Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Hiki unachouliza ndicho nilichokisema kwenye bandiko hili.
Jee umesoma hizo makala 2?.
Nimesisitiza, ili mahakama kutenda haki, sio kwa mahakama kutenda tuu haki, bali haki hiyo pia lazima ionekane imetendeka!.

P
Wapo majaji wenye weredi sana tu.Tatizo ni wanasiasa wameingilia sana mfumo wa kimahakama kiasi cha majaji kubabaika kwenye maamuzi yao na wananchi kuanza kujiuliza juu ya uwezo wao.
 
Wapo majaji wenye weredi sana tu.Tatizo ni wanasiasa wameingilia sana mfumo wa kimahakama kiasi cha majaji kubabaika kwenye maamuzi yao na wananchi kuanza kujiuliza juu ya uwezo wao.
Upashanaji habari umesaidia sana kuonyesha udhaifu wa baadhi ya majaji wetu, na mawakili wa utetezi kwenye cross examination, mfano kwenye kipengele cha The admisibility of evidence, inajulikana wazi admission uliyopatikana kwa torture is not admissible, kwenye zile trial within trial, kuna ushahidi usiotia shaka, makomandoo walikuwa tortured and yet Statements zao zikawa admited!, hata a layman anajiuliza what sort of judges do we have?!.
P
 
Ndugu yangu Mayalla wanasiasa ndio mabosi wetu kwahiyo majaji wamefungwa mikono.kama hiyo kesi unavyosema iko dhahiri kabisa kuwa kuna uonevu fulan.kwa mfano urio anasema aliwapeleka wale makomando kama undercover hivi Bro kwa uzoefu wako ndio undercover anapelekwa vile kweli.ebu niambie Paschal Mayalla.
 
Ina maana jopo la majaji waliofikia huu uamuzi, hawafahamu hili?
 
Ina maana jopo la majaji waliofikia huu uamuzi, hawafahamu hili?
The judges are human beings hivyo wanaweza kukosea kama binaadamu mwingine yoyote na ni mara kibao, majaji kibao errs in law, mahakama ya rufaa inakuja kutengua uamuzi wao, kwa mfano hiyo ya statements obtained by torture, ni jukumu la mawakili wa utetezi kumwaga nondo za precedent with authorities hadi kumfunga jaji mikono asipokee huo ushahidi. Kwa vile guilty verdict inapatikana kwa ushahidi beyond reasonable doubt, kwenye ushahidi wa upande wa mashitaka, umeonyesha just too many reasonable doubts to warrant no case to answer, lakini matundu yote hayo trial judge hajayaona. Waliosema "justice must not only be done, but must be seen to be done" wana maana yao!.
P
 
Ktk nchi hii kama jambo litakuwa interested na ule mhimili uliojichimbia chin zaid lolote laweza kufanyika
 
Kufuatia hukumu ya Kina Halima Mdee na kundi lake, kwenye badiko hili I was right!.
Wanabodi,
Baadhi ya mabandiko yangu sio mabandiko ya average mind ni mabandiko ya deep thinkers, moja ya mabandiko hayo ni Bandiko hili Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Maadam Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya kina Mdee, hiki nilicho andika kwenye bandiko hili, sasa ndio kinakwenda kutokea!. It will be very devastating and disturbing!.

Wale ambao sio average mind, wana uwezo to connect the dots, baada ya Chadema kumtimua Zitto kwa dhulma, there are bad things that happed to Chadema na wahusika wa kadhia ya Zitto, but no one connected the dots and linked the consequences, hivyo sasa baada ya Chadema kuwatimua hawa Wabunge 19, naombeni sasa watch closely what will happen to Chadema and the main players and connect the dots.

God forbids!.
P.
 
Kina Mdee wameshindwa kesi kwa legal technicalities and not points of law. Chadema haikuwatendea haki, mahakama haijawatendea haki, Spika ndie pekee amewatendea haki ila baada ya hukumu ya jana Spika anafungwa mikono, Kina Halima Mdee na kundi lake wanatimuliwa rasmi na sasa hapa ndipo karma unaingia kazini.

Naendelea kusisitiza Kina Halima Mdee na kundi lake watendewe haki, karma is real!.
P
 
Legal technicalities hazikubaliki tena? Kaka kwanini usiiachie hiyo chuki kwa chadema ili uwe huru? Kwanini uteseke? Kwahiyo hiyo karma yako itampata nani, jaji wa mahakama kuu au chadema? Unaamini pia kifo cha aliyekuita mwenye njaa ni karma?
 
Karibu Mitaa hii, uone nilivyowazungumzia majaji wetu.
Pasco
 
Legal technicalities hazikubaliki tena? Kaka kwanini usiiachie hiyo chuki kwa chadema ili uwe huru?
Mkuu Getang'wan, unaamini naichukia Chadema?.
Kwanini uteseke? Kwahiyo hiyo karma yako itampata nani, jaji wa mahakama kuu au chadema?
Karma inampata mhusika tuu wa uovu na sio mtekelezaji wa wajibu wake.
Mfano wale walio m pyu pyu Lissu, kama walitekeleza amri halali, then karma haiwahusu, bali itamhusu aliyewatuma!.
Unaamini pia kifo cha aliye... ni karma?
Hili Sio Swali!, hilo ni jibu!, usiulize majibu, Uliza maswali.
P
 
Uwezo mdogo???? au NI UHUNI
 
Kaka Pascal Mayalla , nje ya mada kidogo: Uteuzi wa majaji umefanyika juzi. Tumeona mwendesha mashtaka wa Zanzibar ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania (Tanganyika ama bara), je hili lipoje kisheria na kikatiba? Mahakama Kuu ni jambo la kimuungano au ni Mahakama ya Rufaa pekee ndio ya kimuungano au ni mahakama kwa ujumla tu ni ya kimuungano? Au ni kuwa huyu Haji Suleiman Haji alikuwa Mwendesha Mashtaka wa Zanzibar lakini ni mtu wa Bara?
 
mfano kwenye kipengele cha The admisibility of evidence
Mwaka jana tarehe 07.12.2021, Jaji Mlyambina alikataa kupokea kielelezo cha kielektroniki mahakamani kwa kudai kuwa kiapo cha authenticity kimeongelea HEARSAY evidence (ushahidi wa kuambiwa), ilikuwa ni video inayoonesha askari polisi watatu wakinikamata isivyo halali. Kifungu kinachoongelea admissibility of electronic vidence hakizuii ushahidi kupokelewa kwa kuwa tu ni hearsay, hilo la hearsay linapaswa kuangaliwa wakati wa kupima uzito wa kielelezo na sio wakati wa kukipokea.

hata a layman anajiuliza what sort of judges do we have?!.
Kwenye trial, nimeeleza kuwa uharibifu ulifanywa kwa kuvunja funguo ya gari langu, Askari polisi aliyeharibu wakati akitoa ushahidi amesema kuwa alivunja funguo ya gari wakati ananikamata ila akaitengeneza, Kwenye hukumu Jaji anasema ninatakiwa kuprove uharibifu uliofanyika na uthibitisho wa risiti ya kununulia funguo.

hiyo ya statements obtained by torture, ni jukumu la mawakili wa utetezi kumwaga nondo za precedent with authorities hadi kumfunga jaji mikono asipokee huo ushahidi.
Jukumu la mahakama sio kumfunga mtu asiye na hatia bali ni kuhakikisha kuwa wanaofungwa na kuadhibiwa ni wale tu wanaokutwa na hatia. S (an infant) vs Manchester City Recorder & Others (1969) Vol III All ER 1230
Jukumu la mahakama kuhakikisha wenye hatia wanafungwa lipo sawasawa na lile la kuhakikisha wasio na hatia wanaachiwa huru.

Yaani hata kama mtu hana wakili, kama atasema aliteswa ndipo akatoa statement, ni jukumu la mahakama kuchambua na kupata ukweli kama statement ilitoka kwa mateso au la, sio liwe jukumu la mtuhumiwa kupambana kuthibitisha hilo. Mahakama kwenye kesi za jinai haikai kama Refa tu bali inachambua kila kitu kuhakikisha hakuna chembe ya shaka inayobaki, na chembe ya shaka ikiwepo tu, faida inaenda kwa mtuhumiwa.
 
Haya maandiko yako mareefu unatuchodha tu bila sababu. Acha unafiki- FULL STOP!
Unajua wazi ukoloni wa ccm ndio sababu ya mahakama kutokuwa huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…