Ukweli kuhusu Simba Sports Club

Ukweli kuhusu Simba Sports Club

Hichilema

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
1,608
Reaction score
1,687
Natumaini u buheri wa afya.

Kumekuwa na mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uchezaji wa Simba. Ukweli ni kwamba baada ya Simba kujitathimini kwa muda mrefu imeamua kubadili falsafa yake ya kupiga pasi nyingi za nyuma na madoido yasiyokuwa na tija.

Tathimini ilionesha ili timu ifike mbali kwenye mashindano ya Afrika inapaswa ianze kucheza direct football. Mpango huu siyo mpya na haukuanzia kwa mwalimu Robertinho, umeanza kwa kumleta mwalimu Pablo Franco Martin na Zoran na sasa Robertinho.

Kutokana na kikosi kilichokuwepo kabla ya kuja Pablo, Zoran na Robertinho baadhi walionekana hawaendani na direct football hasa kufanya pressing mfano Phiri na Chama ambao wote hawakupendwa na Zoran na hata Robertinho.

Mpango uliofuata ni kuanza kuleta wachezaji wenye vimo virefu. Inonga na Sadio K na sasa Fabrice. Kabla ya hapo timu ilicheza vizuri pira biriani lakini inaambulia kupigwa goli 5 goli 4 kwenye Champions League na bila shaka kwa misimu hii miwili iliyopita kuna unafuu unaonekana timu imetolewa kwa mikwaju ya penalti.

Timu nyingi zinazocheza mpira wa kufurahishana hazina chao Afrika mfano Mamelody na Belouzdad. Kwa wale wanaosema Simba mbovu mara timu haipigi pira biriani wasahau labda kama itakuwa ni njia ya kupoteza muda baada ya kushinda goli nyingi.
 
Huo ni mtego na utaziumiza timu nyingi zisipojihadhari

Mtego kwa dakika zote 90?? Inapotokea time haichez mpira uliotegemewa, hata kama ni shabiki lialia wa Simba, kubali tu mapungufu na uamini kuna siku mtayarekebisha.

Singida FG alikukalia kooni MECHI NZIMA, Yanga nae hivyo hivyo, au ndo ulikuwa UNAWATEGA? Acha visingizio vya kitoto mkuu.
 
Mtego kwa dakika zote 90?? Inapotokea time haichez mpira uliotegemewa, hata kama ni shabiki lialia wa Simba, kubali tu mapungufu na uamini kuna siku mtayarekebisha….!!! Singida FG alikukalia kooni MECHI NZIMA, Yanga nae hivyo hivyo, au ndo ulikuwa UNAWATEGA..??? Acha visingizio vya kitoto mkuu…!!!
NAongea ninachokijua, siko hapa kuongea mipasho. Inaonekana una stress. Muda utaongea
 
Unaweza kuwa na hoja ila naona kama umezunguka ila nia ya uzi huu ni kusema Phiri hafai kuwepo tena pale Simba! Phiri hakuwepo kipindi cha Pablo, alikuja Simba June 2022 na pia Zoran alikuja muda huo huo akaondoka baada ya miezi 2 tu tena kama sikosei msimu ukiwa haujaanza. Msimu ulivyoanza, Phiri akawa kinara wa magoli.

Phiri hakuwepo wakati Simba inafungwa goli 5 5 ila kina Kapombe, Zimbwe, Manula, Mzamiru, Boko walikuwepo!
 
Simba sio mbovu tatizo watu wanailinganisha na Yanga lazima itaonekana mbovu tu.
Yanga wanacheza direct football, lakini unaona wanavyomiliki dimba.?
Yanga walipocheza na Al Hilal waliachwa wachezee mpira wanavyotaka mwisho wa siku watu wanacheza kimkakati wakaitoa, wakabaki wanalialia mpira walicontrol wao kama walivyokuwa wanalialila baada ya mechi ya ngao. Hata mechi ya kwanza na Club Africain na mechi ya Simba ya 2-0, Yanga waliachwa wachezee mpira watakavyo huku wenzao wanatafuta matokeo.

Hizi habari za Yanga kutaka kucheza mpira wa kasi na direct football zimeanza baada ya kuiangalia Simba na kumsikia Robertinho anataka nini. Niliwahi kusema huo ni mpira wa Uingereza, ni mpira wa matokeo zaidi. Cha kushangaza tunauangalia kwenye TV na kuupenda ila ukichezwa hapa tunaukataa. Mimi binafsi sikuwa napenda Simba ilivyokuwa inacheza sana back passes zisizo na malengo.
 
Acha Uongo, YANGA kabla ya kuja Nabi ilikuwa ndo mfumo wao, kusema eti wanataka kuiga Kwa Robertinho ni uongo
 
Mtego kwa dakika zote 90?? Inapotokea time haichez mpira uliotegemewa, hata kama ni shabiki lialia wa Simba, kubali tu mapungufu na uamini kuna siku mtayarekebisha….!!! Singida FG alikukalia kooni MECHI NZIMA, Yanga nae hivyo hivyo, au ndo ulikuwa UNAWATEGA..??? Acha visingizio vya kitoto mkuu…!!!
Hao walioikalia Simba kooni (Singida na Yanga) waliifunga Simba?
 
Acha Uongo, YANGA kabla ya kuja Nabi ilikuwa ndo mfumo wao, kusema eti wanataka kuiga Kwa Robertinho ni uongo
Kipindi cha Nabi Yanga waliridhika na mpira wa pasi nyingi maana ulikuwa unawapa matokeo kwenye ligi ya ndani ingawa mara nyingi ushindi ni wa goli 1 au zikizidi 2. Haya matamanio ya kutaka kucheza mpira wa kasi yamekuja baada ya Robertinho na kuona jinsi gani Simba inautumia mfumo huo hasa kimataifa kupata matokeo.

Kama unabisha nionyeshe mtu wa Yanga aliyewahi kuongelea habari za mpira wa kasi au direct football kabla Robetinho hajaja.
 
Yanga walipocheza na Al Hilal waliachwa wachezee mpira wanavyotaka mwisho wa siku watu wanacheza kimkakati wakaitoa, wakabaki wanalialia mpira walicontrol wao kama walivyokuwa wanalialila baada ya mechi ya ngao. Hata mechi ya kwanza na Club Africain na mechi ya Simba ya 2-0, Yanga waliachwa wachezee mpira watakavyo huku wenzao wanatafuta matokeo.

Hizi habari za Yanga kutaka kucheza mpira wa kasi na direct football zimeanza baada ya kuiangalia Simba na kumsikia Robertinho anataka nini. Niliwahi kusema huo ni mpira wa Uingereza, ni mpira wa matokeo zaidi. Cha kushangaza tunauangalia kwenye TV na kuupenda ila ukichezwa hapa tunaukataa. Mimi binafsi sikuwa napenda Simba ilivyokuwa inacheza sana back passes zisizo na malengo.
Ulikuwa na hoja ila hapo kwa yanga kubadilika baada ya kuiona simba na kumsikia robetinho umekosea pa kubwa sana
 
Kipindi cha Nabi Yanga waliridhika na mpira wa pasi nyingi maana ulikuwa unawapa matokeo kwenye ligi ya ndani ingawa mara nyingi ushindi ni wa goli 1 au zikizidi 2. Haya matamanio ya kutaka kucheza mpira wa kasi yamekuja baada ya Robertinho na kuona jinsi gani Simba inautumia mfumo huo hasa kimataifa kupata matokeo.

Kama unabisha nionyeshe mtu wa Yanga aliyewahi kuongelea habari za mpira wa kasi au direct football kabla Robetinho hajaja.

Kocha Plujm alikua akiuishi.
 
Natumaini u buheri wa afya.
Kumekuwa na mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uchezaji wa Simba. Ukweli ni kwamba baada ya Simba kujitathimini kwa muda mrefu imeamua kubadili falsafa yake ya kupiga pasi nyingi za nyuma na madoido yasiyokuwa na tija.
Tathimini ilionesha ili timu ifike mbali kwenye mashindano ya Afrika inapaswa ianze kucheza direct football. Mpango huu siyo mpya na haukuanzia kwa mwalimu Robertinho, umeanza kwa kumleta mwalimu Pablo Franco Martin na Zoran na sasa Robertinho.
Kutokana na kikosi kilichokuwepo kabla ya kuja Pablo, Zoran na Robertinho baadhi walionekana hawaendani na direct football hasa kufanya pressing mfano Phiri na Chama ambao wote hawakupendwa na Zoran na hata Robertinho.
Mpango uliofuata ni kuanza kuleta wachezaji wenye vimo virefu. Inonga na Sadio K na sasa Fabrice. Kabla ya hapo timu ilicheza vizuri pira biriani lakini inaambulia kupigwa goli 5 goli 4 kwenye Champions League na bila shaka kwa misimu hii miwili iliyopita kuna unafuu unaonekana timu imetolewa kwa mikwaju ya penalti. Timu nyingi zinazocheza mpira wa kufurahishana hazina chao Afrika mfano Mamelody na Belouzdad. Kwa wale wanaosema Simba mbovu mara timu haipigi pira biriani wasahau labda kama itakuwa ni njia ya kupoteza muda baada ya kushinda goli nyingi.
Sawa jifunze kupangilia mwandiko. Hausomeki kabisa
 
Kipindi cha Nabi Yanga waliridhika na mpira wa pasi nyingi maana ulikuwa unawapa matokeo kwenye ligi ya ndani ingawa mara nyingi ushindi ni wa goli 1 au zikizidi 2. Haya matamanio ya kutaka kucheza mpira wa kasi yamekuja baada ya Robertinho na kuona jinsi gani Simba inautumia mfumo huo hasa kimataifa kupata matokeo.

Kama unabisha nionyeshe mtu wa Yanga aliyewahi kuongelea habari za mpira wa kasi au direct football kabla Robetinho hajaja.
Wewe jamaa ni muongo sana. Yanga na Simba ni timu zinazopishana katika falsafa. Simba falsafa yao ni soka la pasi nyingi huku Yanga falsafa yao ni kutumia nguvu na kasi na mifumo ya Yanga mara nyingi hutumia mawinga kupata magoli. Unasema eti Simba imepata mafanikio kimataifa kwa mpira wa kasi wa Roberinho. Kwani kipindi cha mpira biriani Simba hawakufanya vizuri? Hawakufika hatua sawa sawa na ya Roberinho?
 
Back
Top Bottom