Ukweli kuhusu Simba Sports Club

Kwenye mechi hizo ulizotaja nani alikuja kushinda baadaye,kweli super chura
 
Jiulize hizo zilizoizidi zilishinda? Na kama hazikushinda ujue ndo mbovu zaidi

Hazikushinda. Je, Simba nae alishinda within hizo dakika 180..?? Au kwa lugha nyepesi tuseme WOTE WABOVU…?? Kama utasema walishinda kwa sababu ya zile penalti, sidhani kma ni matarajio ya timu kubwa kma Simba kusubiri penalti.
 
Mtego kivipi? Kuna direct football na poor performance. Kama timu inazidiwa hadi mashambulizi direct football gani hiyo muda wote watu langoni kwako tu?
Morinho alipokuwa Chelsea alichukua makombe kwa kupaki basi ,na mda wote wanashambuliwa mara anafanya counter na goli halirudi,vile vile Huwa unaangalia mechi za Atletico Madrid?
 
Morinho alipokuwa Chelsea alichukua makombe kwa kupaki basi ,na mda wote wanashambuliwa mara anafanya counter na goli halirudi,vile vile Huwa unaangalia mechi za Atletico Madrid?
Kama ndio mbinu inayolipa kwanini Atletico hawana mafanikio katika mashindano ya ndani na ya kimataifa? Kwanini hiyo mbinu Morrinho haimpi mafanikio kama ndio mbinu bora au Morrinho kastafu ukocha baada ya kutoka Chelsea? Tumeona timu zinazocheza falsafa ya total football ndio zikipata mafanikio kuliko wapaki treni. Mpira ni mchezo wa makosa, kuruhusu kushambuliwa kwa sana kunakukufanya kulazimishwa kufanya makosa. Al Ahly wametawala soka la Africa, je kutawala kwao kumetokana mpira wa kupaki basi?
 
Kila mechi ina mbinu zake,unaposema Morihno na Simeone hawana mafanikio unadhani kuchukua ubingwa EPL ni kitu rahisi,pia Atletico washachukua makombe ila inatokea ukicheza mfumo flani kuna kipindi timu zingine zitakuzoea na kujua madhaifu,mechi ya Marudio club bingwa mamelodi vs Wydad bila shaka uliangalia, aliyemiliki sana ndo alipigwa.

We unataka Simba icheze ule mfumo waliocheza na Raja Casablanca ?mnamiliki mpira mda wote lakini mnapigwa
 
Wakati mwingine kama hamna vya kuzungumza ni bora mkapiga kimya. Mnaongea uongo mnadhani wote ni makolo kolo tu. Yan eti ujio Robertinho ndio amesababisha tuupende mpira wa kasi🤣🤣🤣

Kati ya huyo Robertinho na Nabi nani alitangulia kuja TZ? Kabla ya Mbrazil kuja Yanga ilikua inachezaje?
 
Ulifanya kazi pia na Waydad, Yanga au hukuangalia?
 
Mpira wa anao anao sio mbaya,ila una elekea wapi mf Messi na Bernado ni wachezaji ambao wanao wanao sana ila output yao siku zote inakuwa ni nzuri,mfano mwengine Kibu, Gervinho wa Arsenal nk nao wanao wanao sana ila output yao inakuwa ni mbovu.

Mayele ataendelea kufunga magoli ya aina yote kuanzia solo goal mpaka ya kutengewa.
 
Muda utazidi kuniprove right. Utafika muda huu uzi watu wataukimbia
 
Mwisho wa siku nani alinufaika na matokeo?
 
Vipi bado mnaamini Mayele ataendelea kufunga magoli ya aina zote kama ulivyosema hapa?
 
Vipi bado mnaamini Mayele ataendelea kufunga magoli ya aina zote kama ulivyosema hapa?
Bado ni mzuri kwangu na atafunga akiacha ujinga wake wa kuhisi katupiwa vitu vya kushirikiana.
 
Bado ni mzuri kwangu na atafunga akiacha ujinga wake wa kuhisi katupiwa vitu vya kushirikiana.
Nilikwambia huyo Mayele pamoja na uzuri wake ni mfumo ulioundwa pale Yanga ndiyo ulikuwa unambeba, mfumo uliokuwa tayari kumvumilia hata akipoteza nafasi 5 akafunga ya 6, mfumo hata akicheza mechi 4 bila kufunga mnaona siyo dili ila akienda timu nyingine atapata tabu.

Inaonyesha ameona dalili za kuachwa na Pyramids na labda kuna kipengele katika makubaliano kinachoipa Yanga upendeleo wa kwanza kabla ya timu nyingine iwapo Pyramids wataamua kumuacha na yeye labda hataki kurudi Yanga. Kwa hiyo anajenga mazingira ya kusema pale siyo sehemu salama kwangu.
 
Mayele ni mzuri kudrop kawaida,toka huko alipo toka alikuwa anafunga,kaja Yanga misimu miwili plus Confederation Tores,Shevchenko walivyo drop Chelsea hawa kung'ara sehemu yoyote ila haiondoi umahili wao.Mayele kwangu bado ni mzuri sema tu yy mwenyewe kaamua kijivuruga kwa mawazo ya kijinga.
 
Unaniuliza mimi au niwaulize nyie mliofanya replacement ya Robertinho kutokana na aina yake ya mpira.
Nilichokisema ni kwamba Simba imeachana na mpira wa kujifurahisha na kuelekea kwenye mpira was malengo toka imlete Pablo na waliomfuata watu wakadhani namtetea Robertinho
 
Bado upo kwenye hali ya kutokubaliana na hali ila kiufupi Mayele anahitaji mfumo unaoweza kuwa tayari kumvumilia na kumpa playtime ya kutosha bila kujali mchango wake uwanjani. Mayele siyo mchezaji wa kumpa dakika 10 halafu akupe matokeo kama ambavyo wamekuwa wanampa kwenye AFCON, hizo dakika 10 kama mfumo siyo sahihi kwake anaweza kugusa mpira mara moja tu.

Jiandae kisaikolojia maana dirisha lijalo unaweza kumkuta Azam FC ila afadhali mtakuwa mnashare kiwanja kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…