Ukraine na uwezo wa medani waishangaza dunia

Ukraine na uwezo wa medani waishangaza dunia

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,026
Kufuatia uvumizi wa urusi ndani ya ardhi ya jirani yake ukraine dunia imeshuudia kwa mara nyingine sura halisi ya uzalendo na uwezo wa watu kulinda uhuru wao. Kwa sababu zake mwenyewe wengi walitarajia compaign ya babu putin ingeweza kufanikiwa mapema ikizingatia uwezo wa jeshi lake katika nyanja zote za medani ila hali imekuwa tofauti maana ni mwezi sasa vikosi vyake vinahonja juice chungu ya wanaume wazalendo walioamua kufa wakiilinda nchi yao

Kwa vijana ambao hawajasoma historia kwa mapana yake Russia chini ya Stalin aliwahi kutuma jeshi lake kuvamia kitaifa kidogo cha Finland alichokutana nacho mpaka sasa hawezi kusimulia maana alichapika kwelikweli, niwaambie kuwa na jeshi kubwa ni jambo moja ila kwenye uwanja wa medani ( battle field) ni kitu kingine kwani ndani ya miezi mitatu warusi ( wajamaa wenzetu) walichakazwa na jeshi dogo lilojaa wakulima lakini shupavu na hodari. Kuna mtu anaitwa simo hayha au white death anatajwa kuwa sniper hatari zaidi kuwahi kutokea duniani, jamaa aliwafyeka sana wasocialist sio mchezo.

Kuna vijana wengi wako sympathetic na ukraine kuwa ni bora angejisalimisha kwa putini badala ya kutinisha misuli dhidi ya mbabe ni ukweli wengi hawajui maana halisi ya uzalendo zaidi ya kusoma na kusikia kwa wanasiasa wetu wakitafuta mtaji wa siasa.

Licha ya kuzidiwa kila kitu na urusi bado watu wa Ukraine wanasababu ya kupigania nchi yao dhidi ya uvamizi wowote ule kama ambayo wanatoa mechi ngumu kwa majeshi dhaifu ya babu putin, najua kuna watu watapinga ila ukraine wanakitu ambacho russia hana nacho ni morale na uhodari ndani ya uwanja wa medani. Ukraine wameshinda maeneo muhimu yaani morale victory na propaganda na ndio maana hawakupunic baada ya kuvamia wamesimama na kupambania ardhi yao.

Russia historically inakabiliwa na nidhamu ya uoga kutokana na ucommunist ambao msingi wake nikuwafanya watu kuwa humble submissive kwa viongozi wao hili lipo hata kwetu tz kwa waswahili. Hata kwenye vita ya pili ya dunia warusi walikufa sana sababu ya top down decision making yaani Rais akiakiamua amemaliza hata kama taarifa zinaonesha kuna mtego, rejea Stalin alipuuza taarifa za kijasusi kuwa Hitler angevamia kilichotokea ni historia mpaka leo.

Wepiganaji wa ukraine na mercenaries wameonesha weledi kwenye uwanja wa medani kwani mpaka sasa urusi hajafanya significant advance zaidi ya kurusha makombora akiwa mbali maana kwenye ground ni mchumba tu anatomaswa tomaswa na St javelin. Analyst wengi wanafanya speculation kuwa mfumo wa utawala wa uongozi umeoza au hawakujipanga vizuri na mission. Wanajiuliza inakuaje wanashindwa kuwa simple logistics kama mafuta ya kutosha ili kunywesha vifaru na magari. Kitu kingine ukraine wamefanya nikuwapa junior officers kufanya maamuzi badala ya kusubili wakubwa wao. Kuharibu supply line kumewatesa vijana wa Putin kwa aibu wengine wameonekana wakiiba kuku na chakulu kwenye supermarket.

Wanaodhani Russia ni super power anaweza kushindana na mabeberu alete fact kwenye uwezo wa Russia umeonekana wazi na mbinu za kizembe
 
Hiyo vita usiichukulie kirahisi hivyo
Bila Nato huyo zelensky aishatoka kitambo,na Russia atashinda tu mark my words,ni muda tu..
Naakisha shinda beef anahamishia Kwa wanaa wanaojidai kumsaidia🤸
 
kwa miji ilivyo geuzwa kifusi namna ile? utafikiri ukraine imepigwa na garika la sodoma na gomola
Ni kweliView attachment 2163101
Screenshot_20220324-064344.jpg
 
Propaganda zinafanywa na ulaya na USA .hao Ukraine target ya kwanza ni kuwaondolea hata hiyo nguvu ya propaganda,angalia riport ni za upande mmoja wa Ukraine,Tena zilizo chanya zaidi.🏃

Propaganda zinafanywa na ulaya na USA .hao Ukraine target ya kwanza ni kuwaondolea hata hiyo nguvu ya propaganda,angalia riport ni za upande mmoja wa Ukraine,Tena zilizo chanya zaidi.🏃
Ndugu unapaswa kwanza kujua propaganda machinery na dhima yake ndani ya uwanja wa medani, war propaganda ni silaha kama kifaru mana ni taarifa zilozopikwa kubomoa au kuboost morale ya wapiganaji walioko front au wanaotarajia kuingia. Kaka Russia walifanya propaganda kuwa waukraine hawako happy na uongozi wao hivyo watapokelewa kama wakombozi, ila ilikuwa tofauti baada ya kuface resistance. Propaganda kaka ni sehemu ya vita
 
Hiyo vita usiichukulie kirahisi hivyo
Bila Nato huyo zelensky aishatoka kitambo,na Russia atashinda tu mark my words,ni muda tu..
Ni kweli ndugu, ukraine anapata back up ya mabeberu , but these men have strong balls, Russia in its military power amepata casaulities wengi Russia mwenyewe amethibitisha
 
Ndugu unapaswa kwanza kujua propaganda machinery na dhima yake ndani ya uwanja wa medani, war propaganda ni silaha kama kifaru mana ni taarifa zilozopikwa kubomoa au kuboost morale ya wapiganaji walioko front au wanaotarajia kuingia. Kaka Russia walifanya propaganda kuwa waukraine hawako happy na uongozi wao hivyo watapokelewa kama wakombozi, ila ilikuwa tofauti baada ya kuface resistance. Propaganda kaka ni sehemu ya vita
Bahati mbaya propaganda haitoki jikoni nyumbani,zinatoka majiko ya nyumba za majirani Tena wambali,hivyo kulishwa sumu nje nje🤸
 
Kuna baadhi ya miji warusi waliingia sasa hivi wanatanani kutoka ila hata hivyo njia ya kutoka nayo ni ngumu.
Utatuma je vifaru na magari ya kijeshi yakiwa yamesheheni wanajeshi bila kupiga mahesabu ya plan B?
Russia waliingia na plan yao A kwamba wanachukua nchi ndani ya mda mchache.

Hawakufikiri ikiwa hiyo plani itafeli nini kitachukua nafasi. Ndio huko sasa unasikia wameishiwa mafuta na chakula. Hata kama urusi itatuma makombora ya mbali kuharibu majengo ya miji kama wanavyofanya ni jambo gumu kwa jeshi la ardhini kuingia mjini kupora matumizi maana inalindwa na wazalendo walio apa kufa wakilinda haki ya hati miliki ya taifa lao.

Sasa imebaki mjini hakuingiliki, nyumbani hakurudiki.
 
Bahati mbaya propaganda haitoki jikoni nyumbani,zinatoka majiko ya nyumba za majirani Tena wambali,hivyo kulishwa sumu nje nje🤸
Kaka kujua kuwa hii ni propaganda unapaswa kufanya analysis ili kupata hitimisho, hata hivyo propaganda hazipikwi kwa bahati mbaya zinazalishwa kwa malengo maalumu, kwa mfano wa communist walikuwa wanaonesha kutupa chakula kuonesha wanacho kingi lakini kimsingi njaa inawaua, Russia pia anafanya propaganda licha ya kuwa kazidiwa kwenye hizi medani, kwa mfano picha zilizoonesha wanajeshi wa urusi wanatoa msaada wa kibinadamu ni propaganda like
 
Kwani nawe umepata ajira kuwa propaganda machine ya waukrain Kwa mgongo wa Nato au ni mzalendo wa Ukraine ya bongo.?

Back
Top Bottom