Ukristo unaruhusu ndoa ya mke wapili kwa mujibu wa andiko hili

Ahsante mkuu
 
Salama dokta, bila shaka uko vizuri kutoka upande huo wa dunia.

Ni kweli, Yesu alinukuu hilo andiko kutoka mwanzo ili kuijenga hoja yake vizuri huku akiwakumbusha kwamba anachokifanya yeye si kitu kipya ila ni vitu ambavyo vilikuwepo isipokua vilivurugwa kimpangilio kiasi cha kufanya watu washindwe kuelewa ni upi msimamo halisi wa kiimani, je, waoe wake wengi kama ambavyo babu zao walifanya au waoe mke mmoja, na yeye akaliweka sawa.

Kwakuanza kuwakumbusha asili ambavyo ilikua hapo mwanzo na kwa namna hiyo hiyo basi watu hao mke na mume wakiungana wawili wanakua mwili mmoja.

Kuna pahala nilijaribu kuelezea jana ya kwamba biblia ni kama katiba ya kiimani na katiba hii haibadilishwi kwa namna ya kibinadamu bali kwa namna ya kiMungu pekee(kwahiyo Yesu asingekuja mambo yote haya yangebaki kuwachanganya watu kwa kutokujua msimamo halisi wa kiimani ni upi).

Kwahiyo awali agano la kale (hasa torati) ilifuatwa na watu waliishi kwa muda kidogo na kufanywa kuwa kama katiba ya kiimani kwa nyakati zile ila baadae kutokana na nyakati kubadilika ilionekana mambo mengi yalikua na upungufu kiasi cha kuwafanya watu waanze kufanya mambo kitofauti na hii nayo ilikua sababu moja wapo ya Yesu kuja ili katiba ifanyiwe marekebisho(ndio maana utaona licha ya miujiza mingi ambayo aliifanya ila pia alitumia muda mwingi kubadili baadhi ya misimamo ambayo iliwekwa kwa namna ya torati na kuwaelekeza namna sahihi ya kuifuata).

Na katika maeneo kadhaa ambayo Mungu alitoa mapendekezo kwa mtu mmoja mmoja ya kuongeza mke yalitokana na sababu za hapa na pale na katika maeneo yote hayo hayakusema moja kwa moja ya kwamba hii itakua ndio Sheria ya ndoa kwa watu wote ulimwenguni, na hii ndio ilichangia pia kuleta moanganyiko kidogo kiasi cha kufanya watu washindwe kujua msimamo halisi ni upi hadi pale Yesu alipowakumbusha na kuwaambia wapi wasimamie.
 
Ukristo is too general.
Katoliki ni kristo lakini wanamwamini Bikira Mara kama muombezi wao wafike Mbinguni.
WAlokole ni wakristo na wanamwamini Yesu na Roho mtakatifu kama muombezi wao kwa kuugua kusikoweza kusemeka.
Sasa , kuwa specific, walokole ni mume na mke mmoja, hakuna exception.
 
Mbona agano la kale wengi tu kati ya wachamungu walioa wake wengi ....tatizo kuna tofauti kati ya agano la kale na injili ....injili inatambua na kulidhia wake wengi ila hai shauri kuoa wake wengi ndani ya ukristo(injili) yaani kwa wale walio batizwa mke ni mmoja tu ila kama ulikuwa na wake wengi basi inawatambua hao wake kuwa ni wake zako halali
 
Ni wapi MUNGU MWENYEZI aliruhusu nipe andiko nione

Hao akina lameck wote walivunja agano la MUNGU MWENYEZI wengine wakaenda mbali zaid hao wajukuu wa Adam wakawa wanauwana wao kwa wao

Je na kuawana MUNGU aliwaruhusu?

Si kila kitu ambacho biblia imeandika basi kimeruhusiwa no bali kimeandikwa ili wewe ujifunze mtumish mwenzagu
 
Agano la kale mungu alikuwa hana tatizo na kuoa wake wengi ...tena yeye mwenyewe kathibitisha na kuwajalia watumishi wake furaha ya wake wengi ...kasome mfalme daudi pale alipo fanya uzinzi na mke wa uria na kufanya fitina ya kifo cha mume wa huyo mke hili kuficha aibu ....baada ya ilo tukio mungu alimtuma nabii kwa daudi kasome mungu alisema nini kumwambia daudi kuhusu daudi na wake zake wengi ..... kuna maneno mungu ana mwambia daudi nimekupa wake wengi na kama ungetaka zaidi ninge kuongezea wake, hapo daudi alikuwa na zaidi ya 7 tayari ....sasa hapo tunaona Mungu mwenye anamwambia daudi kuwa angeweza kumwongezea wake. DR Mambo Jambo Beira Boy
 
Kwani kuongeza mke unahitaji support ya verses za bibilia? We zingatia Sheria za KAIZARI anaye kutawala duniani
 

Tumepokea kwa Utekelezaji.....eko kabisa
 
Kwani kuongeza mke unahitaji support ya verses za bibilia? We zingatia Sheria za KAIZARI anaye kutawala duniani
Kila mmoja na njia zake, hivyo wenye imani ya kidini wanahitaji vifungu ili wafanye baadhi ya mambo.
 
Swali lako siwezi kulijibu mimi, ila yesu alisema hajaja kuipinga tourati.
Exactly, tourati Ina nguvu katika Sheria na kanuni, hivo hata asiyeamini unaweza fikiri anaamini, ila injili Ina nguvu rohoni, hata usiyefikiri ana imani unaweza Kuta ndio anaamini,kwa ufupi tourati haikuwa na kasoro,ila ilitekelezwa kwa usanii mwingi,

Kutatua Hilo tatizo bwana wa sabato anashuka mzimamzima na kuwajaza watu roho MTAKATIFU ili waamini Kisha wafuate,na siyo wafuate bila hata ya kuamini, ukristo unaanzia ktk falsafa hii,

Utaona Yesu anasisitiza mambo mengo ambayo ktk tourati ni kinyume, mfano kujiukumu Kila unapotaka kuhukumu, ktk tourati kama ulitenda Dhambi na haukukamatwa usingehukumiwa, rejea kisa Cha mwanamke aliyefumaniwa,


UPENDO, huu utafakari , ukihisisha na visa vya na hukumu za tourati, yesu anasisitiza misamaha mingi, a thing kwenye tourati ni jino kwa jino,

Lakini kubwa zaidi yesu anadhihirisha kwamba asili ya Mungu ni msamaha na UPENDO, ndio maana hata baada ya Dhambi ya adamu na Eva Bado hakuutenga ulimwengu, alituma mitume na manabii, aliithaminisha damu iliyolaaniwa kwa sadaka ya wanyama, kama ng'ombe, mbuzi na njiwa. Tunavozaliwa tu alisisitiza tukombolewe,

Baada ya miaka mingi alitoa sadaka ya damu ya jumla kwa kumruhusu mwanae mpendwa achinjwe, ile damu ilimwagika, na wengi tuliwekwa huru kupita damu hiyo


Jina Yesu litukuzwe,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…