Jagwanana
Senior Member
- Jul 3, 2024
- 130
- 224
Ukristo uliingizwa na wazungu Afrika kwa mara ya kwanza katika karne ya 1 AD Misri na Tunisia na baadae kuenea kaskazini. Karne ya 4 AD Ethiopia iliufanya ukristo hata kuwa dini ya kitaifa chini ya mfalme Ezana kwenye himaya ya Aksumite.
Lakini umeenea zaidi Afrika Chini ya jangwa la Sahara ikiwemo Tanganyika kwenye karne ya 15 chini ya wamisionari waliokuwa wanakuja kututawala, kututumikisha na kutuibia mali zetu ikiwa ni njia nzuri ya kutubadilisha kisiasa, kifikra na kitamaduni( wakati wa ukuaji wa himaya ya kirumi), kuenezwa ktk njia zote zilizokuwa zinafanya biashara pamoja na za watumwa.
Machifu na viongozi wetu walikumbatia ukristo kwa sababu ya kujenga urafiki na wazungu au kwa nguvu lakini lengo la wazungu likiwa ni kutubadilisha tuwe na imani kama yao ili tutawaliwe kirahisi kifikra na kiuchumi, biblia wakiishikilia mkono mmoja lakini bunduki mkono mwingine ukifanya masihara nao aliyefanya masihara na hao watakatifu, basi jua kwako imeenda!
Ambacho hakikubadilika ktk ukristo wa leo ni kutawala na upigaji. Mchungaji yuko juu ya kila mtu na hata juu ya familia za watu. Wakiamua wachungaji baba mwenye familia jua kwako imeenda Utakalolisema kama ushauri kwa mkeo atakuchenjia ndani mpaka utakoma hata kama ukiuliza mbona hela zote za familia unapeleka kanisani. Zitapelekwa, mchungaji ataambiwa unakatalia hela na hakuna kuongea na wewe wiki nzima.
Mahubiri mengine ya kitapeli na yanajulikana kabisa huu ni utapeli lakini inahalalishwa na watu na serikali inakaa kimya kabisa watu wakiibiwa, na hata kuingilia maamuzi ya kiafya katika familia za watu kwa maombi yasiyokuwa na miguu wala mikono. Kwa utawala huu walionao leo wananunuliwa magari ya kifahari, wanalishwa mahotelini kifahari, watoto wao wanasomeshwa shule za maana na wengine wanajengewa nyumba za kifalme kutoka kwa waumini wao ambao wengi hata mlo mmoja kwa siku ni shida.
Ukristo kama ilivyokuwa nia ya wakoloni kuja kutupiga na kuzineemesha kiutajiri nchi za ulaya, leo wakati nchi hizo zimeshakuwa matajiri, wachungaji na viongozi wa kidini wamekuwa ni wapigaji wa wananchi tena bila huruma au aibu. Baadae tutakuja kuona wakitosheka kwa kula na kusaza wachungaji ndio watakuwa maraisi wa nchi zetu baada ya mafisadi kuchoka maana ndio wenye hela.
Kwa hiyo mtu asinidanganye kunisomea kifungu hiki cha neno ktk bibilia kinasema hili au lile. Nawajua.
Mnapambania kutukuza utamaduni wa watu weupe niwaamini ili mnitawale kiuchumi na kifikra.
Na mara nyingi hata serikali nyingi za Africa zunajua tunapigwa, ila wanazisaidia serikali nyingi "KUTUNZA AMANI, ILI MAFISADI NAO WAENDELEE KULA KWA AMANI" na sio kwa maslahi ya falimia yoyote. Kama unabisha nitafutie kanisa lolote lili kubwa kama utaona mzee wa kanisa ni muuza mchicha. Cheo chako kanisani kitategemea kitita cha hela kilichoko mfukoni mwako na ndiye utakayekuwa na sauti kanisani.
Wanaitwa mihimili ya kanisa. Wachina wanawapa watoto wao majina ya kichina, wahindi ya kihindi, wajapani ya kijapani lakini usipompa mtoto wako jina la kikoloni basi utaitwa mpagani, neno ambalo nia yake ni kudhalilisha imani za wazazi wetu ili upuuzi wao uendelee kushika mizizi wa kutuibia fikra na mali zetu. Walitutenganisha na wazazi kuwapeleka utumwani bila kujali familia zao zitaishije huko nyuma na leo wachungaji wengine ndio vinara wa kuvuruga familia za watu. Yaleyale. Mvimbishie kichwa mchungaji uone! Kudadeki. Atakuhibiri mpaka masiko yako yang'oke kichwani. Kisa umtii tu. Simtii yoyote!
Kwa leo Ukristo ni kitu kinachosikitisha kukiona!