Mimi ninachoweza kusema Ni kwamba hizi dini mbili zimebeba utamaduni na asili wa maeneo zilikotoka.Waliotuletea wamefanikiwa kutubrainwash 100% hasa mwafrika.
1.Kiasili nchi za arabuni Kuna jangwa,so miti ni tatizo,katika Hali ya kawaida tangu zinaanza hizi dini isingewezekana kukaa kwenye viti vinavyotokana na miti.How come mtu wa Iringa kwenye miti ya kutosha nae anaingia nyumba ya ibada anakaa chini kisa muislamu,au anakula kwenye mkeka badala ya kukaa kwenye mess ya kisasa kisa dini?.. Inafikirisha.
2.Mtu anapozikwa kwa mujibu wa hizi dini mbili wanamwaga maji juu ya kaburi(huita maji ya baraka).Kiasili Kama nilivyosema zilikotoka hizi dini mbili Kuna jangwa,mtu akizikwa usipomwaga maji na kuweka jiwe(Shahid) kaburi litafutika na upepo mkali..sisi kwetu kwenye udongo wa kichuguu,kuchikba kaburi Hadi mnatumia
Tindo kumwaga maji Ni usanii tu.Hakuna sababu ya msingi Mmebeba kila kitu.
3.Kwa sababu ya Hali ya hewa ya mashariki ya Kati kuwa jangwa,maana yake Kuna joto Kali sn,wenzetu walikuwa wana tabia ya kuvaa nguo nyepesi mchana(mnaita kanzu) na kushinda kwenye nyumba zenye hewa (mfano masjid).Sisi tulipoletewa dini tumelibeba hilo,tunashinda kwenye nyumba za ibada kuanzia asubhui Hadi jioni kwa ksingizio Cha thawabu..Tukatafute hela tuache uvivu,kwetu hakuna joto..Zanzibar kanzu ndy nguo za kushindia,hata watoto wanacheza huku wakiwa wamevaa kanzu,kiss sisi ni washika dini!!
Kwa wakristo ndiyo balaa,uzungu Kama wote!!
1.Mtu mweusi na utamaduni wa faza krismasi wapi na wapi?
2.Mizimu yao wakaita saints(watakatifu)
Mtakatifu Martin de Porres,mtakatifu Aqcuilina,mtakatifu John.Sisi mizimu yetu ambayo ilikuwa tukiomba inatuletea neema Kama mvua na na chakula shambani wakatukataza kutambua maana tunamkufuru Mungu...Ujinga!!
3.Mavazi yet yenye kutambulisha tamaduni zetu Kama kaniki,shanga na ndonya wakatuambia tusiingie nayo kanisani vina maagano na mapepo...wametuletea suti zao!!
4.Ukienda kumbatiza mtoto ukamwita jina la kikwenu Kama awowo apewe unaambiwa Hilo siyo jina la kumpa mtoto,wanakuchagulia kwenye list ya watakatifu wao.."mwanao ataitwa Samuel" wakati wao tunasoma majina yao ktk history mtu alijiita Livingstone
Tumeenda mbali siku hizi ukiomba jina mzuri la mtoto wako wanakuchagulia majina ya ulaya na arabuni(Asia)..Mwanao mwite Fahima..mwanao muite Shadya..Mwanao muite Jackson !!
Africa siku tutakapoanza kuurudia utamaduni wetu ndiyo siku tutakapoanza kufanikiwa katka kila kitu..