni mtoto ndipo itafuata mabadiliko hayo mengine kama ya utandawazi n.k

Nje kidogo ,😉😉 na mimi nitafutie mchumba wa kitanzania lakini zingatia maadili.
 
Sasa watoto wadogo wanaona vibao kata huku mitaani unategemea nini
Wasaz wao wenyewe wanashiriki vibao kata huku wanajumuika na watoto zao
Baba mama mkononi wameshikilia smartgean

Ova
 
Ugumu wa maisha ukosefu wa kazi kipato huchangia sana maadili kuyumba. Maana watu ili mkono uende kinywani wanafanya vitu kinyume na maadili mfano umalaya nk.
AlhamduliLlah, katika umri wangu nimejaaliwa kuishi na kutembelea nchi mbali mbali nje ya Tanzania.

Cha kushangaza, Tanzania niionavyo kukosa kazi kunachangiwa sana na maisha yetu tunavyoishi. Utakuta tumewazowesha vijana "kula kulala" wanapokuwa hawana kazi za kufanya bila kulipia kiaina hiyo" kula kulala".

Utakuta kijana anaweza kwenda kuishi kwa shemeji, mjomba, shangazi, ma mdogo, ma mkubwa au ndugu, jamaa na marafiki akala akalaa bila wasiwasi hata chembe. Na "ukoo" upo adhi kabisa kumpokea na kumweka hata miaka. Mifano hai ni mingi sana.

Hayo hutoyakuta nje ya Tanzania kwa kiwango cha Tanzania, tunajenga au tunabomoa?
 
Back
Top Bottom