Ukuta Shule ya Sekondari Ngasaro, Shirati Rorya waanguka. Wanafunzi wawili wafariki

Ukuta Shule ya Sekondari Ngasaro, Shirati Rorya waanguka. Wanafunzi wawili wafariki

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Wana JF,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa wanafunzi wawili wa shule ya sekondari Ngasaro Wilaya ya Rorya(kata ya mkoma) wafariki dunia mchana huu baada ya kuangukiwa na ukuta.

Kwa taarifa nilizozipata ni kuwa ukuta huo ulikuwa unatenganisha vyoo na madarasa.

Chanzo: Mmoja wa familia ya wafiwa aliyepo Shirati Rorya.

Bado nawasiliana nae kwa taarifa za kina zaidi.

Update:
Kwa taarifa zilizopo shule ni mpya inamiaka miwili.
Kwamba imefunguliwa mwaka jana na mwaka huu ndio kwanza inakidato cha pili.
Cc Luoman kwa update zaidi.

Update2:
Ambulance iliyoenda kuchukua miili ya marehemu yapinduka na kusababisha majeraha kwa kwa dereva na baadhi ya askari waliokuwamo.
 
...kwa taarifa zilizopo shule ni mpya inamiaka miwili.
Kwamba imefunguliwa mwaka jana na mwaka huu ndio kwanza inakidato cha pili.
 
Sheria ya uzembe ichukue mkondo wake kuna watu wa kuwajibika hapo.
Na hii ndio maana yake, haiwezekani watu wawe wanafanya mambo ya kizembe yanayopelekea kugharimu maisha ya watoto wasio na hatia, na ukute kafara pia zinahusika. Wapumzike kwa amani watoto wasio na hatia!
 
Back
Top Bottom