Ukweli kuhusu Israel, Waarabu, na Ibrahim

Ukweli kuhusu Israel, Waarabu, na Ibrahim

Uarabu kwa ismail unatokana na yeye kwenda kukaa huko kwenye Penisula ya uarabuni na akaoa huko uarabuni na kupitia ismail koo nyingi na kabila nyingi zilitengenezwa na kwa sababu Mungu aliweka agano na Abraham kuwa atakuwa Baba wa mataifa mengi basi Waarabu wao wakaona Taifa lao limetokana na ismail, wakamwita Baba wa waarabu
Kwahiyo hata ismail angekua mchina kwakuwa alienda huko uarabuni zingetengenezwa koo za kiarabu na sio za kichina
 
Ibrahimu ni baba wa imani. Wakiwemo Waarabu na uzao wa Jacob(Israel).

Hivi Esau yule kaka yake Jacob uzao wake ndo upi kwa dunia ya leo?
 
Ibrahimu ni baba wa imani. Wakiwemo Waarabu na uzao wa Jacob(Israel).

Hivi Esau yule kaka yake Jacob uzao wake ndo upi kwa dunia ya leo?
Uzao wa Esau wanahusishwa kimapokeo na Waedomu. Waedomu waliaminika kuwa Wasemiti waliokuwa wakiishi eneo la Edomu, lililo katika sehemu ya kusini ya Yordani ya kisasa. Katika simulizi ya Biblia, Esau anachukuliwa kuwa baba wa Waedomu, na uzao wake mara nyingi huitwa Waedomu.
 
Sawa sielewi nieleweshe,una maana gani kusema israel ilianza kwa yakub na baba yake asiwe ukoo huo?? Kinasaba unaweza kuwa kabila au ukoo ambao baba yako sio ?? Ina maana huyo mtu alikana nasaba damu na ukoo wa baba yake na babu yake anaanzisha kabila lake na ukoo wake ambao hauna uhusiano na baba yake na babu yake? Wewe hapo unaweza sasahivi ukaamua ukawa sio kabila wala ukoo wa baba yako ma babu yako?na huyo ismail huo ukoo wa waarabu alianza kwa nani?
Yakobo si alizaliwa akiwa yakobo,,baadae akapewa jina la ukubwani,akaitwa israel,,,🤗haina maana kuwa DNA nazo zilichange kuendana na jina,,
We baki na ukweli kuwa Rebeca alikua ni binti wa ki syria,,,,Abraham nao anaeza kuwa alizaliwa Ur,,lakini baba yake ni mzaliwa wa Paran,syria,,
Sara mke wa Abraham nae ni syria kwasababu sara alikuwa ni mtoto wa babake na Abraham,,yaani Abraham alioa dadake,,hivyo wote hawa asili yao ni syria,,
Hata isaack alipotoka kuoa ilikuwa marufuku kuoa binti wa caanan,,alirudi kwao syria kuoa,,,vilevile hata jacob alirudi kutafuta mke syria,,,
Kwahiyo waisrael ni uzao uluofuata wa jacob,,hao sasa ndo wana wa israel,,,yaani wana wa jacobo,,🤷.
Abraham,sara,isaack huwezi kuwaita waisrael maana hawa qualify
 
Uzao wa Esau wanahusishwa kimapokeo na Waedomu. Waedomu waliaminika kuwa Wasemiti waliokuwa wakiishi eneo la Edomu, lililo katika sehemu ya kusini ya Yordani ya kisasa. Katika simulizi ya Biblia, Esau anachukuliwa kuwa baba wa Waedomu, na uzao wake mara nyingi huitwa Waedomu.
Mkuu hunijibu
 
Inaonekana hujui maana ya Israeli. Ibrahim yupo Israeli ilikuwa si yenye kutajika maana yake haikuwepo.
Israeli kwa kutumia Koran ni jina la mtu au la nini ? Lilitokana na nini au na nani?
 
Yakobo si alizaliwa akiwa yakobo,,baadae akapewa jina la ukubwani,akaitwa israel,,,🤗haina maana kuwa DNA nazo zilichange kuendana na jina,,
We baki na ukweli kuwa Rebeca alikua ni binti wa ki syria,,,,Abraham nao anaeza kuwa alizaliwa Ur,,lakini baba yake ni mzaliwa wa Paran,syria,,
Sara mke wa Abraham nae ni syria kwasababu sara alikuwa ni mtoto wa babake na Abraham,,yaani Abraham alioa dadake,,hivyo wote hawa asili yao ni syria,,
Hata isaack alipotoka kuoa ilikuwa marufuku kuoa binti wa caanan,,alirudi kwao syria kuoa,,,vilevile hata jacob alirudi kutafuta mke syria,,,
Kwahiyo waisrael ni uzao uluofuata wa jacob,,hao sasa ndo wana wa israel,,,yaani wana wa jacobo,,🤷.
Abraham,sara,isaack huwezi kuwaita waisrael maana hawa qualify
Kuna andiko lolote linalosapoti haya uliyotaandiska hapa?ungeliambatanisha ili kujustfy
 
Kwa mujibu wa kitabu cha Kiyahudi torati ambayo Biblia nayo ikiambatana.... Vinasema kuwa Ibrahim alikuwa na watoto wawili ambao ni Isaka na Ismail. Ismail ni mtoto aliyepatikana nje ya Ndoa baada ya kukaa muda mrefu bila Sara kupata ujauzito, hivyo hajir akachaguliwa na sara hili wapate mtoto. Lakini badae baada ya kilio cha muda mrefu Mungu akawabariki mtoto naye wakamwita Isaka, na Ibrahim akampenda sana huyo mtoto badae Mungu akataka Isaac atolewe sadaka kwa sababu alimtii Mungu ikabidi aende kumtoa Isaka sadaka kwa moyo mmoja, lakini badae akatokea malaika na kumuonesha kondoo kama mbadala... Kutokana na kitendo cha utiifu na imani kwa mungu na kuthubutu kwenda kumtoa Mwanae aliyempenda na aliyempata kwa shida basi Mungu akambariki na kumwambia utakuwa baba wa mataifa mengi na mataifa yatatoka kwako
Okay tumekubali kwamba ismaily ni mtoto wa nje ya ndoa, Kwa hiyo baba wa mataifa. Mengi alifanya dhambi ya kuzini
 
Hahaaaaaaa, Muhaya unatudanganya bwana. Hao waarabu hapo Misri na nchi jirani za afrika Magharibi walikuja majuzi tu kipindi cha utawala wa Ottoman Empire.

Hariri hakuwa mwarabu, Hariri alikuw mmisri wa kale mwenye asili ya Afrika. Ngozi nyeusi mkuu. Ebu fuatilia uzi humu unaoeleza hilo ikihusisha pia ushahid toka michoro ya Mafarao kwenye Pyramid za Giza pia hao mummies wanaofukuliwa sasa wanaoonekana wakiwa na ngozi nyeusi.
Kwa hiyo wakush Ina bidi wawafurushe waarabu wa misri ya Leo 😂
 
Kuna majaribu mengine ni kipimo cha imani
Mungu amuambie mzazi amuue mtoto wake , ili kuonyesha upendo Kwa mungu,

Kwanini mungu awe na wivu wakutaka kupendwa kiasi hiki, mpaka kutoa Amri wengine wauwawe Kwa ajili Yake , Haya ni mapenzi ya namna Gani?.

kwani yy siana jitosheleza Kwa kila kitu,
 
Wahuni walipotosha historia kwa manufaa yao

Bible inasema Ibrahimu alizaa na binti wa Misri(afrika ya watu weusi wana wa ham) na kama iaminikavyo kuwa ibrahimu alikuwa muisrael hao watu weupe, je inakuaje mtoto huyo ishmael aje kuwa mwarabu wakat baba alizaa na binti mweusii?

Ukweli ni kuwa Ishamael alikuwa mtu mweusi ambaye asili yake ni afrika kiufupi kwa leo tungemuita Afro-Asiatic yaan mwafrika mwenye asili ya asia(mtu mweusi) kwa kuongelea hili inatosha kuleta maana kwamba ishamael sio baba wa uislam wala sio baba wa waarabu maana mtu mweusi na uarabu wapi na wapi? Mtu mweusi na uislam wap na wapi?

Wazungu na waarabu walishirikiana kuchafua historia ya mtu mweusi kwa manufaa yao, alafu hiyo nchi mnayoita israel haijawai kuwepo hapo kabla ya kuundwa na umoja wa mataifa miaka ya 1947-8 kabla ya kuundwa hiyo ardhi ilikuwa mali ya watu weusi baadae wakaja kujipachika waarabu hao wapalestina, then baada ya wazungu kuona ilo ni eneo la kimkakati kisiasa, kiuchumi na kijamii(kidini) basi waliamua kutumia historia ambayo haikuwahusu hao wanaojiita waisrael wa sasa bali ilikuwa historia ya waafrika wa zamani, wakaitumia historia hiyo kibiblia kuwa eneo hilo la ardhi ya palestina ni mali na urithi wa hawa majambazi wayahudi wa uongo, uku wakitumia biblia na baadhi ya maandiko ya dini yao ya kizushi, hapa ndipo ugomvi ulipoanza kuzuka.

Wazungu baada ya kujipa ardhi ya palestina kibabe walijenga mahekalu feki, makaburi feki ya watu wa kale hiyo yote ilikuwa target ya kutengeneza historical sites za uongo kama ushahidi kuwa wao waliishi hapo.

Jamani huu mgogoro huwezi kuuelewa kama unatumia dini kuelezea, dini hazijui kitu maana zimekuja juzi tu alafu dini hizo hizo ndizo wamezitumia kama njia ya wao kujimilikisha historia zisizo zao.

Myahudi kuchukiwa ilo eneo ni sababu kavamia eneo ambalo si lake, mkitaka mujue kweli, rudi ufuatilie historia ya kweli kabla ya miaka 1800 kurudi nyuma iyo ardhi ilikaliwa na nani? Na hata huo mwaka wanaodai Yesu aliishi hapo yerusalem ukifuatilia kihistoria utagundua kuwa ni Uongo Hakuna ushahidi wa Yesu kuishi israel ya sasa wala manabii na hao mitume kuishi hiyo israel ya sasa.

Pia hao wayahudi wa uongo hawana historia yoyote ya kuwekwa Utumwan zaid ya ile propaganda ya wayahudi 300 kuteswa na hitra huku baadhi ya wazungu wakabadiri historia na kusema kuwa wayahud zaid ya milion 3 waliteswa na kuuliwa na hitra jambo ambalo si kweli.

Dini ni nyenzo ama siraha wanayoitumia wazungu kupotosha historia nzima ya dunia bila kusahau propaganda za media na masomo ya uongo.

90% ya habari tunazozijua ni uongo, dunia imejaa uongo kila mahala, kuanzia mashuleni, mpaka ktk dini ni uongo mkubwa, historia ya Akina ibrahimu imechakachuliwa mungejitahidi kusoma ukweli halisi mngegundua kuwa hao watu wa middle east hawana ushirika wala uhusiano wowote na matukio+historia za biblia hata chembe,

Historia za biblia kuanzia mwanzo mpaka kitabu cha mwisho matukio yote hayakutendeka huko middle east na hiyo israel ya uongo, bali matukio hayo yalitendeka ndani ya continent la Afrika, baadae ndipo hao mashetan watu weupe wakabadili historia kwa manufaa yao na kuwaleta hizi dini na siasa mnazobishana kila siku na kuuwana ninyi kwa ninyi huku wao wakizidi kutajirika kwa upumbavu wenu.

Topic za kushindania Udini ni upumbavu mkubwa.
 
Tupeane elimu kidogo, kuna watu wanachanganya mambo. Hapa tufundishane jambo moja. Kitu cha kwanza kabisa watu wanachokichanganya ni kuhusu Ibrahim, wengi wanasema Ibrahim alikuwa Mwarabu, ndugu yangu, nikwambie tu kwamba jamaa hakuwa Mwarabu.

Ibrahim baada ya kuzaa na kijakazi ambaye alikuwa Mwarabu, inamaanisha damu yake ilichanganyika na ya Kiarabu na ndiyo maana tunasema Ishmael ni baba wa Waarabu kwa sababu mama yake alikuwa Mwarabu.

Nchi za Kiarabu ambazo zipo kwenye umoja ni hizi, Algeria, Bahrain, Iraq, Jordan, Kuwait, Djibout, Saudi Arabia, Tunisia, United Arab Emirates, Yemen, Somalia, Sudan, Syria, Comoros, Misri, Maurtania, Qatar na Palestina.

Kwa nini Waarabu wanamchukia Israel? Ni kwa sababu si Mwarabu mwenzao. Na hao ndiyo wa kizazi cha Ibrahim. Kwa hiyo kama ulikuwa unahisi Ibrahim alikuwa Mwarabu, futa hiyo akilini mwako.

Hata Iran sio Waarabu, najua wengine mtakuwa hamlijui hili kwa undani. Miongoni mwa nchi za Kiarabu, Iran hayupo kwa sababu yeye si Mwarabu.

So Israel na Waarabu ni baba mmoja ila mama tofauti. Ibrahim alizaa na Muisrael mwenzake kwa kipindi hicho ilikuwa bado haijaitwa Israel na mtoto wake kuitwa Isaka ila yule aliyezaa na kijakazi ambaye ni Mwarabu anaitwa Ishmael. Tatizo kubwa la vita baina ya Mwarabu na Israel ni hapa.

Kama Israel angekuwa Mwarabu, leo usingesikia vita vinavyoendelea huko. Na mara zote Israel anawaambiaga kwamba nchi zote za Uarabuni ni mali ya Israel na ndiyo maana kila anapokwenda kupiga, anachukua ardhi na kutanua nchi yake.

Israel walipewa nchi ndogo sana wakae baada ya kutawanywa na Adolf Hitler, baada ya kuanza kurudi, wakaitaka nchi yao, lakini kwa bahati mbaya waliwaona Waarabu washajigawia ardhi yao. Walichokifanya ni kuanza kupigana nao.

Kama unakumbuka Umoja wa Mataifa uliingilia kati, ulichukizwa na kitendo cha Israel kuwapiga Waarabu, walichokifanya, wakawapelekea Biblia ambayo kwa nyuma kuna ramani ya Israel tangu enzi za Musa. Wakawaonyesha na kuwaambia kwamba nchi zote za Uarabuni ni Israel, tutakapokuwa wengi, tutaendelea kupiga na kuirudisha nchi yetu.

So jua hili. Ibrahim hakuwa Mwarabu. Musa hakuwa Mwarabu. Suleimani mtoto wa Daudi na baba yake huyo hawakuwa Waarabu. Ni Waisrael ambao bado wanaendelea kupigana na Waarabu ili wachukue nchi yao iliyowafanya waondoke Misri.

Uzao wa Ibrahim ndiyo uliomleta Yusufu ambaye akawachukua Waisrael kwenda kuishi Misri. Maisha yalikuwa ya raha sana, watu waliionjoi maisha lakini baada ya mfalme huyo kufa, ndipo akaja mfalme mwingine ambaye sasa hakuwataka Waisrael, akawafanya watumwa wake.

Wakafanyishwa kazi. Baadaye ndipo Musa akazaliwa ndani ya ardhi ya Kiarabu. Akapewa jukumu la kuwatoa Israel kutoka hapo Misri kwenda kwao. Wakati huo ndio ambao nao Waarabu walikuwa wamejinyakulia nchi, tena walikuwa ni watu wakubwa kimuonekano.

Musa akaanza mchakato wa kuwatoa Israel Uarabuni na kuwapelekea Israel. Waliishi Misri kwa miaka 400. Wakaondoka na kwenda Misri, na walitumia miaka 40.

Musa hakuingia Israel, alikufa jangwani na Mungu kumzika. Wale waliofanikiwa kuingia huko Israel ndio walioendelea kuipambania ardhi yao mpaka leo hii.

Hapa kuna jambo moja.

Vita ya Israel na Waarabu itapamba moto hapo baadaye. Itapigwa vita kali sana. Sasa kwa kuwa Israel ataonekana kuwa kiburi na mwenye nguvu sana, dunia nzima itaanza kumcharaza. Huyu Marekani anayeonekana kuwa karibu na Israel naye atamgeuka, kila nchi duniani itamgeuka na kumpiga.

Mwisho wa siku baada ya kuona wanapigwa sana, watakimbilia mpaka kwenye mlima ule aliopaa Yesu, wataomboleza na kulia, hapo ndipo Yesu atashuka kuimaliza vita hiyo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa kila kitu.
Umesema kweli tupu, Mungu akubariki sana. Mungu alisema hivi:-
Yoshua 1:4 SUV
"Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu". Bado taifa teule halijachukua eneo lake lote linao kaliwa na Wafilisti.
 
Kwa sababu chimbuko la uislamu linaanzia kwake
Sidhani kama ni kweli! Ishmaeli hana uhusiano wo wote na Uislam, wala Ishmael hakuwa Mwarabu, alikuwa Mwebrania kufuata ukoo wa baba yake Ibrahim.
Uislam umeletwa na Muhamaad kwenye karne ya 7 na 8, miaka zaidi ya 2000 kutoka kwa Ishmaeli.
 
Wenye dini zao
Screenshot_20231005-063049.jpg
 
Tupeane elimu kidogo, kuna watu wanachanganya mambo. Hapa tufundishane jambo moja. Kitu cha kwanza kabisa watu wanachokichanganya ni kuhusu Ibrahim, wengi wanasema Ibrahim alikuwa Mwarabu, ndugu yangu, nikwambie tu kwamba jamaa hakuwa Mwarabu.

Ibrahim baada ya kuzaa na kijakazi ambaye alikuwa Mwarabu, inamaanisha damu yake ilichanganyika na ya Kiarabu na ndiyo maana tunasema Ishmael ni baba wa Waarabu kwa sababu mama yake alikuwa Mwarabu.

Nchi za Kiarabu ambazo zipo kwenye umoja ni hizi, Algeria, Bahrain, Iraq, Jordan, Kuwait, Djibout, Saudi Arabia, Tunisia, United Arab Emirates, Yemen, Somalia, Sudan, Syria, Comoros, Misri, Maurtania, Qatar na Palestina.

Kwa nini Waarabu wanamchukia Israel? Ni kwa sababu si Mwarabu mwenzao. Na hao ndiyo wa kizazi cha Ibrahim. Kwa hiyo kama ulikuwa unahisi Ibrahim alikuwa Mwarabu, futa hiyo akilini mwako.

Hata Iran sio Waarabu, najua wengine mtakuwa hamlijui hili kwa undani. Miongoni mwa nchi za Kiarabu, Iran hayupo kwa sababu yeye si Mwarabu.

So Israel na Waarabu ni baba mmoja ila mama tofauti. Ibrahim alizaa na Muisrael mwenzake kwa kipindi hicho ilikuwa bado haijaitwa Israel na mtoto wake kuitwa Isaka ila yule aliyezaa na kijakazi ambaye ni Mwarabu anaitwa Ishmael. Tatizo kubwa la vita baina ya Mwarabu na Israel ni hapa.

Kama Israel angekuwa Mwarabu, leo usingesikia vita vinavyoendelea huko. Na mara zote Israel anawaambiaga kwamba nchi zote za Uarabuni ni mali ya Israel na ndiyo maana kila anapokwenda kupiga, anachukua ardhi na kutanua nchi yake.

Israel walipewa nchi ndogo sana wakae baada ya kutawanywa na Adolf Hitler, baada ya kuanza kurudi, wakaitaka nchi yao, lakini kwa bahati mbaya waliwaona Waarabu washajigawia ardhi yao. Walichokifanya ni kuanza kupigana nao.

Kama unakumbuka Umoja wa Mataifa uliingilia kati, ulichukizwa na kitendo cha Israel kuwapiga Waarabu, walichokifanya, wakawapelekea Biblia ambayo kwa nyuma kuna ramani ya Israel tangu enzi za Musa. Wakawaonyesha na kuwaambia kwamba nchi zote za Uarabuni ni Israel, tutakapokuwa wengi, tutaendelea kupiga na kuirudisha nchi yetu.

So jua hili. Ibrahim hakuwa Mwarabu. Musa hakuwa Mwarabu. Suleimani mtoto wa Daudi na baba yake huyo hawakuwa Waarabu. Ni Waisrael ambao bado wanaendelea kupigana na Waarabu ili wachukue nchi yao iliyowafanya waondoke Misri.

Uzao wa Ibrahim ndiyo uliomleta Yusufu ambaye akawachukua Waisrael kwenda kuishi Misri. Maisha yalikuwa ya raha sana, watu waliionjoi maisha lakini baada ya mfalme huyo kufa, ndipo akaja mfalme mwingine ambaye sasa hakuwataka Waisrael, akawafanya watumwa wake.

Wakafanyishwa kazi. Baadaye ndipo Musa akazaliwa ndani ya ardhi ya Kiarabu. Akapewa jukumu la kuwatoa Israel kutoka hapo Misri kwenda kwao. Wakati huo ndio ambao nao Waarabu walikuwa wamejinyakulia nchi, tena walikuwa ni watu wakubwa kimuonekano.

Musa akaanza mchakato wa kuwatoa Israel Uarabuni na kuwapelekea Israel. Waliishi Misri kwa miaka 400. Wakaondoka na kwenda Misri, na walitumia miaka 40.

Musa hakuingia Israel, alikufa jangwani na Mungu kumzika. Wale waliofanikiwa kuingia huko Israel ndio walioendelea kuipambania ardhi yao mpaka leo hii.

Hapa kuna jambo moja.

Vita ya Israel na Waarabu itapamba moto hapo baadaye. Itapigwa vita kali sana. Sasa kwa kuwa Israel ataonekana kuwa kiburi na mwenye nguvu sana, dunia nzima itaanza kumcharaza. Huyu Marekani anayeonekana kuwa karibu na Israel naye atamgeuka, kila nchi duniani itamgeuka na kumpiga.

Mwisho wa siku baada ya kuona wanapigwa sana, watakimbilia mpaka kwenye mlima ule aliopaa Yesu, wataomboleza na kulia, hapo ndipo Yesu atashuka kuimaliza vita hiyo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa kila kitu.
[emoji23][emoji23][emoji23]dah aisee...
 
Back
Top Bottom