Ukristo unaruhusu ndoa ya mke wapili kwa mujibu wa andiko hili

Mimi siongei kwa kutumia maneno ya vijiweni mkuu, najiridhisha kwanza kwa kusoma official sources. Pia sio kila kilichoandikwa kwenye biblia ni chakuchuka na kukifanya katika maisha ya kawaida. Kwenye biblia kumeandikwa pia uovu wa watu mbalimbali nimuhimu kulijua hilo. Nakushauri fuatili Takwimu za idadi ya watu duniani kabla ya kuanza kuropoka (world population by sex) kuhusu matatizo ya kijinsia yana affect jinsI zote me na ke. And by the way shoga hawezi kujitambulisha kama mwanaume bali Transsex
 
Kuna ushahid wa kimaandiko wa hili?
1 Wakorintho 7:2-3

[2]Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
 
lete andiko la yesu hilo?
 
Hoja ya wake wawili, utaona inalenga kutimiza tamaa ya mwanaume kingono; hiyo hoja tuiangalie kiuchumi na katika ustawi wa jamii, hebu tuone faida ya kuwa na wake wawili kiuchumi na kijamii ukiachana na hili mwanaume na upwiru wake.

Maana ukibase kwenye tamaa ya mwanaume utaona hata hao wawili kwa mwanaume hawatoshi maana mwanaume anapenda kujaribu Radha mpya, apate mwenye makalio makubwa, apate mweusi, mweupe, ajaribu kwa English figure, atasimuliwa kuhusu mishangazi ilivyo mitamu atataka akathibitishe ataambiwa isiombe kukutana na mwanamke wa kimakonde hautataka kumuacha mwanaume atatafuta mwanamke wa kimakonde na kujaribu aone kama aliyoambiwa ni kweli, kwahiyo kama hao wanawake watakuwa ni kutibu tamaa ya mwanaume hao wawili au hata wanne hawatoshi kabisa
 
Nasubiri Unionyeshe Yesu alipoagiza Ndoa ya Mke mmoja
 
Mkristo akisema anatumia agano jipya bila agano la kale huyo simuelewi, biblia ni combination ya maagano mawili, Yesu mwenyewe alikuja kuitimiliza torati na sio kuitengua.
 
Kuna mahali Mungu mwenyewe Alitoa amri ya Kuongeza Wake..
Kwa manabii zake kwenye Biblia..

Mungu mwenywe na Yeye alijipinga na Akavunja Amri??
Ni lini Hasa Mungu alitangaza Ndoa ya Mke Mmoja??

Ndoa ya Wake wawili ilianza kwa Lameck na sio Vizazi vingi..
Lameck alikuwa Ni Mjukuu wa Adam
 
Kama Suleiman aliye oa wake 700 na Masuria 300 mwishoe ali kiri ni ubatili mtupu, kuwa na wanawake wengi nisawa na kujilisha upepo.

Wana wake wengi ni tamaa ya mwili wa mwanadamu na ukiendeshwa na tamaa za kimwili dunia itakuletea shida nyingi.
 
Habari Thecoder
Je Unafahamu Kuwa Andiko Hilo Hakulisema Yesu ila Yesu alinukuu Andiko Lililotoka Kwenye Torati??

Mwanzo 2:24..

"Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."

Sasa Basi kama Sheria Hiyo aliweka Mungu Baada ya Kuumba ilikuwaje Yeye mwenyewe Mungu aamuru baadhi ya Watumishi wake waoe wake zaidi ya Mmoja na Wengine aliwaambia yeye mwenywe
 
 
Kwani ukristo uliànza lini? Kabla ya kuzaliwa, kufa, kufufuka na kupaa mbinguni kwa Yesu kristo kulikuwa kuna wafuasi wa Yesu kristo, yaani wakristo?
Hiyo agano la kale ni kabla ya ukristo ila kama wewe ni mfuasi wa dini ya kiyahudi hayo maandishi yanakuhusu kuoa zaidi ya mke mmoja.
 

Sijajua picha hii na bandiko langu vinahusiana vipi?

Lakini hapo hapo nikuulize swali unajua maana ya culture?

Mimi mmasai, nikivaa shanga imetengenezwa jamaica, ama shuka la kimasai limetengenezwa china nitakuwa nimeua culture ama?

Tujadili ndoa ya mke wa pili kwenye ukristo.
Sipo huko kwenye malumbano ya kidini.
 
Nipe wew takwimu mkuu, kuwa wanaume ni wengi kuliko wanawake.
Nipe ratio ya wanaume kwa wanawake nchi kama russia hivi.
 
Sawa mkuu, tengeneza uzi wake, weka picha unaweza kupata mteja, biashara njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…