Ukuaji wa lugha ya Kiswahili: Neno Mbashara

Maana ya neno Mubashara ni "Live" kwa kizungu. Yaani moja kwa moja au ana kwa ana au dhahiri
 
Hapo imetumika sanaa katika kuonyesha weledi wa lugha.......
Kwa mtazamo wängu hiyo ni lugha ya picha imetumika.
Ni sawa tu na mtu akikuambia "Ardhi hii bado bikra" au wazungu wakati mwingine hua wanamsemo wao "A handsome garden"

Ni lugha tu za picha hizo
 
Lugha yoyote inakua na ASILI ya maneno katika lugha nyingine,, ukisoma NADHARIA YA LUGHA Njia moja wapo ya Uundaji wa maneno ni Kutohoa kutoka lugha ya kigeni,, BAKITA kutohoa maneno katika lugha nyingine SI KOSA
 
Kiswahili ni maneno machache sana ni ya kibantu, sijui kwanini tumepumbazika hivyo.
Halafu tunaamini mtu wa kwanza alitokea Africa, sasa tulishindwaje kuwa na maneno yetu ya kutunga wenyewe?

Mzungu katengeneza Rail tukaita RELI, Signal= zinginari,
Akaja mwarabu na maneno mengi tukaiga kuanzia aliko ingilia BAHAR= bahari

Kuna maneno waarabu na wazungu wameiga toka kwetu lakini sio vingi kama sisi.

MUBASHAR ni neno la kiarabu kwani miaka yote hii tumeshindwa kupata neno jipya?
 
hoja yako hasa ni nini??
 
Kuna hili lingine linaitwa 'BASHA MUHANDIS' likiwa na maana ya Chief Engineer nalo lina mzizi kutoka lugha ya kiarabu, lakini hapa kwetu naona haliwezi kuwa na mshiko kwani lina ukakasi kidogo.
 
Sisi ambao huwa huwa tunagusa gusa lugha lugha kiarabu na lugha za wanafunzi wac dini katika maeneo yao,tamko "Mubashara" ni maarufu sana na tunalifahamu tangu zamani.Kwa ufupi asili ya tamko "Mubashara" ni kiarabu na hutamkwa "al-Mubashar" kwa maana moja kwa moja yaani urushwaji wa matangazo au tukio la sauti au kuonekana kupitia kifaa husika.Kwa maana nyingine tamko hili limetoholewa kama lilivyo kimaana na utamkwaji wake kutoka katika lugha ya kiarabu.
 
ITV itabaki kuwa super brand tu.Hivi mnajua neno mubashara limehasisiwa na ITV?
Cha kushangaza clouds wamelidandia na vijana wanajua wao ndio waasisi.Sisemi ni neno jipya"No"Najua lipo kwenye kamusi.Ila walioliubua.Ni ITV tanzania.Sio Clouds group."Tuwe wabunifu"Sifa ziwarudie ITV na Sio Clouds.
 
Hii nayo ni habari ya siasa?
 
Mkuu umeongea ukweli kabisa, neno hilo limevumbuliwa na itv, mahojiano mubashara, bt wazee wa kukopi na kupest wamelishadadia mpk wameharibu maana ya hilo neno.
 
Acha kupotosha watu

hili neno chanzo ni mechi ya mpira wa Yanga na Al Ahly....
mechi ilioneshwa na Azam tv

TV ya misri ndo ilikuwa na hilo neno Mubashara...

ndo watanzania hasa journalist wakalibeba...
 

Siwapendi ITV na Radio One kwa sababu zangu tu za Kisiasa na Kimichezo ( ambazo haziwahusu sana ) ila katika hili la nani ni Muasisi wa neno la ' Mubashara ' sitaki niwe Mnafiki na nichume dhambi bure kwa ' Maulana ' jibu ni Radio One Stereo na ITV hivyo kama Watu wa Clouds fm na tv wanasema ni wao nadhani wanatakiwa ' kutubu ' kwa Mungu kwa kutenda dhambi kubwa sana ya Uwongo kwa Watanzania.
 
Clouds always hudandia jambo na kuliboresha hata kipindi cha Friday Night Live toka EATV wamekicopy japo now kimechukua mkondo wa udaku, kipindi vya mziki wanacopy MTV hawana ubunifu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…