Ukosefu wa waandishi habari vijijini husababisha changamoto lukuki zilizopo huko kukosa utatuzi

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Imezoeleka kuwa habari za vijijini zinapatikana pale kiongozi wa kitaifa akienda huko huku akiongozana na wandishi wa habari toka mjini kwa ajili ya uzinduzi wa jambo fulani kama vile Kisima, Hospital nk lakini baada ya hapo huondoka zao na kurudi walikotoka bila hata ya kuzunguka na kujua changamoto mbalimbali zilizopo vijijini huko.

Hali hii imesabababisha changamoto mbalimbali zilizopo vijijini kusahaulika kabisa,

Moja ya changamoto hizo zinaweza Kuwa ukosefu wa maji safi na salama, ubovu wa miundombinu,Kukosekana kwa Hospital, ndoa za utotoni Ukeketaji wa watoto wa kike nk.

Viongozi kupenda kusifiwa badala ya kukosolewa, hiyo nayo ni shida nyingine inayofanya Habari za vijijini kutosikika na Kutatuliwa na viongozi husika kutokana na Kuwa hawapendi Kukosolewa.

Uminywaji wa uhuru wa habari katika nchi yetu ni Moja ya Mambo yanayofanya wananchi wengi wa vijijini kutotatuliwa changamoto zao au vilio vyao kushindwa Kufika kwenye vyombo vya habari kutokana na Kuwa viongozi Wamekuwa wakiwatishia au kuwaweka ndani waandishi wa habari, na pia kuvifungia vyombo vya habari pindi wanapotumia kalamu zao kuandika changamoto zinazoikumbuka jamii fulani,au kukosoa uongozi.

Viongozi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali waangalie namna ya kuwasiaidia waandishi wa habari katika kuleta changamoto mbalimbali zilizopo vijijini kwani huko ndio kwenye mapinduzi halisi ya kimaendeleo, Taarifa za vijijini zitaamsha mapinduzi makubwa ya maendeleo nchini na pia zitafichua mengi tusiyoyajua.

 
Nashauri! Kwa kuwa wasomi wametapakaa hadi huko vijijini, ni muda sasa wa kujitambua na kuanza kuibua changamoto za vijijini na kuzitupia katika mitandao ya kijamii.

Huko vijijini wana smartphone, wapige picha barabara mbovu na kuzipost mitandaoni.

Waandishi wa habari na vyombo vyao si wa kutegemea, kwa sababu hawako huru kutokana na njaa.

Waandishi wa habari huongozana na kiongozi kwenda kwenye ziara kijijini kwa kulipwa posho na usafiri. Usitegemee mwandishi huyo ataandika mambo hasi.
 
Wazo zuri hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…