A
Anonymous
Guest
Kwa zaidi ya wiki tatu sasa, maeneo ya karibu na Chuo Kikuu cha SAUT hususan mitaa ya Nyamalango, Maduka Tisa–Buhima na Sweya yanaishi bila maji kabisa. Hali imekuwa mbaya kupita kiasi na inaathiri moja kwa moja maisha ya kila siku ya wakazi.
Mara chache sana maji yanaporudi inakua ni usiki wa manane na the water pressure is extremely low, kiasi kwamba huwezi kujaza ndoo kwa muda mfupi. Unaweza kukaa usiku mzima ukisubiri ili upate ndoo moja tu ya lita 20. Wakazi wanaamka usiku wa manane kusubiri maji, wengine wanalazimika kutembea umbali mrefu au kununua maji kwa gharama kubwa sana, jambo ambalo si la haki wala endelevu.
Hali hii imeleta athari kubwa zikiwemo:
Hali hii si ya kibinadamu na inahitaji hatua za haraka na za dharura. Maji ni hitaji la msingi, si anasa. Tunaomba mamlaka husika zisikie kilio cha wakazi wa maeneo haya na kuchukua hatua za haraka kabla hali haijawa janga kubwa zaidi.

- Kukosekana kabisa kwa usafi binafsi (kuoga, kufua)
- Kuongezeka kwa hatari za kiafya kutokana na upungufu wa maji safi
- Changamoto kubwa kwenye matumizi ya vyoo na usafi wa mazingira
- Kusumbua masomo na maisha ya wanafunzi, kwani maeneo haya yanakaliwa kwa wingi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT