Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Februari 1, 2021, Rais Magufuli alimteua Zephrine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa kwa kuwa tu aliandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili. Hukumu yenyewe ilitoka tarehe 29 Januari 2021 kama sikosei, yaani sijui walishauriana saa ngapi na Jaji Mkuu na walishauriana kwa njia gani - simu au maandishi, mtu akala uteuzi; Je kuandika hukumu kwa Kiswahili kweli ilikuwa ndio kitu cha maana kumpa uteuzi wa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa?? Uwezo wa uchambuzi wa sheria wa huyu Jaji ulizingatiwa kweli?? Matokeo ndio haya ya kuwa na majaji wenye uwezo mdogo sana wa sheria pamoja na uchambuzi na kutafsiri sheria.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
TOKA MAKTABA :

6 February 2020

Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli, rais wa TLS atoa nondo kali:

Mfumo wa sheria za jinai ulioko sasa nchini Tanzania , hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji.

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

Dk. Rugemeleza Nshala ameishauri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo Haki Jinai, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.

18 September 2021
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu .

Azungumzia mazito kuhusu

  • Nolle prosequi / kufutiwa mashtaka bila kuelezwa sababu za msingi zaidi ya ofisi ya DPP kusema imeamua kutoendelea na mashtaka
  • Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP
  • Makubaliano kati ya raia na kitu kinachotisha kikubwa yaani raia asiishitaki serikali akiachiwa pia asidai fidia
  • Marekebisho ya sheria yanahitajika ili mahakama iweze kusikiliza haki ya dhamana na ikiwa inafaa mahakama ipewe mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa wakati Polisi na waendesha mashtaka wakiwa wanaendelea kusaka ushahidi
  • Watuhumiwa wengi wanaozea ndani ya mahabusu gerezani kwa muda mrefu wakati inadaiwa vyombo vinaendelea na upelelezi
  • Mtuhumiwa siyo mhalifu mpaka hapo atakapo pata haki yake kwa kuhukumiwa na Mahakama.
  • Hii ya mtuhumiwa kuhukumiwa na Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka au kiongozi yeyote ni uvunjifu wa haki za raia na katiba.
  • Wenye jukumu la kurekebisha mfumo huu Jinai Haki, ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake na bahati kuna wasomi bobezi waliopo ofisini , ni kama Mwanasheria Mkuu Jaji Dr. Feleshi, Waziri wa Sheria Prof. Palamagamba na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Wadau wengine kama TLS, Kituo cha Haki za Binadamu, Vyombo vya Habari na wananchi ni kupaza sauti na kupigia kelele mfumo huu mbovu wa Haki Jinai uliopo sasa hivi.
  • Polisi hawawezi kulaumiwa, wao Polisi hawana jukumu lolote bali kupiga saluti na kutekeleza amri na sheria hii mbovu inayoendesha Mfumo Haki Jamii ( Criminal Justice System) kama wanavyoelekezwa na viongozi wanaowaongoza jeshini na wanasiasa serikalini.
  • Watanzania tuamke toka dhamira zetu zilizo mfu, tupiganie haki hii wote kabisa bila kujali vyeo vyetu, vyama vya kisiasa, itikadi n.k

Rugemeleza Nshala, holds Doctor of Juridical Studies (S.J.D) from the Ivy league Harvard Law School. He holds a Bachelors of Laws Degree (LL.B) from the University of Dar es Salaam, Tanzania (his home country), which he obtained in 1993; the Masters of Laws Degree (LL.M) from Harvard Law School and Masters of Environmental Management (MEM) from Yale School of Forestry and Environmental Studies that he obtained in 1997 and 2007, respectively. Source : Harvard African Development Conference

Haki Jinai / Criminal Justice System

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI​

Imewekwa: Wednesday 15, June 2022

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
View attachment 2471512
Serikali imejipanga kuboresha Mfumo wa Haki Jinai nchini kwa kubaini changamoto na kupendekeza maboresho katika mnyororo mzima wa haki jinai. Hayo yamebainishwa katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau wa Haki jinai nchini. Kikao kazi hicho cha siku tano kimefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu leo tarehe 13 Juni, 2022 Jijini Dodoma.

Dkt. Kazungu amewataka Wadau wa haki jinai kujadili changamoto zinazoukabili mnyororo mzima wa haki jinai na kupendekeza namna bora ya kuboresha mfumo huo ili kujenga mfumo madhubuti wa sheria unaoaminika na jamii katika utoaji haki.

Maoni yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yatatumika kuboresha Andiko la Mapendekezo ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai Nchini kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi 2026/27.

Aidha, Dkt. Kazungu amesema mabadiliko ya mfumo wa haki jinai yamekuja wakati muafaka kwani hayo yamekuwa moja ya maono ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo

Source : https://www.sheria.go.tz/news/serikali-yajipanga-kuboresha-mfumo-wa-haki-jinai

Mkuu bagamoyo, asante kwa hii post, kwa ruhusa yako, naomba kuitumia kama mbolea kuboreshea baadhi ya mabandiko yangu ya kilio cha haki.

Natanguliza shukrani.

Paskali
 
Wanabodi,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Majaji wapya 28 wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema na hapa ninanukuu

Rais Samia akaendelea kwa kuitaja Ibara ya (107) A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mamlaka ya utoaji haki ni Mahakama, “hivyo jukumu lililopo mbele yenu ni kubwa sana, basi ni vyema mkatekeleze majukumu yenu mliyopewa kwa uaminifu, mkaongoze vyema na mkaongozwe na utu na nafsi zenu katika kuwatumikia wananchi,” Mwisho wa kunukuu. Kwa bahati mzuri, mimi nimebahatika kuwa mwanafunzi wa Prof. Ibrahim Juma, hivyo namfahamu vizuri kwa kauli, uwezo na matendo, jicho hilo la rohoni analo, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mahakama ndio mhimili rasmi wa utoaji haki Tanzania, hivyo nina imani kubwa na Mhimili wa Mahakama chini ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, licha ya changamoto za utoaji haki, inauwezo wa kuwapatia haki Watanzania.
Paskali
Update
Wanabodi, hili ni bandiko la zamani likiuangazia uwezo wa baadhi ya Majaji wetu kutoa uamuzi wa haki kwa kukosa jicho la roho la kuangazia haki.

Hoja hii imeleta matokeo chanya ambayo nimeyaeleza hapa
Msikilize Rais Samia anesema nini kuhusu majaji
P
 
Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa haki, naomba kutoa historia fupi ya maisha yangu na jicho la ndani.

Lengo la simulizi hii ni kuwadurusu baadhi ya majaji na mahakimu wetu, jee wana uwezo wa kubaini hatia kwa kutumia jicho la ndani?, jee kwenye utoaji wa humuku zao, wanazingatia "utu na nafsi"?, na sio kutegemea tuu vifungu vya sheria na ushahidi pekee?. Ili jinai itendeke ni lazima kuwepo kwa mambo mawili, actus reus (kitendo cha jinai) na mens rea, (nia ya kutenda jinai). Jee mfumo wetu wa kupata majaji na mahakimu wetu, unahusisha amplitude test kubaini uwezo wa hao majaji na mahakimu kutumia jicho la ndani la utu na nafsi kubaini nia ovu ya kutenda jinai?. Jibu ni hapana!.
Msanii wa Nyimbo za asili ya Kisukuma, Dawa Juma mkazi wa Kijiji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya Tsh. Milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa mahakama ya wilaya Chato, Amalia Mushi, baada ya mshitakiwa kukiri kosa mbele ya mahakama hiyo.
This is a typical case ya this scenario Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Any right thinking member of the society, akiyasoma tuu hayo mashairi, atagundua this man is insane!, huyu sio mtu wa kupelekwa jela, ni mtu wa kupimwa akili na kuanza matibabu!.

GT Pasco nilipoona unamtaja bwana Lakha nilipatwa na shauku ya kumfaham mtu huyu hakika nilipata wasaa wa kusoma kitabu Cha kesi ya uhaini hakika alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa sana.

Pia niligundua kwamba majaji wa kipindi kile walikuwa majaji hasa sio hawa tulio nao sasa wanatia mpaka aibu kuwasikiliza bila hata kusoma hukumu zao ambazo hata mtu asiye na basic ya Sheria akisoma anaona wazi kabisa kwamba hatuna majaji na mahakimu bali wahuni.
 
Kiukweli hili linasikitisha sana!.
P
 
Wanabodi,

Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa haki, naomba kutoa

Kwa maoni yangu, tatizo la msongamano wa kesi, sio idadi ya majaji na mahakimu, bali ni ubovu wa sheria zetu na uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu kukosa jicho la roho kubaini hatia, na udhaifu wa vyombo vyetu vya upelelezi. Mfano kwa tukio kama lile shambulio la Lissu, hata sisi tuu waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji IJ ya siku moja tuu, kubaini chanzo cha wasiojulikana hao, na kukitumia kama lead kuwabaini, lakini kwa vyombo vyetu vya uchunguzi ni mpaka leo hakuna taarifa zozote!.

Kwa bahati mzuri, mimi nimebahatika kuwa mwanafunzi wa Prof. Ibrahim Juma, hivyo namfahamu vizuri kwa kauli, uwezo na matendo, jicho hilo la rohoni analo, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mahakama ndio mhimili rasmi wa utoaji haki Tanzania, hivyo nina imani kubwa na Mhimili wa Mahakama chini ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, licha ya changamoto za utoaji haki, inauwezo wa kuwapatia haki Watanzania.

Paskali
Wanabodi, hili ni bandiko la kitambo, hoja yake ni uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu wetu kuwa na jicho la tatu, jicho la ndani, jicho la roho kubaini haki.

Hoja hii inathibitishwa na kinachoendelea ndani ya mhimili wa Mahakama sasa. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, ametimiza umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria tangu Juni 15, lakini kufuatia kukoseana majaji Rufaa wenye uwezo wa kushika nafasi ya Jaji Mkuu, imebidi Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma aongezewe muda kidogo wakati wa kumuandaa mrithi wake.

Hivyo hoja yangu hii inapata nguvu!, yaani licha ya kuwepo majaji kibao wenye sifa za kuwa Jaji Mkuu, lakini bado hawatoshi, hali inayopelekea Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake, kuongezewa muda mpaka mrithi muafaka apatikane.

Kuongezewa muda huku, kukamuibua Jaji Stella Mugasha Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT? hivyo na mimi nikashauri Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.

Kuna vitu watu tunasema humu, wana wanapinga!. Majaji Rufani wenye sifa za kuwa Jaji Mkuu, wangekuwepo wa kutosha, kusingelikuwa na need kumuongezea muda CJ aliyemaliza muda wake!.
P
 
Kuna vitu watu tunasema humu, wana wanapinga!. Majaji Rufani wenye sifa za kuwa Jaji Mkuu, wangekuwepo wa kutosha, kusingelikuwa na need kumuongezea muda CJ aliyemaliza muda wake!.
Mkuu, wewe umejuaje kuwa majaji wa Rufani waliopo hawana sifa?? Kwa nini hata huyo Mugasha uone hana sifa wakati ameichambua vyema ibara ya katiba na kuitetea kuhakikisha uvunjifu hauendelei kuishi?
 
watu hawaelewi tu. hakuna hakimu au jaji asiyekula rushwa. kama yupo ni wachache sana. ukiondoa majaji wa mahakama ya rufaa, waliobaki woote kwenye judiciary hata uwaongezee milioni mia kwenye mshahara watakula tu rushwa kwasababu mahakama za kiafrika ni rushwa rushwa rushwa.
 
Mkuu, wewe umejuaje kuwa majaji wa Rufani waliopo hawana sifa?? Kwa nini hata huyo Mugasha uone hana sifa wakati ameichambua vyema ibara ya katiba na kuitetea kuhakikisha uvunjifu hauendelei kuishi?
Huenda mheshimiwa Rais kaona ingeleta shida kuwa na CJ mwanamke (hata kama sifa anazo)
1. Rais
2. Spika
3. CJ tena!?
 
Huenda mheshimiwa Rais kaona ingeleta shida kuwa na CJ mwanamke (hata kama sifa anazo)
1. Rais
2. Spika
3. CJ tena!?
Kama tulikuwa nao, wote ni wanaume, kwanini iwe shida wakiwa wanawake?.
P
 
Mkuu, wewe umejuaje kuwa majaji wa Rufani waliopo hawana sifa?? Kwa nini hata huyo Mugasha uone hana sifa wakati ameichambua vyema ibara ya katiba na kuitetea kuhakikisha uvunjifu hauendelei kuishi?
Hili sio swali!. Nimesema waliopo wote hawatoshi ndio maana imebidi aliyepo aongezewe muda wakati mrithi wake akitafutwa!.
P
 
Hili sio swali!. Nimesema waliopo wote hawatoshi ndio maana imebidi aliyepo aongezewe muda wakati mrithi wake akitafutwa!.
P
Ni swali. Aliyeongeza muda hajasema sababu ya kumuongezea muda, wewe umekuja na hitimisho. Ndio napenda kufahamu nini kilichokufanya uwaze hivyo? Ungeweza kusema kuwa kapendelewa lakini umesema kuwa ni kwa kuwa wengine hawana vigezo.
 
Kiswahili ni kigumu, kigezo pekee cha mtu kuteuliwa Jaji Mkuu ni kuwa JR. Hivyo ma JR wote wamekidhi vigezo vya kuwa CJ, sasa inapotokea CJ aliyeyopo amemaliza muda wake, anaongezewa muda, maana yake ni waliopo in line of seniority hawatoshi, hivyo mchakato wa kumtafuta anayetosha ukiendelea. Tofautisha kukidhi vigezo na kutosha!.

Mkuu, mahakamani moja ya sababu ya kumtaka Hakimu au Jaji kujitoa kwenye kesi ni upendeleo. Wote, mdai na mdaiwa, mnakuwa na haki sawa ya kusikilizwa lakini kwa makusudi au kwa sababu azijuazo Jaji au Hakimu anaamua kumpa haki zaidi mmoja wenu (anampendelea). Sasa hata kwa JM ningetegemea nyongeza yake isiyostahiki ioneshe kuwa ni upendeleo, lakini wewe umehitimisha kuwa hawatoshi, na hautoi sababu ya kufikia hitimisho hilo. Masuala ya kutosha hayapo kikatiba.
 
“Hawatoshi” 🤔. Code muhimu sana hii ya chama inayoeleweka na wanachama kindakindaki. Katiba haihusiki kabisa hapa.
 
View attachment 1841771View attachment 1841772

Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila siku za Jumatatu, huwaletea makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambayo huchapishwa na gazeti la Nipashe la Jumapili, ambazo ziko kwa mtindo wa maswali, majibu ya maswali hayo, utayapata wewe mwenyewe, na kisha tutawatafuta wahusika, ku balance hii mada, hivyo kwa mada hizi za mhimili wa Mahakama, mtu wa kubalance tuhuma hizi ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Baada ya makala kuhusu Ofisi ya DPP, wiki hii, naugeukia Mhimili wa Mahakama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Majaji wapya 28 wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema na hapa ninanukuu

“Tatizo la ucheleweshwaji wa kesi katika Mahakama zetu bado lipo, kama mnavyosema Wanasheria haki inayocheleweshwa ndio haki inayokataliwa, hivyo ni imani yangu kuwa baada ya upatikanaji wa Majaji hawa ucheleweshaji wa kesi Mahakamani utapungua na hatimaye haki kupatikana kwa wakati,” alisema Mhe. Rais Samia.

Rais Samia akaendelea kwa kuitaja Ibara ya (107) A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mamlaka ya utoaji haki ni Mahakama, “hivyo jukumu lililopo mbele yenu ni kubwa sana, basi ni vyema mkatekeleze majukumu yenu mliyopewa kwa uaminifu, mkaongoze vyema na mkaongozwe na utu na nafsi zenu katika kuwatumikia wananchi,” Mwisho wa kunukuu.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alimshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi wa Majaji hao wapya huku akiwa na imani kuwa idadi hiyo italeta mabadiliko makubwa ambayo yataonekana mara moja.

Jaji Mkuu, Prof. Juma alisema “Mhe. Rais napenda nichukue fursa hii kukushukuru kwa kutupatia Majaji hawa, idadi hii itasaidia kupunguza mzigo wa mashauri kwa Majaji waliopo na hivyo kusaidia kuleta mabadiliko ambayo yataonekana mara moja,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Prof. Juma, aliendelea “Mhe. Rais idadi ya Majaji inapanda na kupungua kulingana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kustaafu kwa Majaji pamoja na Majaji wengine kupangiwa majukumu mbalimbali, hivyo bado tunaomba kuendelea kupatiwa Majaji kadri nafasi zinapopatikana ili kuendelea kutoa huduma ya haki kwa kuwa wananchi wengi kwa sasa wanafahamu haki zao na hivyo kufungua kesi kwa wingi,” alieleza Jaji Mkuu.

Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa haki, naomba kutoa historia fupi ya maisha yangu na jicho la ndani.

Mimi Paskali Mayalla, zaidi ya kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji, mimi pia mtu wa mastori, yaani stori teller, hivyo kwa wapenzi wa mastori, unaweza kufuatilia sehemu hii ya Mastori ya Pasco Mayalla, ila wewe kama sio mtu anayependa mastori, unaweza ku skip hii segment ya mastori
Mastori ya Pasco Mayalla

Lengo la simulizi hii ni kuwadurusu baadhi ya majaji na mahakimu wetu, jee wana uwezo wa kubaini hatia kwa kutumia jicho la ndani?, jee kwenye utoaji wa humuku zao, wanazingatia "utu na nafsi"?, na sio kutegemea tuu vifungu vya sheria na ushahidi pekee?. Ili jinai itendeke ni lazima kuwepo kwa mambo mawili, actus reus (kitendo cha jinai) na mens rea, (nia ya kutenda jinai). Jee mfumo wetu wa kupata majaji na mahakimu wetu, unahusisha amplitude test kubaini uwezo wa hao majaji na mahakimu kutumia jicho la ndani la utu na nafsi kubaini nia ovu ya kutenda jinai?. Jibu ni hapana!.

Tanzania ili mtu kuwa hakimu, ni kwanza kuhitimu shahada ya sheria, na kuomba ajira ya uhakimu, kwenye kuajiriwa, kupitia Tume ya Kuajiri ya Mahakama iliyo chini ya Jaji Mkuu, ila kwenye hadidu za rejea, hakuna amplitude testi yoyote kupima uwezo wa waombaji kuwa na jicho la ndani la kubaini jinai, na matokeo yake ndio baadhi ya hawa mahakimu kwenye mahakama zetu wenye uwezo mdogo, na matokeo yake ni kwa baadhi yao, kutokuwa na uwezo wa kutoa hukumu za haki huku wengine wakituhumiwa kula rushwa!. Udhibitisho wa tuhuma hii ya uwezo mdogo wa mahakimu wetu kutoa hukumu za haki ni mlolongo wa rufaa, na matokeo ya rufaa nyingi kukubaliwa.

Ili kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ni Tanzania, ni kwanza kuwa mwanasheria, kisha jina lako likapendekezwa na Tume ya ajira ya Mahakama, na kupelekwa kwa rais, mtu unateuliwa kuwa jaji, napendekeza, ili Tanzania tupate majaji kama Lord Denning, tuongeze vigezo vya mtu kuteuliwa Jaji. Kila mtu anaweza kuwa mwanasheria, lakini sio kila mwanasheria anaweza kuwa Jaji. Mfano mzuri ni mtu aliyekuwa DPP kinara wa ukandamizaji wa haki, halafu mtu huyo anateuliwa kuwa Jaji, unategemea nini?!. Kama akiwa DPP alifanya madudu yote yale ambayo sasa ndio yanafumuliwa, akiwa Jaji, atatenda haki?. Unless kama wakati akiwa DPP, baadhi ya maamuzi yake ilikuwa ni kufuata maelekezo, then sasa akiwa Jaji, atakuwa Jaji mzuri, lakini kama akiwa DPP alishindwa kutenda haki, haitegemewi akiwa Jaji atatendaje haki!.

Nchi za wenzetu hadi wana vifaa maalum vya kubaini kama mhusika anasema uongo, (lie detectors), Majaji wetu na Mahakimu lazima wawe na uwezo huo, ili kuepuka kuwatesa watu kwa kuwasweka ndani miaka mingi watu wasio na hatia. Yako mazingira mtu anakutwa na ushahidi wa kuhusika na jinai fulani, na wengine hadi kuhukumiwa kunyongwa, na akiisha nyongwa ndipo ushahidi unakuja kupatikana kuwa amehukumiwa kwa makosa. Majaji na Mahakimu wetu, wakiwa na jicho la rohoni, wataweza kuiona haki na kutoa hukumu ya haki hata kama ushahidi utaonyesha kuhusika.

Kwa maoni yangu, tatizo la msongamano wa kesi, sio idadi ya majaji na mahakimu, bali ni ubovu wa sheria zetu na uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu kukosa jicho la roho kubaini hatia, na udhaifu wa vyombo vyetu vya upelelezi. Mfano kwa tukio kama lile shambulio la Lissu, hata sisi tuu waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji IJ ya siku moja tuu, kubaini chanzo cha wasiojulikana hao, na kukitumia kama lead kuwabaini, lakini kwa vyombo vyetu vya uchunguzi ni mpaka leo hakuna taarifa zozote!.

Kwa kesi kama ya kina Rugemalila, sisi waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji siku 7 tuu, kuwawekea ushahidi wote mezani, lakini vyombo vyetu vya uchunguzi, ni zaidi ya miaka 4 sasa na bado kesi haijaanza kusikilizwa!, kwenye mazingira kama hayo, hata tungekuwa na majaji 100, wangefanya nini?.

Kwa bahati mzuri, mimi nimebahatika kuwa mwanafunzi wa Prof. Ibrahim Juma, hivyo namfahamu vizuri kwa kauli, uwezo na matendo, jicho hilo la rohoni analo, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mahakama ndio mhimili rasmi wa utoaji haki Tanzania, hivyo nina imani kubwa na Mhimili wa Mahakama chini ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, licha ya changamoto za utoaji haki, inauwezo wa kuwapatia haki Watanzania.

Kufuatia mhimili wa mahakama kushiriki Maonyesho ya Saba Saba, makala ya wiki ijayo, nitawaletea ushiriki wa Mahakama kwenye Saba Saba.

Paskali
Update
Wanabodi kuanzia sasa, kwenye hoja zangu ninazoibua, zile ambazo zimepatiwa majibu nitakuwa natoa update ya hoja husika na jibu la hoja iliyopatiwa majibu.

Kwenye bandiko hili nilitoa hoja kuhusu uwezo wa majaji wetu kuwa na jicho la ndani la kubaini haki.

Hoja hii imeleta matokeo chanya ambayo nimeyaeleza hapa
Msikilize Rais Samia anesema nini kuhusu majaji
P

sina mashaka na uwezo wa mahakimu au majaji wetu Tanzania, BUT sina imani nao kabisa kwa sababu wana itikadi za CCM ya Ole Sabaya, na Pole pole, ya Bashiru, ya Makonda nk. Tangu CCM iingiwe na roho ya ku inflict pains to innocents mahakimu wetu wamekuwa wakiakisi nia hiyo. Hata kama kesi ya kubambika ya Mbowe, au ya masheikh, au ya wale waliohukumiwa maisha kutokana na kesi ya uchaguzi kufutwa bado BADO JINSI KESI HIZO ZILIVYOENDESHWA NA MAJAJI WETU HATUTASAHAU. HIVI KWELI MTU ALIYETUMIKA KUWAPORA WATU FEDHA KUPITIA PRE BARGAIN ANA KUWA JAJI????? Sidanganyiki. sina shida na CCM shida yangu ni roho tesi iliyowaingilia.
 
Mkuu unataka kuitenga CCM na dola (mahakama) na watendaji wake? Hapo umeshadanganyika! Hiyo roho tesi iliyomo ndani yao ndio CCM yenyewe!

Huwezi kupewa nafasi ya maana katika serikali ya CCM kama huwezi kuwa na “roho ya kutu” mara ikibidi!
 
Back
Top Bottom