Ukristo ni Uzungu na Uislamu ni Uarabu?

Ukristo ni Uzungu na Uislamu ni Uarabu?

Najaribu kuwaza ni kwa nini watu wengi wanaonesha kuwa ili uwe muislam mzuri ni lazima utumie mambo mengi ya kiarabu kuanzia kuvaa mpaka kuongea kwa lafidhi ya Kiswahili cha kiarabu.

Lakini pia wakristo wengi nao ili ionekane wewe ni mteule wa mungu uzungu ni lazima uwe ni sehemu ya maisha yako. Siku hizi kila anayejiita "Nabii" au "Mtume" ni lazima pia ajitahidi kuhubiri kwa kiingereza au aweke mtafisiri wa Kiswahili kwenda kiingereza.

Hivi huwezi kuwa Mkristo safi bila ya kuitwa Silvanus, Tarchistus, Moses, Jenipher, Peter au Magdalena? Na majina ya Mohamed, Hussein, Jumah, Hidaya, ndiyo alama ya Uislamu. Hivi mtu akiitwa CHANDIMU hawezi kuwa muislamu au mkristo?

Hivi Uislamu ni Uarabu na Ukristo ni Uzungu??
Huwa tunatafuta kuwakoga wakinzani wetu wa dini ili watuonee gere.Vilevile kujinasibisha huko,huwafanya "mahasidi" wetu kutuona/kufikiri na kuwateka akili kwamba tupo kamili gado kiimani yetu kuliko yao.
 
Huu ni ukweli ambao haupingiki

ili uwe mkristo

-Vaa Suti& viatu vyeusi
-Lugha yako nzuri ni kingereza kwenye utafsiri wa maandiko
-Oa mke mmoja
-Hakuna Talaka
-Uko Sawa na mke wako kwenye maswala ya Haki
-jiite majina ya kizungu kama John,mark etc

ili uwe Mwislamu

-Vaa Hijab & Kanzu
-Jiite majina ya Kiarabu
-Lugha yako Bora ni kiarabu
-lugha ya Kitabu chako ni Kiarabu
-ibada ya hija ni ibada ya kipagani ilikwepo kabla hata kabla ya uislamu
 
Tunaweza tukaziAfricanize Didi zetu pendwa, kuliko kuwa Wabaguzi kwa waluotuletea Ustaarabu.

Tusipende kushutumu kila kitu.
 
Hizi dini ni tamaduni zao wala sio Mungu kama wanavyodai..mana waafrika hata imani tulikua nazo.

Chamsingi hizi dini tuziweke katika tamaduni zetu ili ziendane na sisi kama wazungu walivyo ufanya uyahudi kuwa ukristo kupitia tamaduni zao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tunaweza tukaziAfricanize Didi zetu pendwa, kuliko kuwa Wabaguzi kwa waluotuletea Ustaarabu.

Tusipende kushutumu kila kitu.
kuafrikanisha dini hizi ni jambo lisilowezekana. Dini huja na tamaduni zake.
 
kuafrikanisha dini hizi ni jambo lisilowezekana. Dini huja na tamaduni zake.
Linawezekana, hizi Dini ni za Kisemitic, Uislamu huko India/Pakistani wameweza kuufanya wa kienyeji na kuzaa Ahmadiya Ismailiyaa na Singasinga.

Ukristo Waulaya wameweza kuufanya wa kienyeji hadi kuweka Image yao ya masaya kuwa awe na Blue eyes na Blond na mambo mengine mengi.

Sasa sisi na low iq zetu tunajifanya hatujiwezi kwa lolote mpaka turudi kwenye upagani na uchawi wa kutoa kafara za watoto kwa mizimu.
 
Linawezekana, hizi Dini ni za Kisemitic, Uislamu huko India/Pakistani wameweza kuufanya wa kienyeji na kuzaa Ahmadiya Ismailiyaa na Singasinga.

Ukristo Waulaya wameweza kuufanya wa kienyeji hadi kuweka Image yao ya masaya kuwa awe na Blue eyes na Blond na mambo mengi.

Sasa sisi na low iq zetu tunajifanya hatujiwezi lolote mpaka turudi kwenye upagani na uchawi wa kutoa kafara za watoto kwa mizimu.
Kwa kuwa tuna Low IQ ndiyo haitawezekana. Tamaduni zetu kwa vizazi vingi zimekubali kuchukua tamaduni za wengine na siyo kuzifanya zikubaliane na za kwetu. kwa ivo haiwezekani.
 
Watu wakishakuwa walevi wa dini huwa hawaambiliki.
 
Kuna utofauti kati ya uislamu na ukristo kuhusu tamaduni,ukristo haujamezwa sana na uzungu kama uislamu ulivyo kwa uarabu na ndio maana suala la mavazi au lugha havina ulazima kama utambulisho wa kidini.Sehemu zenye wakristo wengi mila za kiafrika zinaenziwa kiasi fulani kuliko upande wa pili.haiingii akilini kwa mnyakyusa anayeitwa Lugano eti aitwe Loveness baada ya kubatizwa!huko pwani hakuna neno upendo kwa kizaramo?!

Sent from my BBF100-6 using JamiiForums mobile app
 
Mzee wa bandari wewe si mkristo pia? Na wewe Ni mtumwa?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
MI ni mkristo ambaye najifunza mambo zamani nilikuwa Mtumwa WA kifikra but now sio hivyo but asilimia kubwa ya watz ni watumwa WA kifikra mpk Sasa.... Hawataki majina Yao wanataka kila kitu cha Slave master
 
Mkuu

Wenye akili Sana walitugawa vizuri KIROHO ili watutawale vizuri!!

1.yaani, ishmael-uarabu-upalestina=uislamu

2.Isaka-yakobo-israel-uzungu=ukristo

Sasa basi kiimani tumegawanyika katika makundi mawili aidha mzungu au mwarabu!Lengo kuua tunyukane!


Na kweli tunanyukana KIROHO na kimwili Hadi leo!!

Epukeni mtego wa kunyukana sisi sote ni ndugu!!
 
Back
Top Bottom