Mkuu samahani sana kama nitasema haya ila naomba kusema kuwa wewe sio Judaism na haupo katika dhehebu lolote la judaism..
Kwanza hakuna Myahudi anayejitapa kujua uyahudi akataja jina la Mung_ kwa ukamilisho wake ila wewe umelitaja zaidi ya mara 10 wakati Talmud,Mishnah ,,Halakhah zinakataza kufanya hivyo na huesabiwa dhambi kufanya hivyo..
Tafakuri ya Torah ulizotaja hazifanyiki kila siku bali hufanyika Jumatatu ,Alhamisi na Shabatt mchana ( siku ya sabato Mchana)..na si kila siku hufanyika tafakuri siku nyingine hufanyika aliyot (maneno ya barka yaliyopo kwenye torah na husomwa kabla ya Borkhu prayer)
Twende kwenye Hagbah na Glilah ambayo wakristo ndo huita magombo na umegusia vitabu vya Yashayahu (Isaya) , Nehemya (Nehemia) DaniEl hujavijua vizuri kwa sababu huwezi kusoma biblia peke yake bila kusoma talmud na Halakh na pia ukapitia kidogo rabbinic narrative zozote utakuwa unajidanganya tu...
Hata kama nikikuambia uelezee ujumbe ulioletwa humo kwa ulivyoamdika naamini kabisa Utashindwa (Nisamehe kwa kusema hivyo
jinsi ya Ibada za kiyahudi zinavyofanywa ni 90% differ from Christian Prayer...
wewe umekataa challenge kwasababu naamini unachokisema ni 100% Uongo na kuhusi kuwajua Wayahudi ni kweli siwezi kufika hata 50% yakuwajua ,But atleast nimekaa nao and i was practising judaism atleast naweza nisiwajua wayahud nikajua Mila tamaduni na Misingi yao kwa 30%...
MWISHO MKUU hatushindani kwamba apatikane mshindj ila huwa nachukia kuona mtu anapindisha ukweli kwa manufaa yake binafsi i think unaweza kuwa umeniona hata sehemu nikisema au kuwatetea watu wa imani fulani ukahisi mimi ni mlengo wa sehemu ile..
kwa sasa mimi Sijafungamana na imani yoyote...Bali nipo katika matendo nayofahamu mwenyewe...