Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Yaani tuna Majaji vilaza ?
 
Yaani tuna Majaji vilaza ?
Kiswahili ni kigumu sana!, kwenye bandiko hili kuna issue yoyote ya ukilaza?.

Hapa tunazungumzia kutosha!, unaweza kuwa na sifa zote na umekidhi vigezo vyote na bado ukawa hutoshi!. Ma JR wote wana sifa na vigezo vya kuwa CJ, lakini bado CJ ameongezewa muda!, do you know what does this mean?.
P
 
Inawezekana pia waliopo hawaoneshi utiifu kwa mama, kwahiyo watafanya kweli na ukweli hautakiwi. Bora awepo zimwi unayemjua kuliko malaika usiyemjua
 
Wanabodi kuanzia sasa, kwenye hoja zangu ninazoibua, zile ambazo zimepatiwa majibu nitakuwa natoa update ya hoja husika na jibu la hoja iliyopatiwa majibu.
Na ikitokea nimetoa hoja kuhusu jambo lolote, hilo jambo likitokea, nitakuwa nakumbushia tuu.
Kwenye bandiko hili nilitoa hoja kuhusu uwezo wa majaji wetu kuwa na jicho la ndani la kubaini haki.

Hoja hii imeleta matokeo chanya ambayo nimeyaeleza hapa
Msikilize Rais Samia anesema nini kuhusu majaji P
Justice must not only be done, but must be seen to be done!.
Jee hii hukumu ya leo, kuhusu issue ya DPW na Bandari zetu, haki imetendeka?. Jee imeonekana kutendeka?.
P
 
.Kwa maoni yangu, tatizo la msongamano wa kesi, sio idadi ya majaji na mahakimu, bali ni ubovu wa sheria zetu na uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu kukosa jicho la roho kubaini hatia, na udhaifu wa vyombo vyetu vya upelelezi.
Bandiko hili ni la siku nyingi ila kwa hii issue ya Dr. Slaa kuzungumza kupindua serikali, na kushikiliwa kwa tuhuma za uhaini, kwa kusikiliza tuu yale matamshi ni sedition case na sio treason, naamini bandiko kama hili litawasaidia vyombo vyetu vya uchunguzi kuwa na jicho la haki na kuwatendea haki. Kama kuna mtu yoyote anaamini Dr. Slaa alitaka kupindua serikali, na kama serikali inapindulika kwa matamshi tuu, then s/he needs h/is/er head seriously be examined!.
P
 
Don't attribute to incompetence something that can be explained by malice. Mhimili wa mahakama wanashirikiana na executive kuminya haki za raia. That simple. But the only constant in this world is change. Wataruja wee lakini watarudi chini. We will be waiting for them.
 
Naunga mkono hoja
 
Naunga mkono hoja
 
Mkuu Nguruvi3 , hili la mhimili wa Mahakama kutokutenda haki ni tatizo kubwa that needs to be addressed properly!. Niliwahi kulizungumza humu Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Hii hukumu ya suala hili imenisikitisha sana, nimeiandikia kitu, na sasa siishii kwenye kuandika tuu humu, mitandaoni na magazetini, bali sasa kuanzia Jumapili hii, naanza kuzungumza public kupitia Channel Ten Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten. Mahakama Zitoe Haki Hata Bila Kuombwa!.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=e1S0KY-zlJOC034E
Naamini kuna vitu ambavyo haviendi vizuri na vinaendelea kwenda mrama kwasababu watu hamvizungumzi, naamini kabisa, mkivizungumzia, publically with honesty and integrity, things will change!.

P
 
Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa hahaki
Karibu mitaa hii nmeandika makala 4 mfululizo magazetini kulalamikia uwezo wa baadhi ya majaji wetu
P
 
Karibu mitaa hii nmeandika makala 4 mfululizo magazetini kulalamikia uwezo wa baadhi ya majaji wetu
P
UTAWAALAAMU MAJAJI NA WENGINEO TU BURE
ILA SHIDA KUBWA NI MAAMUZI YANAYOTOKA JUU
TUACHE KUZUNGUKA MMBUYU
HUO NDIYO UKWELI

MAAMUZI KUTOKA JUU

ova
 
Karibu mitaa hii nmeandika makala 4 mfululizo magazetini kulalamikia uwezo wa baadhi ya majaji wetu
P
paschal, majaji wengi nchi hii huwa wanateuliwa kisiasa. imagine mtu amefundisha chuo, hajapractice mahakamani vya kutosha, anapewa ujaji. wengi huwa akifika mahakamani kama majaji wanaelekezwa hadi na makarani wazoefu, na wanajifunzia kazi palepale, wanaharibu sana sana. jaji anatakiwa kuwa mtu mwenye experience na practice.huwezi kuwa mtu wa theory ukawa jaji mzuri. wengi wanateuliwa kisiasa ili wakiwa pale wawe wanasevu matakwa ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…