Black listed
Senior Member
- Apr 6, 2023
- 181
- 260
Hii sio kweli, Isaka na Ishmael hawakuzidiana sana kiumri. Wakati Sarah (mkewe Ibrahim) anamfukuza kijakazi wake na mwanawe, Ishmael alikuwa bado ndogo sana.Isaac alizaliwa miaka 14 baada ya ishmael,,wakati isaack na ismael wanagombana na kupelekea hajira na mwanawe kufukuzwa,tayari isaack alikua na walau miaka 5,🤗which means ishmael alikua karibu 20 years old
Maandiko yanasema, baada ya kufukuzwa, walitembea umbali mrefu sana, na wakiwa njiani waliishiwa chakula na maji. Ilifika wakati, mama na mtoto (Ishmael) walishikwa na njaa na kiu kali, na kuishiwa na nguvu kiasi cha mama kuona mwanaye anakufa.
Mama alikata tamaa, na akamlaza mtoto chini akisubiri afe. Ndipo Mungu alifanya maajabu, mama alipogeuka tu akaona chemchemi ya maji yakibubujika. Akachukua kibuyu chake, akateka maji, akanywa yeye na mengine akamnywesha mwanaye. Hapo wakapata nguvu, mama akambeba mtoto na kuendelea na safari.
Kwa maelezo hayo, unaweza kuona kuwa Ishmael alikuwa bado mdogo, maana alibebwa na mama yake wakati wote wa safari. Tunaweza kusema, wakati huo, Isaka alipozaliwa, Ishmael hakuzidi miaka miwili.