Swali lako siwezi kulijibu mimi, ila yesu alisema hajaja kuipinga tourati.
Exactly, tourati Ina nguvu katika Sheria na kanuni, hivo hata asiyeamini unaweza fikiri anaamini, ila injili Ina nguvu rohoni, hata usiyefikiri ana imani unaweza Kuta ndio anaamini,kwa ufupi tourati haikuwa na kasoro,ila ilitekelezwa kwa usanii mwingi,
Kutatua Hilo tatizo bwana wa sabato anashuka mzimamzima na kuwajaza watu roho MTAKATIFU ili waamini Kisha wafuate,na siyo wafuate bila hata ya kuamini, ukristo unaanzia ktk falsafa hii,
Utaona Yesu anasisitiza mambo mengo ambayo ktk tourati ni kinyume, mfano kujiukumu Kila unapotaka kuhukumu, ktk tourati kama ulitenda Dhambi na haukukamatwa usingehukumiwa, rejea kisa Cha mwanamke aliyefumaniwa,
UPENDO, huu utafakari , ukihisisha na visa vya na hukumu za tourati, yesu anasisitiza misamaha mingi, a thing kwenye tourati ni jino kwa jino,
Lakini kubwa zaidi yesu anadhihirisha kwamba asili ya Mungu ni msamaha na UPENDO, ndio maana hata baada ya Dhambi ya adamu na Eva Bado hakuutenga ulimwengu, alituma mitume na manabii, aliithaminisha damu iliyolaaniwa kwa sadaka ya wanyama, kama ng'ombe, mbuzi na njiwa. Tunavozaliwa tu alisisitiza tukombolewe,
Baada ya miaka mingi alitoa sadaka ya damu ya jumla kwa kumruhusu mwanae mpendwa achinjwe, ile damu ilimwagika, na wengi tuliwekwa huru kupita damu hiyo
Jina Yesu litukuzwe,