Ukraine yaharibu ndege vita 40 za Urusi leo

Ukraine yaharibu ndege vita 40 za Urusi leo

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
73,321
Reaction score
103,590
Ukraine imesema imekamilisha shambulio lake kubwa zaidi la masafa marefu tangu vita na Urusi kuanza, baada ya kutumia droni zilizosafirishwa kwa siri kushambulia kwa pamoja ndege za kivita takriban 40 katika kambi nne za kijeshi nchini Urusi siku ya Jumapili.

Rais Volodymyr Zelensky alisema operesheni hiyo iliyopewa jina la "Mtandao wa Buibui" ilihusisha droni 117 zilizotumiwa na idara ya usalama ya SBU, na kushambulia "asilimia 34 ya ndege za Urusi zinazobeba makombora ya kimkakati ya cruise".

Vyanzo vya SBU viliiambia BBC News kuwa maandalizi ya mashambulizi hayo yalichukua mwaka mmoja na nusu.

Urusi ilithibitisha kushambuliwa kwa maeneo matano, ikiyaita mashambulizi hayo kuwa "kitendo cha kigaidi".

Mashambulizi hayo yamekuja huku wajumbe wa Urusi na Ukraine wakielekea Istanbul, Uturuki, kwa raundi ya pili ya mazungumzo ya amani siku ya Jumatatu.

==================================================

Ukraine says it has completed its biggest long-range attack of the war with Russia on Sunday, after using smuggled drones to launch a series of major strikes on at least 40 Russian warplanes at four military bases.

President Volodymyr Zelensky said 117 drones were used in the so-called "Spider's Web" operation by the SBU security service, striking "34% of [Russia's] strategic cruise missile carriers".

SBU sources told BBC News it took a year and a half to organise the strikes.

Russia confirmed Ukrainian attacks in five regions, calling them a "terrorist act".

The attacks come as Russian and Ukrainian negotiators head to Istanbul, Turkey, for a second round of peace talks on Monday.

Source: BBC News
 
Habari zilizopo kwa sasa na uthibitisho wa video ni kuwa Ukraine imefanikiwa haribu ndege vita zaidi ya 40 ndani ya Urusi.
Haijulikani wamefanikiwa vipi kwani umbali huo FPV drone haziwezi fika
Unaleta habari nusu nusu ina maana huna hakika
 
Habari zilizopo kwa sasa na uthibitisho wa video ni kuwa Ukraine imefanikiwa haribu ndege vita zaidi ya 40 ndani ya Urusi.

Haijulikani wamefanikiwa vipi kwani umbali huo FPV drone haziwezi fika

Siku ya jana pia wamefanikiwa lipua madaraja mawili ndani ya Urusi

SSB chini ya Budanov ni habari nyingine
 
There is no Air Defense System which is 100% foolproof, it's a fact the bellicose Russians will have to contend with.
 
There is no Air Defense System which is 100% foolproof, it's a fact the bellicose Russians will have to contend with.
Hapana hizo drones zimekua launched inside russia, so hizo Air Defence system hazikua na kazi na walijua hilo ndo maana wame launch kutokea kwenye malori karibu na hizo Bases.
Zingetokea Ukraine zisingefika zote.
 
Cha msingi wewe kaa karibu na TV au Smartphone yako, kitakacho ipata Ukraine hii week au ijayo Dunia itashangaa, jiandae kwa Retaliatory Strike moja ya balaa zito l.
 
Ikundo eno, taru hano
Nimetafuta uthibitisho wa Video kuona hizo bombers zikiwa in flames sijaona, ila ukweli ni kwamba hizo Airbase zimeshambuliwa ila uhakika wa ndege 40 sijapata bado, kuna exaggeration inaendelea hapa
 
Back
Top Bottom