Ukraine na uwezo wa medani waishangaza dunia

Ukraine na uwezo wa medani waishangaza dunia

Bado URUSI hajatangaza Vita lakini Tayari Zelensky keshaomba Msaada kila pande ya Dunia!
Leo watu Wamagharibi wanataka Sisi watu Weusi tuwaunge mkono kuinyanyasa URUSI!
Ulaya na Marekani wanaipa msaada Ukraine wa kila kitu ili kuidhibiti hii Operation ya kijeshi!
Lakini watu wanazidi kuikimbia Nchi yao,Rais wao yuko desperate!

Mungu aepushie mbali isitokee URUSI akatangaza VITA na Ukraine pamoja na Washirika wao!
Huko Ulaya kutageuka Majivu.
Hakutakuwa na Mshindi.
Dunia itakuwa ngumu sana kuishi.
 
Atakapokubali kushindwa na nchi ipo total destroyed..uje tena na bandiko lingine la kumponda kwa kufanywa jinga na Western
Ukraine sio wajinga, siku zote kunakofuka moshi ujue kuna moto Huu ni ugomvi wa ndugu umeanza kitambo sana, wamesimama kulinda uhuru wa nchi yao, wamekubali kufa kuliko kusurrender kwa Mrusi, kwa akili yako ulitaka wajisalimishe kizembe. Wewe inawezekana huwezi hata kuua nyoka akivamia nyumba yako utaikimbia na kwenda kulala nje
 
Bado URUSI hajatangaza Vita lakini Tayari Zelensky keshaomba Msaada kila pande ya Dunia!
Leo watu Wamagharibi wanataka Sisi watu Weusi tuwaunge mkono kuinyanyasa URUSI!
Ulaya na Marekani wanaipa msaada Ukraine wa kila kitu ili kuidhibiti hii Operation ya kijeshi!
Lakini watu wanazidi kuikimbia Nchi yao,Rais wao yuko desperate!

Mungu aepushie mbali isitokee URUSI akatangaza VITA na Ukraine pamoja na Washirika wao!
Huko Ulaya kutageuka Majivu.
Hakutakuwa na Mshindi.
Dunia itakuwa ngumu sana kuishi.
Ulichokiona mpaka sasa ndio uwezo halisi wa Russia kwenye vita. Nadhani Putin anamshukuru Mungu alinzisha vita na nchi kama Ukraine, angeanza kwa NATO ingesababisha Urusi kutekwa yote tena ndani ya muda mfupi.
 
vijana wa kibongo niwaoga waoga ndio wanaongoza kuwashauri waukraine wajisalimishe wangejiuliza nyerere angejidalimisha kwa idamin leo ingekuwaje
Kwa sababu hawajali national integriy pia inferiority complex ni tatizo, lakini wenzetu wa ng'ambo kufia vitani kwa ajili ya nchi yao kitu cha kawaida, vijana wa Zamani walitembe kilometre nyingi sana kwa mguu kumuadabisha idd Amini baada ya kuvamia nchi yetu, lakini vijana wa leo hawana uwezo hata wa kuoa fisi akivamia zizi la ng'ombe
 
Kufuatia uvumizi wa urusi ndani ya ardhi ya jirani yake ukraine dunia imeshuudia kwa mara nyingine sura halisi ya uzalendo na uwezo wa watu kulinda uhuru wao. Kwa sababu zake mwenyewe wengi walitarajia compaign ya babu putin ingeweza kufanikiwa mapema ikizingatia uwezo wa jeshi lake katika nyanja zote za medani ila hali imekuwa tofauti maana ni mwezi sasa vikosi vyake vinahonja juice chungu ya wanaume wazalendo walioamua kufa wakiilinda nchi yao

Kwa vijana ambao hawajasoma historia kwa mapana yake Russia chini ya Stalin aliwahi kutuma jeshi lake kuvamia kitaifa kidogo cha Finland alichokutana nacho mpaka sasa hawezi kusimulia maana alichapika kwelikweli, niwaambie kuwa na jeshi kubwa ni jambo moja ila kwenye uwanja wa medani ( battle field) ni kitu kingine kwani ndani ya miezi mitatu warusi ( wajamaa wenzetu) walichakazwa na jeshi dogo lilojaa wakulima lakini shupavu na hodari. Kuna mtu anaitwa simo hayha au white death anatajwa kuwa sniper hatari zaidi kuwahi kutokea duniani, jamaa aliwafyeka sana wasocialist sio mchezo.

Kuna vijana wengi wako sympathetic na ukraine kuwa ni bora angejisalimisha kwa putini badala ya kutinisha misuli dhidi ya mbabe ni ukweli wengi hawajui maana halisi ya uzalendo zaidi ya kusoma na kusikia kwa wanasiasa wetu wakitafuta mtaji wa siasa.

Licha ya kuzidiwa kila kitu na urusi bado watu wa Ukraine wanasababu ya kupigania nchi yao dhidi ya uvamizi wowote ule kama ambayo wanatoa mechi ngumu kwa majeshi dhaifu ya babu putin, najua kuna watu watapinga ila ukraine wanakitu ambacho russia hana nacho ni morale na uhodari ndani ya uwanja wa medani. Ukraine wameshinda maeneo muhimu yaani morale victory na propaganda na ndio maana hawakupunic baada ya kuvamia wamesimama na kupambania ardhi yao.

Russia historically inakabiliwa na nidhamu ya uoga kutokana na ucommunist ambao msingi wake nikuwafanya watu kuwa humble submissive kwa viongozi wao hili lipo hata kwetu tz kwa waswahili. Hata kwenye vita ya pili ya dunia warusi walikufa sana sababu ya top down decision making yaani Rais akiakiamua amemaliza hata kama taarifa zinaonesha kuna mtego, rejea Stalin alipuuza taarifa za kijasusi kuwa Hitler angevamia kilichotokea ni historia mpaka leo.

Wepiganaji wa ukraine na mercenaries wameonesha weledi kwenye uwanja wa medani kwani mpaka sasa urusi hajafanya significant advance zaidi ya kurusha makombora akiwa mbali maana kwenye ground ni mchumba tu anatomaswa tomaswa na St javelin. Analyst wengi wanafanya speculation kuwa mfumo wa utawala wa uongozi umeoza au hawakujipanga vizuri na mission. Wanajiuliza inakuaje wanashindwa kuwa simple logistics kama mafuta ya kutosha ili kunywesha vifaru na magari. Kitu kingine ukraine wamefanya nikuwapa junior officers kufanya maamuzi badala ya kusubili wakubwa wao. Kuharibu supply line kumewatesa vijana wa Putin kwa aibu wengine wameonekana wakiiba kuku na chakulu kwenye supermarket.

Wanaodhani Russia ni super power anaweza kushindana na mabeberu alete fact kwenye uwezo wa Russia umeonekana wazi na mbinu za kizembe
Wanasema Mungu amewashukia Ukraine maana wanajeshi wa Russian wanasaidia kuwamaliza wenzao... Yani wameamua kulinajisi Taifa lao la Rassia...
 
Point yangu ni uwezo wa medani ambao ukraine wametuonesha, point ni national spirit yaani watu kuwa na uchungu na taifa lao. Ni kweli kuwa Russia amemzidi vitu kalibu vyote ukraine lakini kwenye hii vita Russia ametepeta mpaka anafanya uharibifu wote huo, hata kama weye ni shabiki wa putini babu yako ameonekana insane coz ameharibu Maisha ya jirani yake hii chuki hataisha kirahisi ipo siku waukraine watalipa kisasi
Vipi Iraq,Syria na Afghanistan kwenyewe hakukuharibiwa?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema Mungu amewashukia Ukraine maana wanajeshi wa Russian wanasaidia kuwamaliza wenzao... Yani wameamua kulinajisi Taifa lao la Rassia...
Inasikitisha sana, yaani top down decision sio jambo jema sana kwenye dunia ya leo, kuna mawasiliano ya wanajeshi ya Russia yamevuja yanatia huruma Sana, maana baadhi ya makombora yanawaangukia wao wenyewe, na taarifa zingine japo nivigumu kudhibitisha kuwa unit zilizogoma kusonga mbele zimenyimwa supply zijifie zenyewe
 
Vipi Iraq,Syria na Afghanistan kwenyewe hakukuharibiwa?.

Sent using Jamii Foru

Vipi Iraq,Syria na Afghanistan kwenyewe hakukuharibiwa?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uonezi wowote unaofanywa na yoyote lazima upigwe, haimanishi beberu mkuu alikuwa right kuivamia afighanistan japo kwa kipindi hicho ilikuwa imegawika na issue za Taliban na Sharia law, kuhifadhi magaidi na kadhalika hata Russia mwenyewe alishawahi kuivamia afighanistan akachakazwa akaondoka, ila sasa Russia kuivamia ukraine kume expose uwezo wa mabeberu kwenye kupika propaganda na uwezo pia wa ukraine kupambania nchi yao
 
Hizi mashine nazisikia sana ktk hii vita, inasemekana hazikosei kabisa.
Achana ni hizi mzee baba kuna uzi jamaa kaandika kuwa zama za vifaru zimefika mwisho maana vinakaangwa sio mchezo, technical specifications zake ni habari nyingine, yaani ni automatic ukichungulia tu ukipata target ukapiga imo
 
Na inashika namba 4 ktk silaha za kuangusha vifaru, sasa fikiria kuhusu hiyo namba 1 ya mfaransa.
Wafaransa hawatajwi lakini wako vizuri kwenye kuunda silaha, wanaunda fighting jet bora zaidi duniani rich beberu mkuu anakuwa overrated na f 35 zake
 
Bado URUSI hajatangaza Vita lakini Tayari Zelensky keshaomba Msaada kila pande ya Dunia!
Leo watu Wamagharibi wanataka Sisi watu Weusi tuwaunge mkono kuinyanyasa URUSI!
Ulaya na Marekani wanaipa msaada Ukraine wa kila kitu ili kuidhibiti hii Operation ya kijeshi!
Lakini watu wanazidi kuikimbia Nchi yao,Rais wao yuko desperate!

Mungu aepushie mbali isitokee URUSI akatangaza VITA na Ukraine pamoja na Washirika wao!
Huko Ulaya kutageuka Majivu.
Hakutakuwa na Mshindi.
Dunia itakuwa ngumu sana kuishi.
Hiki unachoomba ndicho nami ninachoomba.
 
Ulichokiona mpaka sasa ndio uwezo halisi wa Russia kwenye vita. Nadhani Putin anamshukuru Mungu alinzisha vita na nchi kama Ukraine, angeanza kwa NATO ingesababisha Urusi kutekwa yote tena ndani ya muda mfupi.
Unless akimbilie nuclear.
 
Ndugu unapaswa kwanza kujua propaganda machinery na dhima yake ndani ya uwanja wa medani, war propaganda ni silaha kama kifaru mana ni taarifa zilozopikwa kubomoa au kuboost morale ya wapiganaji walioko front au wanaotarajia kuingia. Kaka Russia walifanya propaganda kuwa waukraine hawako happy na uongozi wao hivyo watapokelewa kama wakombozi, ila ilikuwa tofauti baada ya kuface resistance. Propaganda kaka ni sehemu ya vita
Kwenye vita ya pili ya dunia US walikuwa na kikundi kinaitwa Ghost army, kilikuwa kinafanya propaganda na matokeo ya kumfanya mgermany achanganyikiwe.
Mfano kutengeneza vifaru fake kumbe ni mabaloon yamejazwa upepo n.k
 
Hii mbinu waliitumia hata waingereza, wanaweka vifaru fake kuzitega ndege Germany maana zilikuwa hatari zana pilot wake walikuwa trained kwelikweli, Germany hatajwi lakini hawa jamaa wakiamua kulejenga jeshi lao niwadeadly balaa
 
Pia uingereza walitegesha maiti wameivisha gwanda la kjeshi ikiwa na vtambulisho ma briefcase yenye masterplan ili kumlaghai mgermany na kweli akaingia king kwa kudhani wana mpango wa kuvamia sehemu nyingine
 
Back
Top Bottom