Ukraine yafanya mashambulizi ndani ya Urusi tena karibu na Moscow

Huyu jamaa si jana tu hapo alikuwa anataka akutane na putin wafanye mazungumzo wayamalize kaisha kubali kushindwa?
Always appear weak when you are strong.
 
Nikwambie tu Vita ikapoisha Ukraine wataijenga Nchi yao, wakati sisi na wewe tuko pale pale, na kwa taarifa yako licha ya Vita Ukraine umeme, Internet, Maji na Hospitali bado wana huduma nzuri kuliko 90% ya nchi za Africa
Kuna matrilioni kadhaa za warusi yalikuwa yamehifadhiwa na mabilionea na urusi ulaya, yote yamepigwa pini, wamesema kuwa vita vikiisha, pesa hizo zitatumika kuijenga Ukraine.
 
hapa inabidi tuungane na MK254 kuamini mrusi ni super power wa mchongo ila nahisi kuna hujuma ndani ya jeshi la Urusi na kama Putin asipoangalia anaweza pata pigo moja la hatari
Sio hujuma watu wenye akili za kuweza kutengeneza appstore, android, windows software wameanza kufanya KAZI. Tutegemee makubwa kwa warusi kupata shida katika hii dunia
 
Mbona tuliambiwa anga la Urusi limefungwa na hata punje ya mchele haikwepi rada za Urusi
 

Punguza ushabiki
 
Huyu jamaa si jana tu hapo alikuwa anataka akutane na putin wafanye mazungumzo wayamalize kaisha kubali kushindwa?

Mnayumbishwa na kuyumba, dogo anaendelea kuonyesha ulimwengu picha ya unyonge na anayedhulumiwa, maana tangu mwanzo amekua akiomba wayamalize, ila chini kwa chini anang'ata, na Putin alivyo mjinga anaingia kwenye huo mtego kichwa kichwa.
Hata shuleni kuna wanafunzi wa kihivyo, wachokozi sana kimya kimya ila maneno ambayo huwatoka mdomoni kwa sauti utadhani wanaonewa sana, uspokua makini kama mwalimu utaishia kuadhibu asiye.
Dogo amekua akimburuza Urusi kwenye huu ugomvi, analialia na kuomba wayamalize kwenye runinga na press conferences zote tangu siku ya mwanzo, ila amepokea masilaha kama yote na ameyatumia kuua Warusi wengi sana na kulipua zana zao, amemtia Putin hasira na hasara na kumtamausha pakubwa maana Putin alidhani gemu ataimaliza ndani ya siku chache atakua amempindua dogo na kuweka pandikizi lake Kiev.

Hiyo picha ya dogo anayocheza ya kuonyesha unyonge na ambaye analialia imesababisha aonewe huruma sana na ulimwengu na kufanya Putin aonwe kama bonge la shetani, ni wachache tu ndio mnamsifia Putin. Leo hii hata China imeanza kumchoka maana amekawia sana sio ambavyo ilikusudiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…