Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Labda niulize tena kivingine; "wanawake" wamehusika vipi na kuporomoka kwa maadili kiujumla?

Inawezekana una point nzuri, tulizana, shusha pumzi, kunywa maji, fikiri kidogo halafu ujibu kwa kina.
Sawa ngoja nifikirie nitengeneze hoja nzuri.
 
Kwa hiyo unamaanisha maadili mabovu yanasababishwa na serikali?
Serikali ina mchango mkubwa katika kuporomosha maadili yetu kwasababu inafaidika.

Majuzi hapa kulifanyika event ya kuhusu mambo ya madawa ya kulevya. Unamwita Harmonize ambaye amekuwa mtu kupromote hayo madawa, huku unamwacha MTU kama kalapina ambaye ukiachana na kuimba nyimbo za kutokomeza madawa, ana taasisi ya kusaidia watu kuachana na madawa
 
Upendo Tv muda huu
Kwaya kuu za KKKT Dar es salaam
Zipo Mbezi Luis KKKT.

Wanaimba kitu hichohicho
Ukosefu wa maadili.

Wanasisitiza kukemea uovu na kuwajenga vijana katika misingi ya maadili mema.

Tukemee ushoga

Bwana Yesu Kristo Asifiwe
IMG_20231029_180121_421.jpg
IMG_20231029_180525_872.jpg
IMG_20231029_180619_000.jpg
 
Attachments

  • IMG_20231029_180750_029.jpg
    IMG_20231029_180750_029.jpg
    487.3 KB · Views: 3
Makubwa; ushoga umeingiaje tena hapa???😀😀😀
hatuongelei hapa 100% nikipata ja[o nusu percent ni ushindi mkubwa sana.

Kama ulikuwa huelewi, kumtumikia Mwenyezi Mungu ni kuitumikia jamii.

Mficha maradhi, kifo humuumbuwa.

Wewe ni shoga? Kama "ndiyo", tufahamishe ulianza vipi kuwa shoga ili iwasaidie wengine. Au kwa kuwa wewe shoga basi unataka wote wawe mashoga na au waupende ushoga?
 
Maadili yanaendana na nidhamu ya uoga. Kwa teknolojia ilivyokuwa kila mmoja anajua haki zake, nidhamu ya uoga haipo tena na huwezi kumdanganya mtu anayejielewa kuhusu mambo yanayotokea duniani.

Kwa mazingira ya sasa ni mtu mwenyewe binafsi ajiamulie aishi maadili gani ili kuweza kufanikisha ndoto zake; ndio maana mifumo inatunga sheria leo mpaka kesho katika kulinda maadili.

Miaka ya zamani teknolojia ilikuwa ziro, watu hawajui haki zao; leo watu wameshikilia ulimwengu kiganjani, wanajua haki zao, wanataka 50/50. kwa mazingira hayo maadili yatatoka wapi.

Kama tutatumia mifumo mikali ya mateso kama Korea kaskazini, maadili tunaweza kuyasimamia ingawa tutapigwa vikwazo na tutakufa kwa njaa.​
 
Vitabu vya dini ni muhimu sana, nyinyi wenyewe na watoto zenu wanyimeni vyote msiwanyime maadili mema, na hakuna pakuyapata maadii mema zaidi ya kwenye dini.
Tatizo Hamas wanawafanya watu wasiamini dini tena, na kuchukuliwa kama kikundi cha mafunzo ya ugaidi
 
Ulitaka nieneze chuki za upagani?

Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?
Dini zinasaidia kweli mbona ni mapigano tu dunia nzima. Maybe we need to re-think about dini tuachane nazo tuishi as human being sio as Christians au Muslim au sijui dini zingine.

Mwisho wa siku ni hadaa kudai Mungu atawaangamiza wote wasiofuata dini fulani.
 
"Dini" maana yake nini?
 
Tatizo Hamas wanawafanya watu wasiamini dini tena, na kuchukuliwa kama kikundi cha mafunzo ya ugaidi
ANC pia waliitwa "magaidi", kwanini?

IRA waliitwa "magaidi" kwanini?

"HAMAS" wanqlaitwa "magaidi" kwanini?
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?
Nani wa kulea hayo maadili sasa? Wakati waliotakiwa kuyalea hayo maadili wamekimbilia maofisini wote na kuacha watoto wakichungwa badala ya kulelewa.

Huyo mchungaji mwenyewe sasa qualification pekee aliyonayo ni kwakua yeye aliwahi kuwa mtoto.

Nadhani kunusuru mmomonyoko huu wa maadili inabidi VETA waanzishe course za Home helpers au Home nurses ili wakati mkeo anaenda kazini ajue amemuacha mtu ambaye naye yuko kazini.
 
Wewe unahitaji kuletewa maadili na nani?

Wewe wazazi wako hawajakufunza maadili mema nyumbani?
 
Wewe unahitaji kuletewa maadili na nani?

Wewe wazazi wako hawajakufunza maadili mema nyumbani?
Nilifunzwa vyema na Mama yangu kipenzi, wakati baba akiwa anatafuta mkate.

Tatizo kama nilivyolieleza hapo ni kwamba wazazi wa kike wa sasa wako busy maofisini hivyo kuwanyima watoto fursa ya kupata malezi kama niliyopata mie.

Tatizo hilo namna mojawapo ya kulishighulikia ni Kuanzisha mafunzo ya malezi ambayo yatagawanywa kutokana na mahitaji ya jamii husika.

Mathalani wale wanayotaka watoto wao walelewe kimila, kidini (kiislamu au kikristo), au ki-seculler hivyo utaajiri Home nurses/helpers kulingana na mtizamo wa wazazi wahusika.
 
......mi binafsi huwa najiuliza mabinti wa leo kuzaa zaa ovyo ovyo sijui wanajisikiaje, sijui wazazi tumefeli wapi. Binti mdogo kabisa anabeba mimba tena niseme isiokua na baba, mzazi nae atashiriki kumuandalia baby shower shame!! Shame!! Akikaa kidogo kaenda tena kuzaa na mwingine, yani kawaida sahivi kila mtoto kuwa na baba ake.
Mobito
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?
Mitandao ya kijamii imesababishwa Dunia kua Kijiji na kuingiliana kwa tamaduni za mataifa mbalimbali. Tofauti enzi za Mwalimu ilikua Radio moja tu Radio Tanzania na magazeti ya Serikali na chama tu.
 
Hii maada ntasoma comments tu, natamani ungeweka bayana kadhaa zenye tafsiri au mifano ya maadili ili tupite kwenye hio njia na mengineyo
 
Wengi anasingizia globalization jambo ambalo ni kweli Kwa kiasi chake lkn nimeona familia nyingi tu Zina Watoto wenye nidhamu kubwa pamoja na kwamba wanatumia simu nk.

Mimi naamini sana kwenye malezi ya wazazi wazazi wa meacha wajibu wao wamebase sana kwenye maisha ya kazi(utaftaji) sio dhambi lakini tuangalie kati ya kazi na familia yako kipi Cha msingi zaidi? Hasa wamama amabao hawataki kulea Watoto wao wa kuwazaa kabisa na badala yake house girl ndo anashika hatamu ya kumlelea Watoto wake!
Wazazi wetu waliwezaje kutulia sisi hao wazazi wasiokuwa na elimu wamezalisha ma professor wengi sana lkn Leo ni ngumu sana mtu na PhD yake mtoto wake akawa professor!!

Ebu turudi kweny Nature ya viumbe wengine.

Kuku utamlisha chakula uwezavyo lkn ukishika kifaranga chake hapo hapo anakurarua vibaya mno

Simba akiwa na watoto hawezi kukusamehe kamwe hata chui karibia viumbe vyote wako makini sana Kwa wtoto wao isipokuwa binadamu wa Leo!

Mtoto analelewa karibia na wadada wa kazi 7 na zaidi Hadi anajitambua muda Kila house girl na tabia zake hapo utatoa mtoto mwenye maadili? Akitoka hapo unampele nursery school mtoto wa miaka4 seriously? Anaishi huko kakutana na watoto wenye maadili tofaut na hata walimu wake Bado hawana Watoto hawajui malezi !!

Ni mengi sana FaizaFoxy lkn la msingi ni malezi tu. Umeshindwa kumlea mtoto wewe mwenyew Nan akulele Sasa?
 
Na ushoga nao ni hivyo hivyo?
Zamani kipindi tunasoma kuanzia chekechechea tulikuwa tuna fundishwa na mama mtu mzima mwenye Watoto na pengine kaozesha anajua namna ya kudili na watoto watukutu na kuwalejeza kwenye mstarii Leo hii mwalimu wa chekechechea anamiaka 24-25 Hajaolewa au kuoa hajui hata chembe ya malezi!!
 
Back
Top Bottom