Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Kulingana na ripoti ya BoT ya robo ya mwisho ya 2024, mzunguko wa fedha Tanzania unaonyesha ukuaji wa kushangaza, lakini pia unaonesha mapungufu ya kiuchumi yanayohitaji uchunguzi wa kina. Pesa taslimu iliyo nje ya mifumo ya benki imepanda kutoka trilioni 4.5 mwaka 2020 hadi trilioni 7.3 mwaka 2024, ongezeko la 62.2%, huku amana za wateja benki zikiongezeka kutoka trilioni 23 hadi trilioni 40, sawa na 73.9%. Hali hii inaweza kuonekana kama ishara ya ukuaji wa kiuchumi na kufanikiwa kwa sera jumuishi za kifedha, lakini ukiitazama vizuri, inaweza kumaanisha kuna pengo kubwa na hatari kwa uchumi.
Kwanza, suala la utitili wa noti za Shilingi 10,000, ambazo zinachukua 85.8% ya pesa zote taslimu, ni la kushtua na linaibua maswali mengi juu ya afya ya uchumi wetu. Ongezeko hili linaweza kuwa dalili ya mfumuko wa bei (inflation), licha ya kuwa takwimu zinaonesha kuwa mfumuko wa bei bado ni 3.1 kufikia Januari 2025. Mfumuko wa bei unaweza kuwa ndio sababu noti zenye thamani ya chini kama Shilingi 5,000 zipungue katika mzunguko kwa 15.7% tangu 2020. Hiki ni kiashiria kwamba gharama za maisha zinaongezeka kwa kasi, na serikali na Benki Kuu zinashindwa kuleta uwiano wa bei thabiti.
Niwazi kuwa suala la utegemezi wa pesa taslimu zilizopo nje ya mifumo ya kibenki unapunguza uwezo wa Benki Kuu kudhibiti fedha katika uchumi, jambo linaloweza kuleta mabadiliko tusioyatarajia kama hali hii haitatafutiwa ufumbuzi mapema.
Pili, sehemu ndogo ya sarafu (2% tu ya mzunguko) na ongezeko lake la 20% hadi bilioni 163 inaonyesha upungufu wa mkakati katika kusambaza fedha katika mzunguko au kutohitajika kwa aina hiyo ya fedha kwa sababu watu wanauona ni mzigo kuzibeba, hasa kama kuna mfumuko wa bei ambao bado hauko wazi. Ingawa sarafu za Shilingi 500 zinachukua 36.8% ya sarafu zote, ni 0.7% tu ya fedha taslimu zote, hali inayodokeza kuwa miamala ya kila siku inategemea noti za thamani kubwa zaidi kuliko kawaida. Hii hali ya kushangaza kwamba miundombinu ya kidijitali bado haijafika kwa watumiaji vyakutosha kuondoa utegemezi wa pesa taslimu, jambo linaloweza kuwa ni ukosefu wa sera jumuishi au mipango hafifu ya serikali katika hilo ikiwemo gharama za kutumia huduma hizo.
Ongezeko la 238% la noti kwenye mzunguko (kutoka bilioni 199 hadi 674) ni ishara inayopaswa kutiliwa shaka. Hili linaweza kuashiria kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi zisizo rasmi au hata shughuli haramu ambazo hazitaki kuhusisha mifumo rasmi. Aidha, kuongezeka kwa amana za benki kinzana na hilo kwani kuonaonesha pengine ni matokeo ya kuimalika kwa uchumi. Hata hivyo, ipo haja ya kuwa na sera na mikakati ya kudumu ya kuimarisha miamala ya kidijitali na kupunguza utegemezi wa pesa taslimu katika uchumi ili kupunguza madhara yanayoweza kutoka na kuongezeka kwa matumizi ya fedha katika hali hiyo, pia kuzuia uwezekano wa kutokea hatari ya mfumuko wa bei usiodhibitika.
Ongezeko katika mzunguko wa fedha ni linavutia, lakini linatiashaka kama linaamaanisha ukuaji wake matokeo ya mfumuko wa bei. Ipohaja ya kuchukua hatua za haraka kuboresha miundombinu ya kifedha na kuzuia utegemezi wa pesa taslimu ili kuepuka hatari za kiuchumi zinazoweza kujitokeza.